Alhamisi, 22 Novemba 2012

HABARI KATIKA PICHA

Mpiga picha akiwa makini sana katika kupata picha nzuri.nafikiri hapo anawahimiza watabasamu kidogo ili picha itoke vizuri zaidi.
Gari aina ya Fiat (mbaula) ikiwa imebeba mabua
Picha hii inajieleza yenyewe umuhimu wa kuwa na mke mwema
hapa ni gari dogo aina ya PicUp ikiwa imebeba mzigo usio wa kawaida
Hapa ni mahali fulani gari likiwa limebeba mzigo na abiria
Askari akiwa anamsubiri mwenye gari hili amuhoji kuhusu namna alivyobeba mzigo.
Hapa ni kazi tu mapenzi hayana nafasi katika kazi
Haya yalikuwa ni maandamano ya wanaume kupinga kuchomolewa fedha kienyeji na wake zao
Wanasiasa vigogo wakipata tiba ya kikombe cha babu mwasapile
Nimeipenda sana picha hii,inaonyesha kwamba vijana hawa kweli wanapendana.
Picha iliyochakachuliwa(sio picha halisi) ya mzee mwasapile

Jumapili, 18 Novemba 2012

TAFITI: MATUMIZI YA MTANDAO YANAIMARISHA KAZI ZA UBONGO KWA WAZEE





  • Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonyesha kwamba matumizi ya mtandao (internet) kwa wazee yanaimarisha utambuzi (cognition) na kazi za ubongo wao. Utafiti huu ulihusisha wazee wa jinsia zote wenye umri kati ya miaka 55 na 78. Wazee hawa waligawanywa katika makundi mawili. Moja halikutumia mtandao na kundi jingine lilitumia mtandao mara kwa mara.
  • Matokeo yalionyesha kwamba kazi za ubongo wa wazee katika kundi ambalo lilikuwa linatumia mtandao mara kwa mara ziliimarika zaidi kuliko za wazee katika kundi ambalo halikutumia mtandao. Mabadiliko makubwa yalionekana katika sehemu za ubongo zinazoshughulika na kumbukumbu (memory), lugha, kusoma na upambanuzi. 
  • Matokeo haya yamewafurahisha wanasayansi na wanasema kwamba pengine matumizi ya mtandao yanaweza kuwa silaha mojawapo dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na upotevu wa kumbukumbu na utambuzi kama vile Alzheimer.
  •  
  • Sina uhakika kama kweli wazee wa Kiafrika wanahitaji mtandao kuimarisha kazi za ubongo wao. Mimi nadhani kwamba michezo kama vile bao, drafti na hata kuhesabu ng’ombe wanaporudi nyumbani kila jioni ni mazoezi tosha yanayoweza kusisimua kazi za ubongo, mazoezi ambayo yamesaidia kuwafanya wazee wengi wa Kiafrika kubakia makini kiutambuzi (cognitively) hata katika umri mkubwa. Sijui kama tulikuwa na wagonjwa wengi wa Alzmeimer barani Afrika kabla ya hili wimbi jipya la utandawazi tunaolishuhudia kwa sasa. Isitoshe, tulikuwa tunakula vyakula vya kiasili na mfumo wetu wa maisha ulituwezesha kufanya kazi sana. Sasa mambo yamebadilika sana na pamoja nayo magonjwa ya moyo, saratani, kiharusi na si ajabu "dementia" na Alzheimer sasa yanatuandama.