Jumamosi, 19 Agosti 2017

MATOKEO YA KUSIFU NA KUABUDU KWA WATAKATIFU.



-     Huleta hofu ya Mungu katikati ya watakatifu.
-     Huyeyusha mioyo migumu katika kupokea mambo ya Mungu.
-     Hulipua vizuizi vya kuikulia neema ya Mungu
-     Nguvu ya Mungu huonekana.
-     Utendaji wa Roho Mtakatifu hujidhihirisha kwa karama kuchanua.
-     Moto wa uamsho hutembea na maelfu ya watu kuokoka.
Matokeo ya kusifu na kuabudu kwa kanisa (Yohana 4:1-23)
-     Mungu hupewa sifa na utukufu
-     Ni ibada ya moyo kwa moyo na Mungu (Yohana 4:24)
-     Roho ya mtu au yule mtu wa ndani ndiye awezaye kuabudu.
-     Mungu ni Roho anawatafuta watu kama hao wamwabudu.
-     Watu hawa ni wachache sana na adimu miongoni mwa wengi waziendeao nyumba za siku za jumapili. Ndio maana Mungu anafanya kuwatafuta.
-     Mungu wetu anayo namna ya kuabudiwa kutoka katika roho ya mtu wa ndani, ni mtu wa ndani pekee ndiye awezaye kumuabudu Mungu ipasavyo.
-     Yeye ndiye mwenye mahusiano na ushirika hai na Mungu.
-     Mtu asiyeokoka hawezi kuabudu Mungu kihalisi (Mt 15: 8-9)
-     Asiye okoka hawezi kuufikia ujuzi wa kweli katika kuabudu.
-     Mtu aliyeokoka ndiye pekee awezaye kuabudu halisi kwa kuwa mwelekeo wa kuabudu ni kutoka kwa mwamini kwenda kwa Mungu
-     Toka kwa mtu wa ndani hadi mawazo kisha maneno.
-     Maneno ni mawazo yaliyovishwa sauti hatimaye kuingia kwenye vitendo (udhihirisho wa mwitikio wa moyo)
-     Twamsifu na kumuabudu Mungu tukijieleza kwake.
-     Upendo wetu,utii wetu,kujitoa kwetu kwake twasema kuwa
§  Mungu ni nani
§  Amesema nini
§  Anafanya nini na alifanya nini
-     Asiyeamini mtu wa litulgia hawezi kufanya yote haya yeye binafsi toka katika vilindi vya moyo wake.
-     Mungu hana ushirika na kiumbe katika kuabudiwa.
-     Katika maandiko (Mt 4: 9-10) majibu ya Bwana Yesu kwa shetani yanaonyesha kuwa Mungu hana mshirika katika kupokea ibada na kiumbe yeyote duniani, mbinguni au kuzimu (kutoka 34:14) Mungu anasema kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu.
Wafilisti katika kitabu cha (1Samweli 5:1-5) waliliteka sanduku la Mungu na kulitia katika nyumba ya dagoni mungu wao. Wakaliweka sanduku la Mungu karibu na dagoni mungu wao,
-     hii ilikuwa ni sawa na kumlinganisha Mungu YEHOVA na dagoni.
-     Kwa waisraeli lilipokuwa sanduku la Mungu ilikuwa ni ishara kuwa YEHOVA yuko mahali hapo.
-     Wafilisti walipoamka asubuhi siku ya pili, kumbe sanamu lao dagoni limeanguka kifudifudi mbele ya Mungu wa Israeli.
-     Huku kichwa cha dagoni na vitanga vya mikononi vimekatika vipo vimelala kizingitini dagoni imebaki kiwiliwili.
YEHOVA Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu, na hatalinganishwa na chochote, maana yeye ndiye muumbaji.
-     Iwe binadamu, malaika au shetani na mapepo yake ambao awali walikuwa ni sehemu ya malaika wa Mungu kisha wakaasi, hapo ndipo walipopoteza nafasi zao katika ufalme wa Mungu mbinguni.
-     Kumbuka kwamba tumeumbwa ili tumuabudu Mungu. Hii ndio moja ya sababu kubwa ya kuumbwa kwa jinsi tulivyo. (Zab 103:1).
Kama vile wanadamu waundapo magari na mitambo mbalimbali, wanaunda wakilenga kutosheleza uwezo wa kutendea kazi iliyokusudiwa.
-     Hali kadhalika ndivyo ilivyo hata tunapoamua kujenga nyumba, barabara, n.k.
-     vivyo hivyo kwa wanadamu kila kiungo chetu kimekuwepo pia kutuwezesha kufikia makusudi ya Mungu ya kumwabudu tuwapo katika dunia tuliyoumbiwa. (Tazama Isaya 45:12).
Viungo vyetu pia hutuwezesha kuwa na mahusiano na dunia lakini tukishatoka duniani na kuvishwa mwili mpya (1Wakorinto 15:40) tujapokuwa katika mwili mpya lakini katika umbo la kibinadamu tutakuwa na;-
-     Miguu inayoweza kucheza kwa urahisi
-     Magoti yanayoweza kujikunja tuabudupo
-     Kiuno na mgongo uwezao kuinama na kuinuka
-     Mabega yawezayo kucheza
-     Mikono iwezayo kupiga makofi kunyanyuliwa juu
-     Kichwa kiwezacho kucheza
-     Kinywa chenye kutoa sauti zenye tuni mbalimbali.
Hakuna kiumbe aliyeumbwa huru kutenda vitendo vingi kama binadamu tazama (Zaburi 139:15).
Sifa za Bwana ni bubujiko la moyo (Yoh 4:10)
-     Bwana alimfananisha Roho Mtakatifu na maji yabubujikayo, ampokeaye humuondolea kiu milele.
-     Maji hayo hububujika kutoka utu wa ndani wa mtu hadi kudhihirika katika utu wan je (utu wa asili)
-     Hali ya ukame kiu haitakuwapo tena, hutasifu na kuabudu kwa dakika 2 na kujisikia kuchoka.
-     Hutakuwa na moyo unaokerwa na bubujiko la Roho Mtakatifu.
-     Hutazuwia kunena kwa lugha (1Wakorinto 14:39)
Kuna watu wanaodhani kuwa utaratibu wao wa ibada ni sahihi,
-     Watu hao hupanga kusifu na kuabudu kwa dakika zisizozidi 10.
-     Lakini matengenezo na mipango yao ya kanisa hupangwa husemwa kwa dakika zaidi ya 30.
-     Poroja za kusalimiana na kutambulishana huchukua zaidi ya saa.
-     Hapo wakisahau makusudi ya Mungu kwa wanadamu.


Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandika kitabu hiki kuhusu ibada.
Naamini kwamba bila ya himizo la Roho Mtakatifu ndani yangu nisingeweza kukamilisha kazi hii.
Ni matumaini yangu kwamba kila atakayesoma atapata msaada na kukua kiroho.
Wito wake kwa Kanisa la Kristo ni kuwataka waamini waijue ibada ya Kiroho na ya Kweli yenye upako wa Roho Mtakatifu. Ambapo waabuduo watamwabudu Mungu katika Roho na Kweli, na kurejesha maana ya sifa, ibada na kuabudu kulikopotea hekaluni mwa Bwana. Ibada ya kweli italeta furaha ya Roho Mtakatifu maishani mwa waamini na kurejesha tumaini la utukufu mioyoni mwao maana tayari wameona uwepo wa Mungu katikati yao, kisha kujenga imani zao, na shauku yao kwenda kuwa pamoja na Bwana Mbinguni.

IBADA NI NINI?
Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu linalofanywa na mtu kwa kiumbe aliye mkuu katika mazingira yake yote, kiroho na kimwili na kiumbe huyo akaaminiwa kuwa ni MWENYE ENZI asiyefananishwa na kiumbe kingine mkamilifu katika matendo yake.
Kuabudu Mungu katika Roho na Kweli kunaweza kukafanywa wakati wowote na mahali popote mradi lengo ni kumfanyia Mungu IBADA.
-     Jambo la muhimu ni yule tunayemwabudu kuliko mahali tunapofanyia ibada
-     ingawa mahali tunafanyia ibada ni kitu chema ,lakini pasipewe nafasi mioyoni mwetu na kuheshimiwa kama sehemu ya ibada.
-     Pamoja na hoja hiyo mahali pa ibada pasipuzwe na kudharauliwa maana pamewekwa wakfu kwa huduma ya Mungu pametakaswa.
-     Mtu akionyesha dharau au kuto paheshimu anaweza kupata madhara,
-     hivyo ni muhimu kila mtu ajue jambo hili na kuenenda kwa utaratibu na kwa heshima mahali hapo.

Kwa vile Ibada ni shughuli ambayo inashikamana sana na mfumo wa maisha ya mwanadamu, na kwamba ibada hutofautiana sana katika maana na mitazamo kulingana na imani ya mtu juu ya Mungu anayemwabudu, ni vema tukaelewa kwa usahihi ibada ninini kwa mujibu wa Biblia ifundishavyo.
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema , ya kupendeza, na ukamilifu”. (Rumi 12:1-2)

Tendo la Ibada ni tendo la kujitoa kama dhabihu, lakini ibada ya kweli lazima dhabihu hiyo iwe hai na takatifu, Mwili, Roho na ufahamu viwe na lengo moja lakumfanyia Mungu Ibada takatifu basi, ambapo ibada nje ya utakatifu si ibada inayompendeza.


IBADA – MAANA YAKE


Ibada ni kumshangaa Mungu. Kwa ufahamu tulio nao na akili ya kibinadamu tuliyo nayo hatuwezi kumwelewa Mungu kikamilifu tukamfahamu.
Isaya 55:8-9:,
“Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”

-     Mungu ni mkuu kuliko uwezo wa ufahamu wa mwanadamu
-     na yuko juu sana kuliko mawazo ya mwanadamu.
-     na yuko juu sana kuliko njia za mwanadamu

kwahiyo hatuwezi kumfahamu vyema. Hivyo basi siku zote tutakapokusanyika pamoja au mtu akiwa peke yake kumwabudu na kukutana naye atamshangaa (tutamshangaa).
-     Hutaweza kukaa mbele za Mungu ukimwabudu katika Roho na Kweli ikawa jambo la kawaida,
-     maana Mungu huyo ni Mfalme Mkuu lazima utamshangaa Mfalme huyo.
-     Utukufu wake utakushangaza na kutamani kumwangalia.


Wafalme wa dunia japokuwa ni wanadamu, raia wao hutetemeka na kuwaheshimu wanapojitokeza mbele na kila mtu hutamani kumwona na kumshangaa, na kukusanyika mahali pamoja ili wamsikilize Mfalme wao. Mungu ni Mfalme wa ajabu anayejihudhurisha kati ya watu wake wanapomfanyia ibada kwa kumwabudu na kuwashangaza waabuduo ambapo na wao wanazama katika mshangao. Zab. 47:7, 66:3, 68:35, 71:16, 89:7

IBADA INAYOKUBALIKA



Si kila Ibada inayofanywa na mwanadamu ni halali na kukubalika na Mungu, hapana. Mungu ni Mungu wa utaratibu na mipango mikamilifu.
Mungu amesema wazi ni ibada ipi anaikubali na kuipokea akaisikiliza. Lakini kwa kuwa ulimwengu ni mpana na wenye tofauti za watu walio na itikadi tofauti na ibada za walimwengu pia ni tofauti.
-     Mungu wa kweli ni mmoja na njia ni moja ya kumfikia ambayo ni Yesu. Yohana 14:1-6, ITim 2:15.
-     Ni katika Yesu ambaye ni mpatanishi wetu na Mungu na ambaye ni kweli, njia na uzima tutasikilizwa na kukubaliwa,

Yesu anasema mtu yeyote hawezi kwenda kwa Mungu isipokuwa kwa njia yake, hakuna njia ya mkato kwenda kwa Mungu, bali ni kwa njia ya Yesu tu. Kwa hiyo ibada lazima iwe,
a.  Ibada katika Roho na Kweli yenye kumtambua Yesu kuwa kiini na mlengwa wa Ibada hiyo Mdo 4:11-12 Waef 2:4-8

b) Si ibada ya mdomoni wala makusanyiko ya kidini na taratibu za kibinadamu zilizobuniwa kwa umahiri na wala si mapokeo ya mila na desturi za watu. Mdo17:22-27

c) Ibada ambayo haimchanganyi Mungu aliyejifunua katika maandiko na miungu mingine, japokuwa miungu hiyo inaabudiwa na mamilioni ya watu pamoja na vitu vilivyotukuzwa kiasi cha kukubalika kuwa Mungu. Zab 115:4-8

Sanamu zao ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadmu. Zina vinywa lakini havisemi, zina macho lakini haioni. Zina masikio lakini hazisikii, zina pua lakini hazisikii harufu. Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, wala hazitoi sauti kwa koo zake. Wazifanyao watafanana nao, kila mmoja anayezitumainia.

Sasa ili tujiridhishe na ibada ya kweli inayokubaliwa na Mungu hebu tuangalie ibada ya mbinguni ilivyo, na jinsi viumbe wa mbinguni wanavyomwabudu Mungu.

IBADA KUU MBINGUNI


Ufunuo 5:6-14
Biblia inafunua ibada kuu inayoendelea mbinguni ambayo washiriki wa ibada hiyo ni wenye uhai wanne na wazee ishirini na nne,
-     Wenye vinubi na vitasa vya dhahabu vyenye maombi ya watakatifu, wakiwa mbele za kiti cha enzi cha Mungu.
-     Viumbe hawa wapo hapo kufanya ibada maalum ili kumwabudu na kumpa sifa Mwanakondoo,
-      wanafanya hivyo kwa kuimba wimbo mpya wenye sifa kwa Mwanakondoo kisha malaika wengi, elfu kumi mara elfu kumi, elfu mara elfu, ambao wamekizunguka kiti cha enzi wanajiunga katika SIFA hizo. Uf 4.8-11
-     Hapa ndipo ibada hii kuu inaanzia, ambapo wenye uhai wanne wasiopumzika mchana na usiku wanamsifu Mwanakondoo wakisema Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu na kusababisha wazee ishirini na nne kuanguka chini na kumsujudia aliye Hai milele na milele,
-     huku wakivua taji zao na kuzitupa mbele ya kiti cha Enzi, wakisema, Umestahili wewe Mungu kupokea utukufu na heshima na uweza kwakuwa ndiwe uliyeviumba vitu vyote kwa sababu ya mapenzi yako vilikuweko navyo vimeumbwa.

Kisha kwa sauti ya pamoja wanasema: Anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu, na Baraka Mwanakondoo aketiye kwenye kiti cha enzi.
Maneno haya saba ni sifa kuu kwa Yesu ambaye ni Mwanakondoo wa Mungu.
Hatimaye baada ya ngurumo hizo za sauti ya sifa, kila kiumbe kilichoko mbinguni, duniani, na baharini vikamsifu Mwanakondoo,
-     na wote wakaanguka wakamsujudia Mwanakondoo. Sifa hii ikatikisa ulimwengu,
-     ulimwengu mzima ukamwabudu Mwanakondoo, Ibada hii haifanywi kwa mtume, nabii, malaika ,miungu wala kwa mwanadamu bali Ibada hii inamlenga Yesu Mwanakondoo.
-     Ibada inayofanywa kwa mtu mwingine mbali na Yesu siyo Ibada ya kweli na Mungu haisikilizi.
-     Inasikitisha kuona Ibada za mamilioni ya watu hazisikilizwi na Mungu kwa kuwa zinafanywa nje ya kumwabudu Yesu.
-     Katika Zaburi 98:1-9 na 96:1-8 Mfalme Daudi anatoa mwaliko wa kumwabudu Bwana kwa wimbo mpya kwa sababu Bwana Ametenda mambo ya ajabu,
-     Daudi anasema, “Inueni sauti, imbeni kwa furaha,
-     Nayo mito ipige makofi, na kulibariki jina lake,
-     Na kutangaza wokovu wake,
-     Kwa kuwa Bwana ni mkuu na mwenye kusifiwa sana.
Wito huu ni wito wakumwabudu BWANA peke yake.
Paulo naye anatia mkazo wa kumwabudu Mungu kwa kutoa mwongozo jinsi ya kufanya ibada katika roho ya uimbaji anasema
Neno la Kristo likae kwa wingi mioyoni mwenu (ndani yenu) katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkimwimbia Mungu kwa Neema mioyoni mwenu. Mkisemazana kwa zaburi na tenzi, na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Mungu mioyoni mwenu, nakumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo” (Kol 3:16-17),

Ef 5:19-20.
-     Ibada ya kweli ni ile inayomlenga Yesu na si vinginevyo.
-     Unaweza kuona jinsi mwanadamu anavyotoa muda wake, nguvu na mali katika ibada hewa kwa viumbe na sanamu, badala ya kumfanyia Mungu ibada katika Kristo Yesu,
-     wito huu ungali na nguvu ile ile kwetu kumgeukia Mungu na kujiunga na viumbe hawa wa mbinguni kumfanyia ibada sahihi Mwanakondoo.
-     Mungu ni mtakatifu na wa haki hana kigeugeu na habadiliki, ni mwadilifu.
-     Hawezi kuweka njia tofauti tofauti za kumwabudu kwa kila mtu.
-     Hiyo ingekuwa sawa na wasafiri wawili waendao mji mmoja lakini kwa njia tofauti zinazoweza kuwafikisha pale waendapo,

-     hilo haliwezekani kwa Mungu maana ni Mtakatifu, kwa utakatifu huo, Mungu ameweka njia moja ya kumwabudu ambayo ni Yesu Kristo.

HUDUMA YA MUZIKI (UIMBAJI) KATIKA SIFA NA IBADA




1. Muziki ni nini?
Ni sanaa inayoishi iliyo hai ambayo inadumu mpaka ulimwengu ujao katika umilele. Huduma zingine zote zitakomea hapa duniani bali muziki hautokoma utakuwepo milele na milele.
“Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia”. (Isaya 35: 10)
Msitari huu unahusu watu waliokombolewa kwamba wataimba milele!
-     Furaha ya milele, ni kiashirio cha uimbaji wa watu hawa kwamba wataimba milele.
-     Muziki Ni lugha ya kiulimwengu inayozungumza na hisia za mtu yoyote,
-     lugha hii hueleweka na msikilizaji, kwa kuguswa utu wake na fahamu, kisha nafsi, moyo, akili na mwili.
-      Haijalishi lugha iliyomo katika wimbo, muziki, kwamba unajua au la,
-     Mawasiliano sahihi yanakuwepo na kueleweka katika hisia za msikilizaji.
Muziki una nguvu ya kuleta amani na furaha moyoni, burudiko na pumziko la akili kiasi cha kumshawishi mtu kukubali nakujiachia katika mivuto yake.
Nguvu ya muziki imeujaza ulimwengu na kupenya katika utamaduni wa kila kabila, taifa, jamii, na lugha, hii inaonyesha muziki hauna mipaka.

Muziki umesafiri bila kizuizi kwa njia za mawasiliano ya vyombo vya habari popote ulimwenguni. Ni vigumu kwa mtu kujizuia kuitikia mara asikiapo muziki ukiunguruma,
-     muziki ni chakula cha masikio na ubongo, muziki mtamu unapoingia masikioni mwa msikilizaji hupenya kwenye akili zake,
-     na akili zake huusukuma mwili na kuanza kutikisa kichwa, miguu, mikono na kiwiliwili, na kucheza, kutokana na utamu wa wimbo na ujumbe wa wimbo huku akirukaruka kufuata midundo ya muziki unaopigwa.
Katika zama zetu, muziki umekuwa ni utambulisho wa taifa na heshima ya nchi, kila nchi duniani ina wimbo maalumu wa Taifa ambao huimbwa kuutukuza utaifa na heshima ya Taifa.
-     Kila wakati tukio la kitaifa, wimbo huo huimbwa,
-      mgeni anapotembelea nchi, huimbwa ambapo kila mtu aliye mahali hapo hutakiwa kusimama kimya huku akiimba wimbo huo.
Hapa ni muhimu tuelewe kwamba muziki si uhuni, ama kudhani kwamba ni kazi ya watoto, watu wasio na kazi au watu maskini, hapana hiyo ni dhana potofu, na mtamzamo hasi dhidi ya muziki, tunapaswa kubadilika kimtazamo na kuona utajiri uliomo katika muziki,
-     Kwamba ni hazina tuliopewa na Mwenyezi Mungu kuwa urithi wetu.
-     Na kumshukuru Mungu kwa vipaji na karama alizowajalia waimbaji na wanamuziki wanaohudumia katika huduma hii ndani ya Kanisa la Kristo.
Dunia ingekosa muziki ingekuwa katika giza nene na maisha yangekuwa butu katika nyanja zote. Muziki ni nyenzo fanikishi katika kuelimisha jamii kwa jambo lolote kwa wepesi na kwa haraka, bila vikwazo ama vizuizi.
Biblia imejaa rejea nyingi za muziki, zaidi ya rejea 800 zinazungumzia muziki.
Huu ni ushahidi wa kutosha juu ya umuhimu wake. Msisitizo huu wa maandiko unaonyesha wazi kwamba muziki ni huduma ya kiroho kweli kweli, na kwamba Biblia ni kitabu cha nyimbo, pia ni kamusi ya uimbaji wa kiroho kwa waabuduo, na kwamba kila rejea ya uimbaji itokane na Biblia.

MUZIKI NI UHAI
Muziki ni uhai wa tamaduni, desturi, mila za jamii za watu ulimwenguni, kila jamii ina mifumo na mitindo iliyojengeka tokea zama za mababu zao wa kale, ambao waliachia maadili vizazi vyao vitakavyo kuwepo baada yao.
-     Historia hiyo ya maadili ilitunzwa na kuhifadhiwa katika nyimbo – muziki umetumika kama Benki ya kutunzia maadili na tamaduni za utaifa.
-     Benki hii ilifanya kazi kabla ya uvumbuzi wa kuandika vitabu kuweka kumbukumbu za taifa na jamii husika.
-     Haya tunayaona kwa Musa na wana wa Israeli Kumb. 31:29-, 32:1-44-47 Maandiko haya yanahusu Musa alipokuwa akiwaaga na kuwapa wosia Israeli kabla ya kufa kwake.

-      Akawafundisha wimbo wa wosia na kuwaamuru wawaimbie watoto wao na watoto wao wawaimbie wimbo huo watoto wao na kuendelea.