sasa hivi ukipatwa na tatizo ndani ya kanisa hali huwa kama hivi |
Unapokuwa nje ya kanisa na ukatazama watu walioko ndani ya
kanisa unaweza ukakosea sana utakapodhani wako mahali salama penye upendo amani
na ushirikiano wa kutosha. Ukweli wala si hivyo! ijapokuwa ilitakiwa iwe hivyo. Ukiwa
ndani ya kanisa ndipo utakapoweza kuona vituko na wakati mwingine mambo ya kukatisha tamaa
kabisa Ashukuriwe Mungu ambaye ndiye mwokozi wetu vinginevyo kanisa limevamiwa mno na umbwa mwitu ambao Biblia ilishasema tangu awali. lakini kwa sababu wote tunamfahamu Yesu kwa mitazamo tofauti basi
kinachobaki ni kubanana humohumo. Hii ni kwa sababu anayetoa utumishi ni Bwana mwenyewe muumba
wa nchi na mbingu. wengine hata wakikukataa lakini kama Mungu amekukubali hakuna mwingine mwenye mbingu. ujasiri wetu unabaki palepale kwa sababu
hakuna kiumbe aliye juu ya Mungu.
ma freemason nao wapo waziwazi |
Naandika makala hii kwa hisia kali kwa sababu
nimeona na kushuhudia mambo mengi sana yasiyopendeza ambayo pengine ni vigumu
kuamini kwamba waliyotenda haya ni watumishi wa Mungu huyuhuyu Yehova au wana
mungu mwingine anayepingana na Yehova.
Nafahamu kwamba maisha ya wokovu ni
mapambano kwa kila sekunde kama sisi tunavyopanga kuharibu kazi za shetani,na
shetani pia naye anapanga kuharibu kazi ya Mungu na kuwapiga watumishi wa Mungu kwa kila
mbinu.
watu watapenda pesa kuliko Mungu |
hata kama umeumizwa kiasi gani mshike sana Bwana Yesu usimuache |
watu
tunaofahamu jinsi walivyojitoa karibu maisha yao yote katika kumtumikia Mungu. na ikatokea kwa sababu yoyote wakaanguka katika dhambi, lakini baada ya kuanguka wakaonyesha toba hivi
ikitokea akakosea mahali fulani tunaweza
tukamnyanyasa kwa kosa moja na tukausahau utumishi wake uliotukuka? Nafahamu
kwamba siku hizi kanisa limevamiwa kama ambavyo biblia ilitabili kwamba
watatokea waalimu na manabii wa uongo,hao mimi sina shida nao na hata mawakala
wao hao wanapaswa kudhibitiwa bila huruma. Lakini ambao wamefanya kazi
ya Mungu kwa uaminifu na kwa Muda mrefu na tunawatambua na tunautambua
mchango
wao wa dhahiri na katika utumishi wao hawajawahi kufanya kosa au
kuanguka dhambini,lakini ikatokea si kwa wao kupenda bali kwa
kulazimishwa wakajikuta wameanguka dhambini, na wakajutia sana kosa hilo
na kuwa tayari kabisa kutengeneza ili warudi kumtumikia Mungu. je ni haki kuwashindilia na kuwalaani kwa kosa moja tu na kuwazuria utafikiri walishawahi kufanya kosa lingine.
hivi ina maana kwamba kuna baadhi ya dhambi ambazo hazina toba? au damu ya Yesu ilimwagika bure pale Golgotha. hii inaonyesha kwamba wapo watu ndani ya kanisa la Mungu wanapoona wenzao wanachapa kai ya Mungu kwa ufanisi wao wanaumia roho na kusaga meno kwamba kwa nini huyu anafanikiwa namna hii? hiyo roho sio ya Mungu aliye hai. Unaweza ukathibitisha hili kulingana na kasi ya kusambaratisha huduma ya mtumishi iliyo ndani yake. utona watu ile roho ya kumsaidia mtu ili atengeeze inakuwa haipo bali roho ya kusambaratisha na kuua kabisa,kwa maana ya kuhakikisha kwamba hata kama kuna neema kidogo haipati nafasi ya kuchipuka. hayo ndiyo macho waliyonayo watu wa mungu wa siku hizi. hii ni tofauti kabisa na macho ya Mungu. na Mungu angekuwa anatuangalia kama hivyo wanavyoangalia ndugu zetu hawa,sidhani kama kuna mtu ambaye angeokoka. maana hatukuokolewa kwa sababu tulikuwa wema mbele ya Mungu bali wingi wa dhambi zetu ndio uliozidish neema ya Mungu.Biblia inasema tukisema hatuna hatuna dhambi tunajidnganya wenyewe na wala kweli haimo ndani yetu,lakini tukiziungama yeye ni wa haki atatusamehe. Tusisahau kwamba ni Mungu ndiye anayetuchagua na ndiye muamui wa haki, wanadamu hawana haki ni wepesi wa kuongeza maneno wakidhani kwamba ndio wameshamaliza kazi,lakini Mungu anazo njia nyingi za kumuingiza Mtu darasani,inawezekana katikati ya matatizo haya Mungu akawa anataka kukuonyesha kwamba siku hizi watu wapo kanisani sio kama ulivyokuwa unawaona na wala sio kama ulivyokuwa unacheka nao. Inawezekana walikualika hata kufanya huduma kwao lakini kumbe ni kwa shinikizo tu la watu wanaokufahamu,kumbe mioyo yao haikuwa na wew kabisa.nawapa pole sana watumishi wote waliosalitiwa, kumbuka Biblia ilishasema watu watasalitiana na ndivyo vitu tunavyoviona ndani ya makanisa siku hizi. naamini kwamba Mungu mwenyewe atawasimamisha,maadamu ameshawabariki. hakuna atakyeweza kuwalaani. tena naamini baada ya hapo mtafanya utumishi mkubwa mara dufu kuliko mlioufanya hapo kabla. Ninapoandika haya nimeona kumekuwa na wimbi kubwa la furaha na vigelegele inaposikika kwamba mtumishi fulani ambaye amemtumikia Mungu kwa uaminifu sana ameanguka dhambini. Katika hali halisi ingefaa liwe jambo la huzuni sana na ikiwezekana kama majeruhi wa vita sisi wengine tungejitahidi kumhifadhi mahali salama tukimtibu jeraha zake ili akipona tuendelee kuwa naye katika mapambano,lakini sivyo wanavyofanya walokole wa siku hizi,unaweza ukapokea meseji za kukutia moyo kutoka kwa watu wasiomjua Mungu wakikuahidi kukuombea rehema kwa Mungu,lakini sio kwa wapendwa wao watatumiana meseji za kupongezana jinsi ambavyo umeanguka,la kushangaza Biblia inatuambia kwamba ni furaha mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja anapotubu,malaika wanafurahi wanampongeza Yesu na kuisifia damu aliyoimwaga msalabani jinsi inavyofanya kazi,kinyume cha andiko hili tunasema ni huzuni kubwa mbinguni kwa mteule mmoja tu anapoanguka dhambini na Yesu na malaika wake wanatuma damu ya upatanisho ili ikiwezekana watumie kila njia wamrejeshe,Yesu anasema hata kama una kondoo (watu)mia na mmoja akapotea waache wale 99 umfuate huyo mmoja. Lakini walokole hawaelewi hilo. Ninachojiuliza inakuwaje wewe habari inayomuhuzunisha Mungu wewe ndio inakufurahisha? Mimi nina mashaka na hiyo roho hata kama wewe ni mlokole wa zamani ndani ya kanisa. Ni jambo linalohuzunisha sana kuishi kwa kuviziana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni