Katika maombi ya dhati na ya kweli, mtu
hujiachia akawa wazi kujieleza na kutoa siri za moyo wake akijua Mungu ndiye msaada
wake na kimbillio lake. (Zab. 46:1-3),
|
“Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada
utakaoneekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari, maji yake yajapovuma na kuumuka,
ijapopepesuka milima kwa kiburi chake”.
Kwa kutambua ukuu wa Mungu na uwezo wake
ndipo ibada ya kweli toka vilindi vya moyo huanza, na mtu hushuka chini sana
katika ufahamu wake kumtambua Mungu ni nani na kumwabudu na kumpa sifa katika
maombi.
-
Katika
hali hiyo ya maombi humfanya mtu ajione si kitu bali astahiliye ni Mungu,
-
Ndipo
wengine huanguka chini na kugaragara kuonyesha upendo mbele za Mungu.
“Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli,
akaomba, akisema, Baba yangu ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke, walakini si
kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo wewe”. (Mathayo 26: 39)
Hata malaika wanaabudu na kuanguka mbele za
Mungu.
Yesu naye aliabudu hata akalia na kutoa
machozi ya damu akiomba.
“Naye kwa vile alivyokuwa alivyokuwa katika dhiki,
akazidi sana kuomba, hali yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini”
(Luka 22: 44)
Ayubu aliomba na kujiachia mikononi mwa
Mungu akisema, najua mtetezi wangu yu hai na pasipo mwili huu nitamwona Mungu.
“Lakini mimi najua mteteaji wangu yu hai, na kuwa
hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, lakini
pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu Nami nitamwona mimi nafsi yangu Na
macho yangu yatamtazama wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu”
(Ayubu 19: 25 -27)
Maombi huvuka mipaka ya mazingira ya mwili
wa nyama na kumleta mtu mahali alipo Mungu katika Roho kiasi kwamba muombaji
anakuwa na mazungumuzo na Mungu ana kwa ana.
Kama Paulo asemavyo ABA yaani Baba aliye
karibu naye kama mwana.
“Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo
hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani,
Baba”. (Warumi 8: 15)
Maombi kama haya yanafanyika katika dhana ya
kumtambua Mungu mwenyezi na ukuu wake, uweza wake, mamlaka na nguvu. Kisha moyo
wa mtu huyu huzama ndani ya ibada kwa maombi na kumwabudu, na kumpa sifa yeye
aliye juu Mungu mkuu. Ufahamu huu unamfanya mtu amheshimu Mungu na kumwabudu
kwa mshangao mkuu, na kumvuta kumpenda na kuichukia dhambi, kama Isaya
asemavyo,
“Mimi ni mtu mwenye midomo michafu na ninakaa kati
ya watu wenye midomo michafu”. (Isaya 6:1-5)
Petro naye akasema,
“Ondoka kwangu Bwana mimi ni mtu mwenye dhambi”. (Luka
5:8-9).
Heshima hii kwa Mungu huona utukufu wa Mungu
ulivyo mkuu na utakatifu wake ulivyo wa ajabu, na kushindwa kustahimili mbele
ya Mungu kisha kusema maneno hayo ya unyenyekevu katika maombi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni