Jumatano, 17 Oktoba 2012

WALOKOLE HAWAJUI KWAMBA TUKO VITANI.


sasa hivi ukipatwa na tatizo ndani ya kanisa hali huwa kama  hivi

Unapokuwa nje ya kanisa na ukatazama watu walioko ndani ya kanisa unaweza ukakosea sana utakapodhani wako mahali salama penye upendo amani na ushirikiano wa kutosha. Ukweli  wala si hivyo! ijapokuwa ilitakiwa iwe hivyo. Ukiwa ndani ya kanisa ndipo utakapoweza kuona vituko na wakati mwingine mambo ya kukatisha tamaa kabisa Ashukuriwe Mungu ambaye ndiye mwokozi wetu vinginevyo kanisa limevamiwa mno na umbwa mwitu ambao Biblia ilishasema tangu awali. lakini kwa sababu wote tunamfahamu Yesu kwa mitazamo tofauti basi kinachobaki ni kubanana humohumo. Hii ni kwa sababu anayetoa utumishi ni Bwana mwenyewe muumba wa nchi na mbingu. wengine hata wakikukataa lakini kama Mungu amekukubali  hakuna mwingine mwenye mbingu. ujasiri  wetu unabaki palepale kwa sababu hakuna kiumbe aliye juu ya Mungu. 
ma freemason nao wapo waziwazi

Naandika makala hii kwa hisia kali kwa sababu nimeona na kushuhudia mambo mengi sana yasiyopendeza ambayo pengine ni vigumu kuamini kwamba waliyotenda haya ni watumishi wa Mungu huyuhuyu Yehova au wana mungu mwingine anayepingana na Yehova. 
Nafahamu kwamba maisha ya wokovu ni mapambano kwa kila sekunde kama sisi tunavyopanga kuharibu kazi za shetani,na shetani pia naye anapanga kuharibu kazi ya Mungu na kuwapiga watumishi wa Mungu kwa kila mbinu. 
watu watapenda pesa kuliko Mungu


hata kama umeumizwa kiasi gani mshike sana Bwana Yesu usimuache
Katika vita kuna kufa kuumia au kurudi nyuma kujipanga upya na watu wanaopigana vita wanajua jambo lolote kati ya hayo linaweza likatokea na ndio maana unakuwepo utaratibu wa kuwasaidia majeruhi wanaoumia na kuwarudisha nyuma kuwatibu na kisha kuwarudisha tena mstari wa mbele wakishapona majeraha ili kuendelea na mapambano. Lakini kwa sasa hivi katika kanisa hakuna utaratibu wa ki Mungu wa kuwasaidia askari hodari wanaposhambuliwa na kuumizwa na adui. kabla  sijaenda mbali sana naomba niweke tafsiri sahihi ambayo ninaitumia katika makala hii. Ninapoongelea kanisa sina maana ya jengo la mahali fulani au washirika wa mahali fulani! la  bali maana yangu ni watu waliozaliwa mara ya pili, kwa kumwamini Bwana na mwokozi wetu Yesu kristo popote pale walipo katika nchi yetu ya Tanzania. Lakini pia watumishi ninaowaongelea hapa ni wale
watu tunaofahamu jinsi walivyojitoa karibu maisha yao yote katika kumtumikia Mungu. na ikatokea kwa sababu yoyote wakaanguka katika dhambi, lakini baada ya kuanguka wakaonyesha toba hivi ikitokea  akakosea mahali fulani tunaweza tukamnyanyasa kwa kosa moja na tukausahau utumishi wake uliotukuka? Nafahamu kwamba siku hizi kanisa limevamiwa kama ambavyo biblia ilitabili kwamba watatokea waalimu na manabii wa uongo,hao mimi sina shida nao na hata mawakala wao hao wanapaswa kudhibitiwa bila huruma. Lakini ambao wamefanya kazi ya Mungu kwa uaminifu na kwa Muda mrefu na tunawatambua na tunautambua mchango wao wa dhahiri  na katika utumishi wao hawajawahi kufanya kosa au kuanguka dhambini,lakini ikatokea si kwa wao kupenda bali kwa kulazimishwa wakajikuta wameanguka dhambini, na wakajutia sana kosa hilo na kuwa tayari kabisa kutengeneza ili warudi kumtumikia Mungu. je ni haki kuwashindilia na kuwalaani kwa kosa moja tu na kuwazuria utafikiri walishawahi kufanya kosa lingine.

 hivi ina maana kwamba kuna baadhi ya dhambi ambazo hazina toba? au damu ya Yesu ilimwagika bure pale Golgotha. hii inaonyesha kwamba wapo watu ndani ya kanisa la Mungu wanapoona wenzao wanachapa kai ya Mungu kwa ufanisi wao wanaumia roho na kusaga meno kwamba kwa nini huyu anafanikiwa namna hii? hiyo roho sio ya Mungu aliye hai. Unaweza ukathibitisha hili kulingana na kasi ya kusambaratisha huduma ya mtumishi iliyo ndani yake. utona watu ile roho ya kumsaidia mtu ili atengeeze inakuwa haipo bali roho ya kusambaratisha na kuua kabisa,kwa maana ya kuhakikisha kwamba hata kama kuna neema kidogo haipati nafasi ya kuchipuka. hayo ndiyo macho waliyonayo watu wa mungu wa siku hizi. hii ni tofauti kabisa na macho ya Mungu. na Mungu angekuwa anatuangalia kama hivyo wanavyoangalia ndugu zetu hawa,sidhani kama kuna mtu ambaye angeokoka. maana hatukuokolewa kwa sababu tulikuwa wema mbele ya Mungu bali wingi wa dhambi zetu ndio uliozidish neema ya Mungu.Biblia inasema tukisema hatuna hatuna dhambi tunajidnganya wenyewe na wala kweli haimo ndani yetu,lakini tukiziungama yeye ni wa haki atatusamehe. Tusisahau kwamba ni Mungu ndiye anayetuchagua na ndiye muamui wa haki, wanadamu hawana haki ni wepesi wa kuongeza maneno wakidhani kwamba ndio wameshamaliza kazi,lakini Mungu anazo  njia nyingi za kumuingiza Mtu darasani,inawezekana katikati ya matatizo haya Mungu akawa anataka kukuonyesha kwamba siku hizi watu wapo kanisani sio kama ulivyokuwa unawaona na wala sio kama ulivyokuwa unacheka nao. Inawezekana walikualika hata kufanya huduma kwao lakini kumbe ni kwa shinikizo tu la watu wanaokufahamu,kumbe mioyo yao haikuwa na wew kabisa.nawapa pole sana watumishi wote waliosalitiwa, kumbuka Biblia ilishasema watu watasalitiana na ndivyo vitu tunavyoviona ndani ya makanisa siku hizi. naamini kwamba Mungu mwenyewe atawasimamisha,maadamu ameshawabariki. hakuna atakyeweza kuwalaani. tena naamini baada ya hapo mtafanya utumishi mkubwa mara dufu kuliko mlioufanya hapo kabla. Ninapoandika haya nimeona kumekuwa na wimbi kubwa la furaha na vigelegele inaposikika  kwamba mtumishi fulani ambaye amemtumikia Mungu kwa uaminifu sana ameanguka dhambini. Katika hali halisi ingefaa liwe jambo la huzuni sana na ikiwezekana kama majeruhi wa vita sisi wengine tungejitahidi kumhifadhi mahali salama tukimtibu jeraha zake ili akipona tuendelee kuwa naye katika mapambano,lakini sivyo wanavyofanya walokole wa siku hizi,unaweza ukapokea meseji za kukutia moyo kutoka kwa watu wasiomjua Mungu wakikuahidi kukuombea rehema kwa Mungu,lakini sio kwa wapendwa wao watatumiana meseji za kupongezana jinsi ambavyo umeanguka,la kushangaza Biblia inatuambia kwamba ni furaha mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja anapotubu,malaika wanafurahi wanampongeza Yesu na kuisifia damu aliyoimwaga msalabani jinsi inavyofanya kazi,kinyume cha andiko hili tunasema ni huzuni kubwa mbinguni kwa mteule mmoja tu anapoanguka dhambini na Yesu na malaika wake wanatuma damu ya upatanisho ili ikiwezekana watumie kila njia wamrejeshe,Yesu anasema hata kama una kondoo (watu)mia na mmoja akapotea waache wale 99 umfuate huyo mmoja. Lakini walokole hawaelewi hilo.  Ninachojiuliza inakuwaje wewe habari inayomuhuzunisha Mungu wewe ndio inakufurahisha? Mimi nina mashaka na hiyo roho hata kama wewe ni mlokole wa zamani ndani ya kanisa. Ni jambo linalohuzunisha sana kuishi kwa kuviziana.

KUKWAMA KWA MALENGO




Tunaposhindwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea, kwa mfano kufeli mitihani, kushindwa kuendelea na ujenzi au kufanya hiki na kile tulichokusudia, mara nyingi hutuingiza kwenye huzuni, lakini kanuni za mafanikio yoyote duniani zinaanzia katika mkwamo.

Hivyo basi tunapoona tumeshindwa kufikia lengo la kile tulichotaka kukifanya haimaanishi kuwa hatuwezi, bali tumepungukiwa nguvu ambazo lazima tuzitafute kutoka katika miili yetu kwa kutumia uwezo na uelewa wetu ambao ni mkubwa mara 1000 ya tunaotumia kila siku katika maisha yetu.

Unapokuwa umekwama katika kitu chochote, jiulize sababu  kwanini umeshindwa. Baada ya kupata sababu hizo tafakari njia na mbinu mpya za kuelekea kwenye ushindi huku ukiamini kuwa mafanikio yanatokana na juhudi pamoja na kutorudia makosa yaliyoleta mkwamo. Haifai kukata tamaa, hata kamaumekwama mara elfu moja.

Tunapokwama mara kwa mara ni vema tukawashirikisha watu katika kila jambo tunaloona kuwa linasumbua akili, ushirikishaji huo unaweza kutusaidia kupata uzoefu kutoka kwa wenzetu ambao pengine wamevuka vikwazo vikubwa tofauti na hivyo tunavyokabiliana navyo.
Jambo la mwisho la kuzingatia tunapoanza hatua mpya za kuelekea katika ushindi tusikubali kurudia kosa, kama kufeli kwako mtihani kulitokana na kutosoma kwa bidii, usirudie kosa hilo ongeza bidii za kusoma au kama umeshindwa kujenga nyumba kwa sababu ya kuwa na matumizi makubwa ya pesa usikubali kuendelea na matumizi hayo, badala yake jibane na utimize nia yako.

MKE KUANZA/KUACHISHWA KAZI

Inaelezwa katika uchunguzi wa kitaalamu kuwa wanaume wengi huhofia wake zao kuanza kazi, hii inatokana na wivu wa kimapenzi . Wanaume hudhani kuwa mke anapokwenda kuajiriwa atakuwa na nafasi kubwa ya kushawishiwa kuanzisha uhusiano mpya na wanaume wengine.

Lakini ukweli ni kwamba huzuni hii mara nyingi huwa ni ya bure na matokeo yake huzaa wivu ambao husambaratisha ndoa na uhusiano. Kitu cha msingi kinachotakiwa kufanywa na mwanaume ni kuwa karibu na mkewe kumjengea hali ya kujiamini na kumtimizia yote anayostahili kama mke, likiwemo tendo la ndoa na ukaribu ambao mara nyingi unatajwa kuwa tiba kubwa ya usaliti.

Aidha kwa wale ambao wake zao wanafukuzwa kazi, jambo la muhimu ni kutiana moyo na kushirikiana kwa ukaribu kutumia muda wa dhahabu kupata kazi. Hili linatakiwa kwenda sambamba na kujaliana wakati wote wa tatizo. Hali yoyote ya kumtenga na kumwacha mkiwa ni hatari kwa uhusiano.
Pamoja na hilo endapo kipato cha mwanamke kilikuwa ni sehemu ya matumizi ya nyumbani basi mume na mke wanawajibu wa kukaa pamoja na kupanga upya matumizi yao ili kuondoa pato ambalo lilikuwa linatumika kutoka katika mshahara wa mwanamke ambaye kafutwa kazi.

CHANZO: Kutoka katika mitandao