Mwaka mmoja baada ya kifo cha Gaddafi, familia yake
iko wapi?
22 Oktoba, 2012 - Saa 08:57
GM
Muamar Gaddafi
Mwaka mmoja baada ya kukamatwa na
kuuwa kwa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi tarehe 20 mwezi Oktoba
mwaka 2011, familia yake iko wapi?
Watoto watatu wa Gaddafi waliuawa
wakati wa harakati za mapinduzi akiwamo aliyekuwa mshauri wake wa usalama wa
kitaifa Mutassim Gaddafi, aliyefariki mikononi mwa waasi siku moja na babake.
Jamaa za Gaddafi wanaosalia
wamekumbwa na hali tata tangu kifo cha Rais huyo mwezi Oktoba, huku mjane wake
akitafuta hifadhi katika nchi jirani ya Algeria, mwanawe na aliyeonekana kama
mrithi wa wake Saif al-Islam yuko gerezani nchini Libya akisubiri kusikilizwa
kwa kesi yake kuhusu uhalifu wa kivita.
Safiya Gaddafi (Mjane wa gaddafi)
Safiya Farkash, mama wa watoto
wanane wa Gaddafi amekuwa akiishi nchini Ageria alikopewa hifadhi kwa sababu za
kibinadamu.
Pamoja na wanawe Ayesha na mwanawe
wa kambo kutoka kwa mke wa kwanza wa Gaddafi, waliingia nchini Algeria wakati
waasi walipoudhibiti mji mkuu Tripoli.
Amepewa hifadhi nchini humo na
kuwekewa vikwazo na serikali vya kutotoa matamshi yoyote ya kisiasa wala
kuingilia mambo ya Libya
Muhammad Gaddafi (Mwanawe)
Ikiwa mambo yangekwenda vinginevyo
Muhammad angehudhuria michezo ya Olimpiki 2012 kama mkuu wa kamati ya michezo
hiyo nchini Libya.
Badala yake, Muhammad mwanawe wa
kwanza Gaddafi, amekuwa nchini Algeria kwa mwaka mmoja sasa tangu kukimbilia
huko wakati waasi walipovamia mji wa Tripoli.
Ni mtoto wa mke wa kwanza wa
Gaddafi, Fathia, pia alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya taifa mawasliano ya simu
za mkononi nchni Libya.
Hatakikani na mahakama ya ICC na
hakuhusika pakubwa na kujaribu kuzima harakati za mapinduzi dhidi ya babake
mwaka jana.
Saif al-Islam Gaddafi (Mwanawe
Gaddafi)
Alionekana na wengi kama ,mrithi wa
babake, alikamatwa mwezi mmoja baada ya kifo cha babake, na amekuwa akizuiliwa
mjini Zintan tangu hapo.
Alihitimu kutoka chuo cha mafunzo ya
uchumi mjini London, na amekuwa sababu ya mvutano kati ya mahakama ya kimataifa
ya ICC ambako anakabiliwa na tuhumza za uhalifu wa kivita na maafisa wa sheria
nchini Libya ambao wanasisitiza kuwa lazima kesi yake iendeshwe nchini humo.
Idara ya sheria nchini Libaya kwa
sasa inaonekana kushinda katika mvutano huo, lakini hakuna tarehe rasmi ya
kusikilizwa kwa kesi yake, inaarifiwa kuwa jela ya kifahari ikiwa na uwanja wa
mpira wa vikapuni na mpishi wake binafsi vimeandaliwa kwa Saif mjini Tripoli
Saadi Gaddafi (Mwanawe Gaddafi)
Saadi Gaddafi, aliyekuwa mkuu wa
shrikisho la soka nchini Libya pamoja na kuongoza vikosi maalum, amepewa
hifadhi nchini Niger ambako anaishi katika makao makuu baada ya kutoroka
kupitia jangwa la Sahara.
Saadi ana sifa tata ambapo alikuwa
akicheza soka katika ligi ya Italia ingawa safari yake ilikatizwa baada ya
kuhusishwa na madawa haramu pamoja na maisha yake ya anasa.
Niger imekataa ombi la Libya
kumpeleka nchini humo huku waziri wa sheria akisema kuwa huenda akahukumiwa
kunyongwa.
Mnamo mwezi Septemba, shirika la
Polisi wa kimataifa Interpol lilitoa onyo ambalo litawaruhusu nchi wanachama
kamkamata Saadi.
Mwezi Disemba mwaka jana polisi
nchini Mexico walisema wana taarifa za kijasusi kuwa magenge ya wafanyabiashara
haramu ambao wanajaribu kumhamisha Saadi nchini Mexico kwa kutumia stakabadhi
bandia.
Hannibal Gaddafi (Mwanawe Gaddafi)
Hannibal ni mtoto wa tano wa Gaddafi
na Safiya Farkash. Inaamini alikuwa kwenye msafara wa magari ya Gaddafi
uliokuwa unaelekea nchini Algeria mwaka Jana .
Alikuwa anaongoza majeshi kulinda
eneo la Gharyan, Kusini mwa Tripoli, kabla ya waasi kudhibiti Tripoli.
Alisifika kwa tabia zake za anasa na
aliwahi kukamtwa akiwa amelewa wakati akiendesha gari aina ya Porsche mjini
Paris.
Alizua mgogoro wa kidiplomasia na
Uswizi baada ya kuwashambulia wafanyakazi wawili wa hoteli nchini humo na
kusababisha babake kuwafunga jela wafanyakazi kutoka nchini humo, na hata
kuiwekea nchi hiyo vikwazo.
Aisha Gaddafi (Mwanawe Gaddafi wa
kike)
Mwanawe pekee wa kike alipewa
hifadhi nchini Algeria pamoja na mamake na ndugu yake.
Siku tatu baada ya kuwasili Algeria,
alijifungua mtoto msichana na kumuita Safiya, jina la mamake.
Licha ya kuwekewa ulinzi mkali na
serikali ya Algeria, aliripotiwa hivi karibuni kuwataka watu nchini Libya
kupindua serikali ya sasa. Kwa usaidizi wa wakili wake Muisraeli, aliitaaka mahakama
ya ICC kuchunguza kifo cha babake
Aisha pia aliripotiwa kuunga mkono
Algeria katika mechi moja kati yake na Libya akisema kuwa serikali mpya ya
Libya haimwakilishi kivyovyote.
Hanaa Gaddafi (Mwanawe wa kuasiliwa)
Kanali Gaddafi alikuwa kwa muda
mrefu akidai kuwa Hanaa aliuawa katika shambulizi la Marekani mwaka 1986 wakati
akiwa na mwaka mmoja na nusu. Lakini tangu mapinduzi kufanyika, kumekuwa na
taarifa kuwa Hanaa yuko hai ingawa hajulikani aliko.
Tarehe 20 mwezi Oktoba, mwaka mmoja baada ya kifo cha Gaddafi, taarifa kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu zilisema kuwa Ibrahim alikamatwa na waasi mjini Tarhouna, maili arobaini kutoka mji mkuu.Maafisa wengine hata hivyo walishuku habari hizo.
Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu
kukamatwa kwake lakini baadaye ikasemekana kuwa uongo.
Alikuwa mwsemaji wa serikali na
kujulikana na vyombo vya habari vya kimataifa, alionekana mwisho mjini Tripoli
kabla ya waasi kuudhibiti mji huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni