Alhamisi, 19 Septemba 2013

PICHA ZA TAMASHA LA SIKU YA SIFA KLPT MAJANI MAPANA

Mchungaji Bright Mashauri akiimba katika siku ya tamasha

Baadhi ya watu waliohudhuria siku ya tamasha wakimtukuza Mungu

Mwimbaji wa nyimbo za injili Hellen kijazi na rafiki yake wakifuatilia waimbaji

Vijana na wazee wakifurahia tamasha.

pia na watoto walimfurahia Mungu wao kwa kuimba na kuabudu

Hellen akimtumikia Mungu katika sifa.



Hellen Kijazi

Hellen Kijazi

Hellen Kijazi

Bright & Furaha Mwakasege

Rev George & Christina Nywage wakijiandaa kwa huduma katika siku ya tamasha


MANENO YA REV GEORGE NYWAGE KWA HELLEN KIJAZI SIKU YA TAMASHA.
Nawashukuru sana waimbaji wote walioshiriki katika tamasha hili, na hasa kwa Hellen kijazi. Huyu ni jirani yangu lakini pia wazazi wake ni watu tunaoelewana vizuri. Kama kanisa tunatambua kipaji alichonacho Hellen tunajua kabisa ana kipaji kikubwa sana kiasi kwamba kushiriki katika tamasha la kiwango kilichoandaliwa na kanisa leo ni kwa ajili ya unyenyekevu na kujishusha kwake mbele za Mungu. Tamasha letu hatujaliandaa kitaalamu sana ni la kiwango cha idara tu, lakini amealikwa na amekuja,waimbaji wa kiwango chake wangependa kuhudumu katika tamasha lililoandaliwa katika ukumbi mkubwa na wenye watu wengi na matangazo mengi, lakini Hellen siku zote amekuwa akimtumikia Mungu kwa unyenyekevu bila hata kudai gharama yoyote hata tunapomwita katika mikutano ya kanisa letu, huwa anakuja na hii ni dalili njema kwa kanuni za Mungu kwamba kila anayeshuka Mungu humkweza. nakuomba uendelee na tabia hiyohiyo na Mungu atakuinua.