TAFITI: MATUMIZI YA MTANDAO YANAIMARISHA KAZI ZA UBONGO KWA WAZEE
- Utafiti
uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonyesha kwamba matumizi ya
mtandao (internet) kwa wazee yanaimarisha utambuzi (cognition) na kazi za
ubongo wao. Utafiti huu ulihusisha wazee wa jinsia zote wenye umri kati ya
miaka 55 na 78. Wazee hawa waligawanywa katika makundi mawili. Moja
halikutumia mtandao na kundi jingine lilitumia mtandao mara kwa mara.
- Matokeo yalionyesha kwamba kazi za
ubongo wa wazee katika kundi ambalo lilikuwa linatumia mtandao mara kwa
mara ziliimarika zaidi kuliko za wazee katika kundi ambalo
halikutumia mtandao. Mabadiliko makubwa yalionekana katika sehemu za
ubongo zinazoshughulika na kumbukumbu (memory), lugha, kusoma na
upambanuzi.
- Matokeo haya yamewafurahisha
wanasayansi na wanasema kwamba pengine matumizi ya mtandao yanaweza kuwa
silaha mojawapo dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na upotevu wa
kumbukumbu na utambuzi kama vile Alzheimer.
-
- Sina uhakika kama kweli
wazee wa Kiafrika wanahitaji mtandao kuimarisha kazi za ubongo wao. Mimi
nadhani kwamba michezo kama vile bao,
drafti na hata kuhesabu ng’ombe wanaporudi nyumbani kila jioni ni mazoezi
tosha yanayoweza kusisimua kazi za ubongo, mazoezi ambayo yamesaidia
kuwafanya wazee wengi wa Kiafrika kubakia makini kiutambuzi (cognitively)
hata katika umri mkubwa. Sijui kama tulikuwa na wagonjwa wengi wa
Alzmeimer barani Afrika kabla ya hili wimbi jipya la utandawazi
tunaolishuhudia kwa sasa. Isitoshe, tulikuwa tunakula vyakula vya kiasili
na mfumo wetu wa maisha ulituwezesha kufanya kazi sana. Sasa mambo
yamebadilika sana na pamoja nayo magonjwa ya moyo, saratani, kiharusi na
si ajabu "dementia" na Alzheimer sasa yanatuandama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni