Mwl:
Furaha Amon
Utangulizi:
Watu wengi mno ndani ya
makanisa wana kiu ya kupata ujazo wa Roho Mtakatifu, lakini bado kuna tatizo
kubwa sana linalohusiana na kutomwelewa vizuri Roho Mtakatifu. Kwa kuwa kiu hii
ni kubwa na tatizo la kutomwelewa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa ni kubwa sana
nimeona ni vema nitumie nafasi hii kutoa mchango kidogo wa kukusaidia kuelewa
kwa kiasi habari za Roho Mtakatifu.
ROHO
MTAKATIFU NI NANI?
“Upepo
huvuma uendako, na sauti yake wasikika, lakini hujui unakotoka wala
unakokwenda; kadhalika yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” (Yohana 3:8)
Tunapoangalia kwa lugha ya
Kiyunani, tunaweza kuona kuwa kitu ambacho ni roho hufananishwa au huelezewa
kwa mfano huu uliotangulia. Hapa tunajifunza kuwa, hakuna mtu anayeweza
kuukamata au kuuona upepo kwa macho ya kibinadamu, bali anachoweza kuona ni
kazi au matunda yaletwayo na upepo. Hali kadhalika hatuwezi kumwona Roho
Mtakatifu kwa macho ya kibinadamu wala kumkamata, bali aliyempokea anaziona
kazi zake waziwazi kabisa
ROHO MTAKATIFU HAKUUMBWA.
Roho Mtakatifu hakuumbwa,
bali ni mojawapo katika Nafsi takatifu za Mungu. Kwa hiyo ni sahihi kusema
kwamba Roho Mtakatifu pia ni Mungu. Kumbuka kuwa tunaposema Nafsi tatu za Mungu
hatumaanishi kuwa kuna Miungu watatu, bali ni Mungu mmoja katika nafsi tatu,
yaani Baba Mwana na Roho Mtakatifu.
Ni vema pia tufahamu kuwa ufalme
wa Mungu ni ufalme wa siri, kwa hiyo hata kumfahamu Mungu kwa ufasaha na utatu
wake ni kitu kisichowezekana kwa akili za kibinadamu zilizoghoshiwa na dhambi,
ni lazima tukubali kwamba ni kwa neema ya Mungu tu. Kwa kawaida ufahamu huu
unapatikana kwa Yule tu aliyeokoka kwa kuzaliwa mara ya pili, na kumpokea Roho
Mtakatifu aliye mwalimu wa kweli. Neno la Mungu linasema;-
“Hakuna
ajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake na vivyo hivyo
mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu” 1 Wakorinto 2:11
Kuna sehemu nyingi sana
kwenye Biblia zinazoelezea nafsi hizi za Mungu na mfano mzuri tunaupata katika
injili ya Luka wakati wa kubatizwa kwa Yesu Kristo;-
“Ikawa,
watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye Kristo amebatizwa , naye
anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa
kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, wewe ndiwe mwanangu, mpendwa
wangu; nimependezwa nawe” (Luka 3: 21-22)
Kwa maelezo ya mistari hii,
tunaziona nafsi zote tatu za Mungu zikijidhihirisha waziwazi kwa wakati mmoja
yaani;-
1.
MWANA
alikuwa majini akibatizwa
2.
ROHO
MTAKATIFU akamshukia kwa mfano wa hua.
3. BABA
akatoa sauti kutoka mbinguni. “Wewe
ndiwe mwanangu, mpendwa; nimependezwa nawe”
Kwa kuwa Roho Mtakatifu ni
nafsi hai ya Mungu, hapana shaka kwamba naye pia ni Mungu na ana sifa ya kuwa
Alfa na Omega kwa maana ya kwamba hana mwanzo wala mwisho na ni makosa kuamini
kwamba Roho Mtakatifu ameumbwa na Mungu.
Kwa
leo somo letu linaishia hapa, usikose kufuatilia sehemu inayofuata ya somo hili.
Kwa msaada zaidi tuwasiliane 0677 609056
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni