Mwl:
Furaha Amon
Utangulizi:
Watu wengi mno ndani ya
makanisa wana kiu ya kupata ujazo wa Roho Mtakatifu, lakini bado kuna tatizo
kubwa sana linalohusiana na kutomwelewa vizuri Roho Mtakatifu. Kwa kuwa kiu hii
ni kubwa, na tatizo la kutomwelewa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa ni kubwa sana
nimeona ni vema nitumie nafasi hii kutoa mchango kidogo wa kukusaidia kuelewa
kwa kiasi habari za Roho Mtakatifu.
TOFAUTI YA HUDUMA YA ROHO
MTAKATIFU KATIKA AGANO LA KALE NA KATIKA
AGANO JIPYA
Roho Mtakatifu hakuanzia
wakati wa Agano Jipya, yeye kama nafsi ya tatu ya Mungu, hivyo hana mwanzo wala
mwisho. Kwa maneno haya, napenda utambue kuwa Roho Mtakatifu alikuwa akihudumu
kwa namna fulani hata wakati wa Agano la kale. Ijapokuwa ilikuwa tofauti sana
ilivyo sasa katika Agano jipya. Zipo tofauti nyingi za huduma ya Roho Mtakatifu
wakati wa maagano haya mawili; zifuatazo ni baadhi ya tofauti hizo.
Wakati wa agano la kale
makao makuu ya Roho Mtakatifu yalikuwa mbinguni. Tunapoyaangalia maisha ya mashahidi
wa kazi ya Mungu katika Agano la kale, na wale wanaojulikana kama mashujaa wa
imani, tunaweza kuona kwa dhahiri jinsi huduma ya Roho Mtakatifu
livyozifaikisha njia zao.
n Roho
Mtakatifu aliwasaidia kuwaonya watu na kuwakemea
n Kwa
Roho mtakatifu mashujaa hawa waliua samba na dubu
n Mashujaa
hawa walitenda mambo mengi makuu yasiyoelezeka kwa akili za kibinadamu.
Wakati wakutenda huduma
zote hizi. Roho Mtakatifu alikuwa na makao yake ya kudumu mbinguni pamoja na
Mungu Baba na Mwana.
KATIKA AGANO JIPYA, TUNAONA
UHAMISHO WA MAKAO YA ROHO MTAKATIFU HUYU WA MUNGU; BADALA YA KUKAA MBINGUNI
ALIHAMIA NA KUKAA NDANI YA KANISA, KAMA YANENAVYO MAANDIKO.
Yesu alipokuja kukaa
duniani; mbinguni aliwaacha wawili, ambao ni Mungu Baba na Mungu Roho Mtakatifu.
Alipomaliza huduma yake duniani alisema
maneno haya kabla ya kwenda kwa Baba yake; Alisema,
“Nami
nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi milele”.
(Yohana 14:16.)
Kwa hiyo baada ya Yesu
kupaa mbinguni, walikuwepo tena watatu mbinguni kwa muda wa siku kumi. Watatu
hawa ni Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, baada ya siku hizo kumi baada ya
kupaa kwa Bwana, Roho alikuja duniani kuchukua nafasi ya Yesu; na kuanzia
wakati huo hadi wakati huu, wako wawili mbinguni, Baba na Mwana na duniani yuko
mmoja naye ni Roho Mtakatifu.
KATIKA AGANO LA KALE ROHO
MTAKATIFU ALIKUWA KWA WATU WACHACHE TU;
Udhihirisho wa huduma ya
Roho Mtakatifu katika Agano la kale ulikuwa tofauti sana na ilivyo sasa. Katika
agano la kale Roho Mtakatifu alikuwa anafanya huduma na kudhihirisha nguvu zake
kwa watu wachache waliokuwa na huduma maalumu mbele za Mungu au kwa taifa teule
la Bwana, ili tupate picha iliyo kamili hebu tuangalie baahi ya watu
walioshuhudia huduma na udhibitisho wa nguvu za Roho Mtakatifu vikitenda kazi
ndani yao wakati wa Agano la kale.
KWA WAAMUZI NA WAFALME WA
TAIFA LA ISRAELI
Waamuzi na wafalme katika
taifa la Israel walikuwa ni muhimu mno katika taifa hilo. Makundi haya mawili
ndiyo yaliyotunza nuru ya Mungu wakati taifa lao lilipokuwa linaingia katika
giza nene. Kwa umuhimu huo waliokuwa nao. Mungu Roho Mtakatifu alifanya kazi
katika maisha yao yote, ila walipomwacha Mungu Roho wa Mungu naye aliweza
kuwaacha kwa huduma hii ya Roho Mtakatifu, waamuzi na wafalme, waliweza kuzima
nguvu za majeshi yenye nguvu, walirarua simba na muda wote walipopigana au
kuongoza chin ya uongozi wa Roho Mtakatifu, waliweza kushinda na zaidi ya
kushinda.
MANABII NA MAKUHANI
Manabii na
makuhaniwalihusika sana kuongoza taifa la Israeli kiroho; wao walikuwa ni mkono
na sauti ya Mungu katika taifa la Israel kiroho; nasema hivi kwani kupitia
kwao, Mungu aliyaweka maneno yake aliyotaka kunena na watu wake, kupitia kwao
Mungu pia aliweza kupokea toba ya watu wake na dhabihu zao.
MWISHO
WA SOMO LA NNE
Kwa
leo somo letu linaishia hapa, usikose kufuatilia sehemu inayofuata ya somo hili.
Kwa msaada zaidi tuwasiliane 0677 609056
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni