Jumatatu, 24 Septemba 2012

MAPAMBANO YA KIROHO


Usijaribu kushindana katika mwili

Ukitaka kupata maana nzuri ya maombi ni vizuri na muhimu kusoma Biblia katika waraka wa mtume Paulo kwa waefeso 6.12 anasema kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama,bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili,juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Mstari huu pamoja na kutueleza ugumu wa mapambano lakini pia umeugawa ulimwengu katika sehemu kuu mbili ambazo ni ulimwengu wa damu na nyama na ulimwengu war oho.,.ulimwengu wa damu na nyama ndio huu ulimwengu tunaoishi ambao tunaona kila kitu kwa macho na ambao tumefungwa na mwili kuoweweza kufahamu mambo mengine ambayo yapo nje ya upeo wa macho yetu. Na ulimwengu wa roho ni ulimwengu ambao upo lakini.
 hauonekani kwa macho lakini ni ulimwengu kamili wenye kila kitu na viumbe ambavyo sisi hatuwezi kuviona ila vyenyewe vinaweza kutuona sisi. Katika sehemu hizi mbili za ulimwengu ulimwengu wenye nguvu sana ni ulimwengu wa roho. Mungu na shetani wanaishi katika ulimwengu wa roho,na wakati Mungu anaumba ulimwengu huu Mungu alikuwa anaumba kutokea katika ulimwengu wa Roho,ulimwengu war oho ndio wenye kuamua mambo yote yanayotokea  kaika dunia hii. Hakuna jambo linalokuja duniani bila kwanza kujadiliwa katika ulimwengu war oho ndio maana katika Biblia huwezi kuona neno  bahati mbaya labda bikira akachukua mimba akazaa mtotoo mwanamume, utaona neno likisisitizia kwamba kama ilivyoandikwa na nabii Fulani. Kwa sababu hiyo ndio maana mtume Paulo anatushauri kuwa tunapopambana katika vita ya kiroho usipambane katika hali ya ulimwengu wa damu na nyama,bali anza kushindana katika 
ulimwengu war oho amabko ndiko mipango na vikao vyote vya kukumaliza vinakaa huko. Mambo ya kiroho tunapambana nayo kiroho na wala si kiakili,ukijaribu kupambana kiakili unakuwa umechelewa. Unaposhindana katika damu na nyama ni sawa na kushindana na matokeo inabidi tu uwe mpole kwa sababu unakuwa umechelewa na unaweza kupata shida zaidi kama ukihamaki. Ulimwegu war oho ndio wenye nguvu kubwa sana na ndio wenye uamua nani afe na lini na sababu ya kifo chake iwe nini, kama ni ajali ya kugongwa na gari utaona mtu ameshavuka barabara lakini tena anarudi na kugongwa. Hiyo ni kwa sababu iliandikwa afe kifo hicho katika muda na saa hiyohiyo iliyotokea ajali. Dunia yetu pamoja na uzito wake wote 


 imeshikiliwa na nguvu ndogo sana katika ulimwengu wa roho ambao unaizungusha bila kupoteza majira wala nyakati na inajizungusha kwenye mhimili wake bila kupoteza njia wala kugongana na sayari nyingine. Lakini kama Biblia inavyosema kwamba katika ulimwengu huu wana wa dunia wana hekima kuliko wana wa nuru wana wa nur baada ya kumpokea Yesu wanaridhika haraka sana. Hawataki tena kujifunza au kutafuta mambo zaidi ya rohoni,wanaridhika na ahadi kwamba wanalindwa na malaika. Tofauti na wana wa giza  wao wamejua kwamba ipo nguvu kubwa ya asili ambayo inaitawala dunia,na wamejifunza sana namna  ya kuitumia nguvu hii kwa manufaa yao. Nguvu hii ya asili inatawala maisha ya wanadamu wote wanaoishi hapa duniani kasoro 
waliookoka peke yao Paulo anasema sisi hatuishi kwa kufuata taratibu za dunia hii. Wana wa dunia wamejifunza kwamba  hii nguvu ya asili katika ulimwengu war oho imegawanyika katika sehemu kumi na mbili 12. Sehemu hizi wamzigawa kulingana na tarehe ya kuzaliwa mtu zinaitwa nyota na wamezipa majina hebu angalia mfano huu
 disemba 22    Feb 18      Mbuzi Capricon
januari  20      feb
ukweli ni kwamba ukiondoa watu waliookoka watu wengine wote watake wasitake nyota hizi hutawala maisha yao ya kila siku na zina nguvu kweli. Watu wanaokwenda kutafuta usaidizi kwa wachawi huangalia kwanza nyota zao. Ndio maana ukifika kwa wachawi wanaoagua anaweza kukutajia shida yako hata bila yaw ewe mwenyewe kumueleza ni kwa sababu anajua watu waliozaliwa tarehe Fulani wako katika kundi la nyota Fulani na watu wa kundi hili kwa kipindi hiki wanasumbuliwa na shida Fulani ama katika biashara,kazini,familia n.k. na wanajua ili wafanikiwe wanatakiwa wafanye nini kama una kesi mahakamani na wewe ni mtuhumiwa na akijua tarehe ambayo mtasimama mahakamani ataangalia kati ya nyota yako nay a anayekutuhumu ni ya nani iko juu.na kama ya kwako iko juu atakwambia nenda hata kama mdai wako ana haki lakini atajichanganya na anaweza akashindwa hata kujibu maswali yako
hekima ya wana wa dunia wanajua kuwa ili ufanikiwe katika mambo yako katika dunia ni lazima upatatane na mtawala wa dunia na kwamba huwezi kufanikiwa mambo ya kidunia bila ya kupatana na mtawala. Ili mambo yako yawe mazuri katika nchi hii ya Tanzania ni lazima uwe na uhusiano mzuri na watawala wan chi na ukitaka upate shida aza kupingana na Serikali. Biblia inatueleza katika Mwanzo 1.26 Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu,wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na wanyama… Mungu aliiumba dunia na kumbabidhi Adamu aitawale lakini tunafahamu pia kwamba Adamu aliipoteza haki ya kuitawala dunia kwa kuitoa kwa hiari yake na kumpa shetani tangu wakati huo ili mtu wa dunia afanikiwe ni lazima kwanza aende kwa shetani kuomba msaada.na shetani vile hana adabu ukienda kwake yeye anataka kusujudiwa  tu kama alivyomwambia Bwana Yesu kule jangwani watu wa dunia hii wanamsujudia shetani kwa namna nyingi sana. Wapo wanaozini na wanyama ,maiti n.k. Mungu wetu ni Mungu wa haki na anatupenda sana hakubishana na shetani juuya utawala wa dunia  alijua kwamba shetani ana haki  ya kuuchukua utawala wa dunia. Kwa sababu Mungu alitoa maelekezo kwa Adamu na masharti ya mti waliokula  Adamu alikuwa na hiari ya kukubali au kukataa kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa haki ilibidi ashuke tena duniani kwa mfano wa mwanadamu na kuja kukaa na wanadamu miaka 33 kati ya miaka hiyo alitumia miaka 30 kuizowea dunia na mazingira yake,miaka mitatu ya kutufundisha mbinu ya kumnyaganya shetani haki ya kuitawala dunia  na baada ya kukamilisha kazi yote alitupa mamlaka ya kukanyaga nguvu zote za shetani wakati wote
 unapokuwa umesimama kwenye mamlaka Mungu anakuwa nyuma yako kutekeleza kile unachokisema au unachokiamrisha. Ndio maana anasema kabla hujaomba yeye anajua yote lakini anataka bado tutamke neno. Maana yake tunapomwambia mgonjwa apone Mungu anamwambia  shetani apishe maana Mungu anatambua kuwa sisi ndio tunaotawala dunia.  

WAZAZI HUCHANGIA WATOTO KUKOSA AKILI DARASANI


Wazazi huchangia watoto kukosa akili darasani

 

Uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na baadhi ya mashirika yanayojihusisha na malezi ya watoto ulimwenguni akiwemo Daktari Janet Gonzalez Mena wa Marekani, umebaini kuwa wazazi ndiyo mwanzo hasa wa mafanikio ya watoto wao na kwamba wengi kati ya vijana wanaoshindwa katika maisha kushindwa kwao kunaanzia ndani ya familia zao.
Malezi ya wazazi kwa tafsiri sahihi ndiyo yanayomkuza mtoto na kumtambulisha katika jamii kwamba yeye ni nani? Tunawapata watu wa kabila la Wanyakyusa,Wanyamwezi, Wayao, Wamakua, Wamakonde kwa sababu wamezaliwa na kulelewa na wazazi wa makabila hayo.

Pamoja na yote, kuzaa peke yake bila ya kusimamia tabia ya mtoto huwa ni kazi bure. Waswahili husema: “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Kwa bahati mbaya wazazi wengi wamekuwa hawaelewi kuwa wao ndiyo wenye jukumu la kumtayarisha mtoto awe mwema na mwenye uwezo wa kufikiri.
Hali hii inatokana na kutokuwepo kwa elimu inayotoa somo la jinsi ya kuwalea watoto bila kuwaharibia ufahamu na kuwadumaza katika uelewa wa mambo.

Jambo la kusikitisha ni kwamba, wazazi ambao ndiyo wenye uchungu na watoto wametajwa kuwa chanzo cha watoto kushindwa kukabiliana na changamoto za kimaisha pamoja na masomo.
Ukichunguza kwa makini watoto wengi wanaokuwa mbumbumbu darasani (nazungumzia wale wasiokuwa na kasoro za kibaiolojia) ni wale ambao wazazi wao hawakuzingatia mambo yafuatayo katika kuwalea tangu walipokuwa wadogo hadi kukua kwao.

 HUDUMA BORA
Wazazi wengi hasa wa dunia ya tatu wanakabiliwa na tatizo la uzazi holela, usiozingatia uwezo wa kulea na kuwapa huduma muhimu watoto wao. Mfano lishe bora, mavazi na malazi. Wanasayansi wanasema chakula bora ndicho kinachoweza kuimarisha ukuaji wa viungo vya mtoto na kuufanya ubongo uwe katika hali nzuri ya kumudu kutafsiri mambo.

Hivyo ni jukumu la mzazi anayetaka mtoto wake awe na uelewa mzuri darasani ahakikishe kuwa anampatia mwanae chakula bora kitakachomjenga afya na kumuwezesha kuwa na mwili wenye nguvu ya kukabili magonjwa ya kitoto. Lakini sambamba na hilo mzazi anatakiwa kusimamia afya ya mwanae kwa kumpeleka hospitalini mara kwa mara kutibiwa na kushauriwa.

UTAMBUZI WA KIPAJI
Jambo la pili ambalo ni muhimu kwa mzazi ni kutambua mapema kipaji cha mtoto na kumuongoza sawa na kipaji chake. Ingawa shule nyingi nchini (Tanzania) hazitoi elimu ya ngazi ya chini lakini baba na mama bado wanawajibika kujua ni elimu ya kiwango gani kutoka shule gani itamfaa mtoto wao.
Inashauriwa kwa mzazi kumtambua mwanae ana uelewa gani, ili ajue namna ya kumsaidia ili afikie kiwango bora cha uelewa.  

Kwa mfano, mtoto akiwa na uelewa wa chini anatakiwa kupelekwa kwa waalimu wazuri wenye uwezo wa kumsaidia anaposhindwa, haifai mtoto wa aina hii kupelekwa shule za ilimradi na kudhani huko atasoma na kuelewa.
Itaendelea wiki ijayo.
Masomo haya ya jinsi ya kumsaidia mwanafunzi wa ngazi yoyote kuwa wa kwanza darasani yanapatikana pia kwenye kitabu changu cha saikolojia, mbinu za kusoma na kufaulu mitihani kinachopatika Dar es Salaam pekee kwa wauza magazeti.
UBAGUZI
Kuna wazazi ambao bila kufahamu madhara ya ubaguzi, wamekuwa wakiendekeza upendeleo kwa watoto kwa kuwapenda zaidi baadhi na kuwachukia wengine. 
Hili ni kosa kubwa kwani watoto wanaobaguliwa wanapokuwa na hisia za kutopendwa hudumaa au kushuka kimasomo na pengine kuharibika kitabia kwa sababu ya kukosa kimbilio la malezi. Haifai kubagua watoto!

KUVUNJA MOYO
Watoto wengi wanaoshindwa kumudu masomo darasani ni wale ambao wamelelewa na wazazi hodari wa kuvunja moyo. Kosa dogo la mtoto humfanya mzazi kuwa kama kichaa kwa kumtusi mwanae na kumtungia majina yasiyofaa, kwa mfano: “Mbwa, mjinga, ibilisi, mbumbumbu” na mengineyo. Wanasaikolojia wanasema kauli mbaya zina uwezo wa kuharibu ufahamu wa mtoto na kumfanya ajione duni na mtu wa kushindwa.
Waingereza nao wana msemo wao, “ukitaka kumuua mbwa mpatie jina baya.” Kwa maana hiyo mzazi anapomwita mtoto wake majina mabaya hasa baada ya kushindwa au kukwama katika mtihani wake anakuwa anamuua na kamwe mtoto huyo hawezi kupata alama za juu badala yake atazidi kukinai masomo na kuamua kuacha au kujiingiza katika makudi ya kihuni.
Kauli zifuatazo zinamfaa mtoto aliyekosa kufikia lengo; “Umepata alama za chini mwanangu, lakini mtihani ujao unaweza kupata zaidi” “Juma kakupita mwezi huu lakini usijali mtihani ujao utamshinda nami nitakupa zawadi kubwa sawa?” “Uwe makini ee, umekosa 7 kati ya 10, ukijitahidi kupata zote utakuwa rubani wa ndege.” Maneno haya yanaweza kumfanya mtoto ajue kwamba amefeli lakini anayo nafasi ya kufaulu.
KUHUBIRI YASIYOWEZEKANA 
Kuna baadhi ya watu ambao midomo yao haiishi kuhubiri mambo yaliyoshindikana mbele za watoto hasa yale waliyoshindwa wao. “Mimi nilikuwa mfanyakazi lakini sikuambulia kitu chochote zaidi ya umaskini, nimesoma miaka kumi na sita, lakini nchi hii hata ukisoma hupati kitu bwana.” Maneno ya aina hii hayatakiwi kusemwa mbele ya watoto wanaotafuta elimu. Wazazi lazima wawe na kauli za INAWEZEKANA.

MIGOGORO 
Migogoro ya kifamilia hasa ya wazazi ni sumu kubwa kwa mafaniko ya mtoto, mara nyingi watoto hujikuta wakishindwa kuendelea kimasomo kwa sababu ya wazazi kutengana na kujikuta wanayumbishwa kutoka kwa mzazi mmoja kwenda kwa mwingine au kulelewa na wazazi wa kambo ambako hupewa malezi yasiyostahili.
USIMAMIZI 
Mzazi anajukumu la kusimamia masomo ya mwanae kwa kumfuatilia mwenendo wake kila siku na kubuni mbinu za kumsaidia kila anapoona hafikii malengo yake.
Wazazi wengi wamekosa kufuatilia elimu za watoto kwa kuendekeza ulevi na kutozingatia ratiba za kurudi nyumbani, jambo hili ni baya kwani linaweza kuharibu mwenendo wa mtoto ambaye anatakiwa kuongozwa kwa karibu kwa kila jambo.