Jumatatu, 3 Septemba 2012

TWENDE LUSHOTO VIEW POINT KATIKA PICHA


SAFARI YETU MBEYA KWA TRAIN

Mara nyingi sana nilimsimulia Flora habari mbalimbali za vijiji vilivyomo pembezoni mwa reli ya Tanzania na Zambia TAZARA na alionyesha hamu sana ya kusafiri na Treni kwani alitaka kufahamu historia na jiografia ya nchi yetu kupitia tazara. na hatimaye tulipanga safari kutoka Tunduma kwenda Dar es salaam.
Huu ni mji wa Vwawa Mbozi ambako ndio nyumbani kwetu ambako wazazi wangu baada ya kustaafu kazi serikalini waliamua kuishi katika mji huu, na sisi pamekuwa ni nyumbani kwetu.
Hiki ni kituo cha garimoshi cha vwawa mbozi
Hapa Flora anaonekana akisubiri kwa hamu kubwa sana galimoshi (gogo)
Baada ya muda garimoshi linaingia likitokea Kapirimposhi Zambia
Flora akikusanya vifaa vyake ili kupanda ndani ya Treni, katika kituo kama hiki Garimoshi hutumia dakika 15 tu.
Baada ya kuingia ndani na kupatiwa chumba ambacho atakitumia kwa kukaa na kulala Flora anaweka vitu vyake sawa
Baada ya hapo tulielekea Buffet kwa ajili ya chakula na vinywaji.
mpaka hapo Flora alikuwa bado hajalikubali Treni aliniambia ni kama linayumba sana nikamwambia atulie ataifurahia tu safari maana tutapita mpaka kweny mbuga za wanyama za Serous ataona wanyama mpaka atasinzia.
Hapa ni safari na muziki wa ala wewe ni kuweka vesi tu maana chuma kwa chuma ni mdundo tu.
Kutoka Tunduma abiria walikuwa wachache sana tofauti na miaka ya nyuma ninavyokumbuka hapa hotelini ilikuwa ni hekaheka muda wote.
Kwa mbali sana unaweza kukiona kiwanda cha saruji cha Songwe eneo hili ndilo wanalojenga kiwanja kikubwa cha kimataifa cha ndege.
Sehemu nyingine unaweza ukatamani ushuke jinsi palivyotulia.
hatimaye tulipita maeneo ya Mbalizi.
Wakati mwingine hali ya hewa ilianza kuwa ya baridi wafanya kazi wa Tazara walitupatia mablanketi mazito kwa ajili ya kujikinga na baridi.
Hapa ni mbeya mjini tulishuka kidogo kwa ajili ya kunyoosha miguu.
Hii ni shule ya msingi majengo hapa ndipo nilipopata limu yangu ya msingi.
Huyu ni rafiki yangu wa utotoni kabisa anaitwa Fredrick Lupembe hapa nilimtembelea ofisini kwake alifurahi sana tulipoonana maana tunapoteana sana
Kama kawaida ukiongozana na Flora huwa anapenda sana kuchepukia kwenye vitu kama hivi kwa ajili ya kujenga mwili.
Kwa kweli picha hii nimeipenda sana hebu nipige na na sanamu hii.
Mandhari nzuri ya kuvutia inaonekana vizuri kabisa katika milima ya Mbeya.
Picha hii inanikumbusha tulipotoka kuangalia makaburi ya ndugu zetu,sio kama tunaamini kitu fulani kuhusu wafu. Hapana tunakwenda kuangalia kwa sababu ya kutunza kumbukumbu.
huu ndio mtaa ambao mimi nimekulia kwa miaka mingi sana. huwa nikifika naona mabadiliko mengi sana ni kama ukiwa fulani hasa nikikumbuka nilipokuwa mdogo rika la hao waheshimiwa wanaocheza mpira wa makaratasi
Hii picha ilipigwa mwenge kama kumbukumbu na sista wangu Rose na mjomba Munde katika duka la vinyago mwenge.
Na hapa ni safari ya kuelekea mashambani.
Flora akia na wifi yake Naomi wakiangalia maeneo ya mashamba ya familia.
Kwa kweli wakati mwingine ulikuwa ni wakati wa furaha sana kuwa katika maeneo ambayo mnakuja kwa nadra sana kiasi cha mara moja kwa mwaka.
Hii ni kumbukumbu ya kutambulisha mchumba Huyu ni mdogo wangu Cecilia Brown Mwakasege siku mchumba wake alipokuja kumchumbia nyumbani kwao Tabata Liwiti.
Pembezoni kidogo ya Jiji la Mbeya picha hii nimeipiga nikiwa eneo la Majengo nimepiga kuelekea usawa wa Iyunga ambako iko stesheni ya galimoshi *TAZARA.