Huu ni mji wa Vwawa Mbozi ambako ndio nyumbani kwetu ambako wazazi wangu baada ya kustaafu kazi serikalini waliamua kuishi katika mji huu, na sisi pamekuwa ni nyumbani kwetu. |
Hiki ni kituo cha garimoshi cha vwawa mbozi |
Hapa Flora anaonekana akisubiri kwa hamu kubwa sana galimoshi (gogo) |
Baada ya muda garimoshi linaingia likitokea Kapirimposhi Zambia |
Flora akikusanya vifaa vyake ili kupanda ndani ya Treni, katika kituo kama hiki Garimoshi hutumia dakika 15 tu. |
Baada ya kuingia ndani na kupatiwa chumba ambacho atakitumia kwa kukaa na kulala Flora anaweka vitu vyake sawa |
Baada ya hapo tulielekea Buffet kwa ajili ya chakula na vinywaji. |
Hapa ni safari na muziki wa ala wewe ni kuweka vesi tu maana chuma kwa chuma ni mdundo tu. |
Kutoka Tunduma abiria walikuwa wachache sana tofauti na miaka ya nyuma ninavyokumbuka hapa hotelini ilikuwa ni hekaheka muda wote. |
Kwa mbali sana unaweza kukiona kiwanda cha saruji cha Songwe eneo hili ndilo wanalojenga kiwanja kikubwa cha kimataifa cha ndege. |
Sehemu nyingine unaweza ukatamani ushuke jinsi palivyotulia. |
hatimaye tulipita maeneo ya Mbalizi. |
Wakati mwingine hali ya hewa ilianza kuwa ya baridi wafanya kazi wa Tazara walitupatia mablanketi mazito kwa ajili ya kujikinga na baridi. |
Hapa ni mbeya mjini tulishuka kidogo kwa ajili ya kunyoosha miguu. |
Hii ni shule ya msingi majengo hapa ndipo nilipopata limu yangu ya msingi. |
Huyu ni rafiki yangu wa utotoni kabisa anaitwa Fredrick Lupembe hapa nilimtembelea ofisini kwake alifurahi sana tulipoonana maana tunapoteana sana |
Kama kawaida ukiongozana na Flora huwa anapenda sana kuchepukia kwenye vitu kama hivi kwa ajili ya kujenga mwili. |
Kwa kweli picha hii nimeipenda sana hebu nipige na na sanamu hii. |
Mandhari nzuri ya kuvutia inaonekana vizuri kabisa katika milima ya Mbeya. |
Picha hii inanikumbusha tulipotoka kuangalia makaburi ya ndugu zetu,sio kama tunaamini kitu fulani kuhusu wafu. Hapana tunakwenda kuangalia kwa sababu ya kutunza kumbukumbu. |
Hii picha ilipigwa mwenge kama kumbukumbu na sista wangu Rose na mjomba Munde katika duka la vinyago mwenge. |
Na hapa ni safari ya kuelekea mashambani. |
Flora akia na wifi yake Naomi wakiangalia maeneo ya mashamba ya familia. |
Kwa kweli wakati mwingine ulikuwa ni wakati wa furaha sana kuwa katika maeneo ambayo mnakuja kwa nadra sana kiasi cha mara moja kwa mwaka. |
Hii ni kumbukumbu ya kutambulisha mchumba Huyu ni mdogo wangu Cecilia Brown Mwakasege siku mchumba wake alipokuja kumchumbia nyumbani kwao Tabata Liwiti. |
Pembezoni kidogo ya Jiji la Mbeya picha hii nimeipiga nikiwa eneo la Majengo nimepiga kuelekea usawa wa Iyunga ambako iko stesheni ya galimoshi *TAZARA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni