Jumamosi, 23 Juni 2012

TANGA GOSPEL STAR SEARCH TULITHUBUTU.


Baadhi ya waamuzi wa shindano la kutafuta vipaji vya waimbaji wa nyimbo za injili Tanga wakiongoza nyimbo za utangulizi wa Tamasha hilo jukwaani. aliye mbele ni Sister Meclin Ludamila akishirikiana na Hellen Kijazi na Devota Mkanumkole

mara nyingi sana ninapokutana na watu mbalimbali wanaopenda nyimbo za injili wa hapa kwetu Tanga au sehemu nyingine, huwa najisikia mzigo ambao kama sijaongea nao kuhusu namna ya kuinua uimbaji wa nyimbo za injili katika jiji letu la Tanga sijisikii vizuri. najua hali hii imeniletea shida na lawama kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili hapa Tanga, nimepata ujumbe kwamba wakija waimbaji kutoka nje ya Tanga ninawambia kwamba Tanga hakuna watu wenye vipaji. nimekanusha mara nyingi na hata nilipopata nafasi kwenye Tv nilifafanua sana jambo hili. ninachosema na ninachoamini ni kwamba Tanga kuna waimbaji wengi wenye vipawa vikubwa lakini wamekosa 

Fainali zilifanyika katika ukumbi huu wa kanisa la Agape ministry zamani ulikuwa ukumbi wa kuangalia picha za senema uliokuwa ukijulikana kwa jina la Legali hall.


Kwaya ya kanisa la sabato Nguvumali waliimba kwa ustadi mkubwa siku ya fainali za kusaka vipaji Tanga.
kutangazwa. na hii imetokana na tabia ya viongozi wetu kuwa na tabia ya changu ni changu. na kwa jinsi wanavyotiliana shaka na kutokushirikiana, ndivyo na waimbaji wanavyoshindwa kushirikiana na matokeo yake tuna kwaya nzuri zina nyimbo nzuri na tuna waimbaji wazuri lakini hawajulikani kwa watu wa Tanga bali wanajulikana kanisani kwao na kwa wachungaji wao. na hata wakipata nafasi ya kwenda katika sehemu ambayo wataonekana na kukuza vipaji vyao mara nyingi huwa ni vita kutoka kwa wakuu wao wa dini. kwa kweli Tanga ina watu wengi wanaopenda nyimbo za injili lakini sisi waimbaji hatujiamini ukiona mtu ameandaa tamasha basi ujue kuna waimbaji wenye majina kutoka nje ya mkoa ili kuja kusaidia kuvuta watu na wenyewe wameshagundua hili,siku hizi kuwapata ni biashara kubwa sana. mimi niliwashauri marafiki zangu waimbaji kwamba ni lazima sisi wenyewe tuanze kuandaa matamasha yanayotuhusu sisi wenyewe. tutafute marafiki tutengeneze familia yetu ambayo itatusaidia kuandaa matamasha bila kiingilio au kwa kiingilio kidogo sana ili tuwazoeshe watu kuupenda muziki wa injili na kuacha tabia ya kwenda kushangaa maji ya bahari ya hindi ufukweni. lakini pamoja na hayo tuanze na kuwatayarisha vijana wadogo ili kuwaandaa katika misingi ambayo nao watawarithisha wengine. Watoto wanahitaji kulelewa katika malezi yatakayowazesha kuishi katika mapenzi ya Mungu na kukua katika kicho.  Ni muhimu sana kwa kanisa kutambua uwepo na mahitaji ya kuandaa watoto katika kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Najua kwa hakika kabisa 
washiriki wa Tanga Gosper Star Search wakiwa katika mazoezi makali kabla ya kuingia katika mchujo.                                                                                                                                                                        
jukumu hili ni la Kanisa kwa ujumla hapa nina maana ya mwili wa Kristo na sio kanisa kama jengo la mahali fulani. sasa kama kanisa limepoteza hamu au limejisahau kuchukua jukumu lake ni muhimu kuzidi kumuomba Mungu ainue watu wengine wenye uwezo na ama Mungu awape uwezo wa kuisimamia huduma hii ambayo kwa kweli inalegalega. ukipata bahati ya kuangalia kalenda za makanisa mengi yaliyopo hapa Tanga huwezi kupata ratiba ya tamasha lolote la waimbaji kwa mwaka mzima. ndio maana ninadiriki kusema sisi tulithubutu na tumeona kwamba inawezekana tumeandaa                                                                                                                                                                                           

Washereheshaji wa tamasha hili pia walikuwa ni watu maarufu sana katika familia ya waimbaji wa nyimbo za Injili hapo ninamzungumzia solo maarufu wa nyimbo za Injili dada Sheilla Mnyanyi na Daniel Manimba.

Flora Mwakasege akiwa na Wageni  rasmi Rev GH Lee na Grace Gangho Lee ambao ndio walitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza mchungaji Lee ndiye mkurugezi wa Emanuel English medium school lakini pia kwa sasa amefungua studio kubwa ya kisasa ambayo ipo katika eneo la Kange nje kidogo ya mji wa Tanga.
Daniel Dedu na Andrew Mtawa walikuwa na kazi kubwa sana ya kuhakikisha kwamba wanawatengenezea nyimbo washiriki tangu mwanzo wa shindano hadi mwisho.ninawashukuru sana kwa kuwa walionyesha uwezo na vipaji vya hali ya juu sana Mungu awabariki na tunatambua kwamba wao ni hazina ya waimbaji wa nyimbo za injili Tanga.
Mchungaji Bright Mashauri akimkabidhi zawadi ya kumtambua mshindi wa pili wa shindano hilo Earnest Daffa


Kwaya ya vijana wa kanisa la KKKT mikanjuni wakitoa burudani kwa washiriki na waalikwa wa fainali.za shindano la kusaka vipaji Tanga 2012.
matamasha matatu kwa mwaka huu 2012,tumeendesha zoezi la kusaka vipaji na washindi wamepatikana. tunawashukuru sana Novelty Youth Centre,Dr Kijazi na marafiki wengine ambao walitusaidia kufikia malengo. na neno litasimama.
Kwanini wao watamani tu kuona na kushiriki vitu kama kili music award au Bongo star search pasipo kuwapa hamasa katika kuinua vipaji vitakavyo mpa mungu utukufu?
Mkurugenzi wa kituo cha kulea vijana Tanga Nolverty Youth Centre akitoa cheti cha utambulisho kwa mshindi wa tatu wa shindano hilo Yohana Kuziwa ambaye alifanya vizuri sana.

Mwimbaji wa nyimbo za injili wa Tanga Hellen Kijazi ambae alikuwa ni mmoja wa waamuzi wa shindano la kusaka vipaji akitoa burudani kwa washiriki kabla ya kwenda kutoa maoni na ushauri kwa washiriki wa Tamasha.


KUMBUKUMBU YA MIAKA 27 YA NDOA

Mara kadhaa nadhani umekuwa ukisikia habari au hata kuhudhuria sherehe za kumbukumbu za ndoa za wanandoa waliodumu kwenye ndoa zao kwa kipindi fulani. Kila ulipopata kuhudhuria "shughuli hizi" umekuwa ukitafsiri vipi? unazipa uzito wowote?
Katika tukio linaloonekana hapa pichani ni picha za Wachungaji na ambao pia ni waangalizi wa makanisa ya KLPT.Wakimtukuza Mungu kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa bila ya migogoro na mimi ninawatakia maisha mema ya heri na baraka tele.

Wachungaji George na Christina Nywage wa kanisa la KLPT Parishi ya Tanga wakiwa katika sura za furaha na shukrani kwa Mungu kwa kutimiza miaka 27 ya ndoa yao. kumbukumbu hii ilifanyika katika kanisa wanaloliongoza lililopo majani mapana Tanga.
Washirika wa kanisa la KLPT majani mapana Tanga wakienda kuwapongeza wachungaji wao kwa kutimiza miaka ishirini na tano ambayo si kidogo.
ni wazi kuwa kuna umuhimu wa kubadlisha pete sasa maana zile za kwanza ni wazi kwamba zitakuwa zimechakaa kwa sababu hiyo zinahitajika pete mpya katika pendo ambalo kila siku linazidi jana na hii ni mfano mwema wa kuigwa kwa washirika na watu wa Mungu wa Tanga.
Hapa wanapongezana baada ya kuvalishana Pete. hakika inapendeza sana kwako mtazamaji wangu,lakini je wewe umewahi kufikiria kumtukuza Mungu kwa jambo lolote? au unaona kila kitu ni haki yako.
washirika wa KLPT hawakuwa nyuma bali walikuja na zawadi za kuwapongeza baba na mama mchungaji kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwalea watoto wao wa kimwili katika maadili mema ya kuigwa lakini pia kwa kuwatunza watoto wa kiroho waliokabidhiwa na Yesu kristo.


Jumanne, 19 Juni 2012

FURAHISHA GOSPEL

KARIBU KATIKA BLOG YAKO YA FURAHISHA GOSPEL UPATE MASOMO MBALIMBALI YA BIBLIA  
     




lengo na makusudi yetu ni kuelimishana na kujengana kama jamii ya watu wanaomwamini Mungu,tutajitahidi kuweka vitu ambavyo vitakusaidia katika kukupa maarifa mbalimbal


SOMO: KUUTAFUTA KWANZA UFALME WA MUNGU

MWL: Furaha Amon


Utangulizi;

Wakati nilipokuwa nikifiria kuandika hili somo, nilikuwa namkumbuka mchungaji wangu mmoja ambaye alikuwa ni mchungaji msaidizi katika kanisa nililokuwa mshirika. Huyu mchungaji ni kama alikuwa hana swali jingine, kila tukikutana ananisomea mstari huu wa Biblia
“Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”. (Mathayo 6:33)
Halafu ananiuliza nijibu ufalme ni nini? Na haki yake ni nini? Kila jibu nililompa alikuwa haridhiki, halafu yeye mwenyewe hatoi jibu. 

Na kila jibu ninalompa analikataa, hatimaye nikaamua kuwa jeuri na mimi nikawa namjibu kwamba sijui na yeye mpaka wakati naandika somo hili hajawahi kunipa jibu na tumepoteana kwa karibu miaka saba sasa. 

Lakini hii haikunifanya niache kufikiria kutafuta jibu sahihi ya swali hili, kwa sababu natambua kwamba Biblia haijawahi kuweka maandiko hewa, kwa sababu kila andiko lenye pumzi ya Mungu liko hai. Kwa hiyo ni muhimu tukashirikiana pamoja katika kujifunza na kutafakari kwa mapana kuhusu ufalme wa Mungu na haki yake. Biblia inasema;-
Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa na kila mtu hujiingiza kwa nguvu. (Luka 16:16)

Ev F Manyeresa
UFALME NI NINI?
Ufalme ni mamlaka, ni utawala wenye uwezo wa juu wa kufanya maamuzi katika maeneo yanayomilikiwa na ufalme huo. Tofauti na utawala mwingine wa kidemokrasia ambao unatafsiriwa kama utawala wa watu uliowekwa na watu kwa ajili ya kuwatala watu. Ambao ki- msingi hauna nguvu na unaweza kuondolewa tu maandamano ya watu waliokuweka, na kila uamuzi unaofanya unaweza kuhojiwa na taasisi mbalimbali zikiwemo za utawala bora na haki za binadamu. Ufalme ni tofauti kabisa na tawala za kidemokrasia, katika ufalme watu na vitu vyote ambavyo viko katika miliki ya mfalme ni mali yake. Na anaweza akaamua vyovyote anavyotaka bila kuhojiwa na mamlaka yeyote, kwa sababu vitu vyote ni mali yake, ikiwa ni pamoja na watu walioko katika himaya yake.
HAKI NI NINI?
Haki ni hukumu inayotolewa bila ya kuwa na chembe chembe za upendeleo wa aina yeyote kulingana na sheria zinazohusika kutoa haki katika utawala fulani ama wa nchi husika au katika miliki yeyote ambayo watu wanaishi kulingana na sheria zinazowaongoza kama ilivyo kwamba kuna utawala wa Mungu na pia kuna utawala wa shetani.
Mtu mmoja ambaye Biblia inasema ndio mtu mkuu zaidi kati ya watu waliozaliwa na mwanamke Yohana Mbatizaji wakati anawaandaa wayahudi kuhusu ujio wa Yesu,  alikuwa na kauli mbiu moja kubwa ambayo Yohana aliwaambia wayahudi.
Mwl Agnes Sameji

“Tubuni; kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia. Mathayo : 3:2
Kwa maana hiyo Yesu alikuja duniani pamoja na kuleta wokovu kwa wanadamu lakini pia alikuja kuleta ufalme wake. Ufalme wa Mungu, ambao ni tofauti  na ufalme wa dunia hii au ufalme wa shetani.
Kwa kawaida kila utawala unakuwa na sheria zake ambazo zinaweza kuwa za kikatiba kwa maana ya kuandikwa, au kutokuandikwa yaani kwa kutumia amri, lakini Yesu alikuja kuleta ufalme na haki yake na ili uweze kuingia na kuishi katika ufalme huu unahitaji zaidi kujua maana ya haki yake. Tafsiri nyepesi ya ufalme ni kama udikteta sababu unalimbikiza nguvu na madaraka kwa mtu mmoja ambaye ndie mfalme.
Kwa hiyo ili uweze kuwa mfalme mzuri inatakiwa uwe mtu ambaye unazingatia haki katika kutoa maamuzi yako kwa sababu ya nguvu kubwa na mamlaka uliyonayo. Usipotenda haki ni hatari sana kwa watu na vitu unavyomiliki. Kwa maana hiyo Yesu alipokuja kuuleta ufalme wake ni muhimu kujua kwamba ili uishi katika ufalme huo ni muhimu kujua haki yake, kwa maana hiyo haki ndio sheria yenyewe itakayokuwezesha kuishi katika ufalme wa Mungu.

Mrs M Kapinga

SIO LAZIMA HAKI NA SHERIA 
 ZIFANANE KATIKA KILA NCHI
Inawezekana sheria za nchi moja zikawa tofauti kabisa na sheria za nchi nyingine, kwa mfano hapa kwetu Tanzania kutumia mirungi ni kosa, sawa na kutumia madawa ya kulevya mengine kama bangi na heroin. Lakini kwa sheria ya nchi kama ya Kenya, kukutwa na Mirungi sio kosa, huko ni zao la biashara. Na inaruhusiwa kutumiwa na kuuzwa popote. Kwa hiyo raia wa Kenya akija Tanzania analazimika kuacha kutumia mirungi vinginevyo akikamatwa na mirungi akiwa katika ardhi ya Tanzania anakuwa na kosa, hata kama kwao anaruhusiwa, lakini sheria za ufalme wa Tanzania hiyo kitu ni marufuku, hapa lazima apate haki yake ambayo ni kifungo.
kama leo utaenda katika nchi zilizotawaliwa na mfaransa, mfano nchi jirani kama Rwanda na Burundi, wao sheria yao ya barabarani inaruhusu magari yanapotembea barabarani kutumia upande wa kulia wa barabara, kinyume na utawala wa nchi ambazo zimetawaliwa na Mwingereza kama nchi za Tanzania, Uganda na Kenya ambazo magari yanatumia upande wa kushoto wa barabara.

Sasa wewe unapoendesha gari kutoka kwenye utawala wa Tanzania ukaingia Rwanda ni lazima ubadilishe upande wa barabara na kama utaendelea kutumia sheria za barabara za Tanzania katika nchi ya Rwanda basi uwe na uhakika kwamba hutafika mbali kabla ya kugongwa au kukamatwa na watunza sheria wa nchi husika.
Sasa Bwana Yesu alikuja kuleta ufalme wake na haki yake,ufalme aliouleta Bwana Yesu una sheria zake za namna ya kuishi, kwa mfano wewe umetoka kuishi kwenye ufalme wa giza, utapata shida sana kuishi kwenye ufalme wa nuru. Kwa tafsiri nyingine ni kwamba, kinachokuwezesha kuishi katika ufalme wa Mungu ni kwa kufuata sheria ambazo ziko katika ufalme wa Mungu. Na moja kati ya kazi za mfalme ni kutoa hukumu au kufanya maamuzi ya haki, Biblia inasema;-

Tazama, Mfalme atamiliki kwa haki. Na wakuu watatawala kwa hukumu (Isaya 32:1)

Kwa maana hiyo Yesu anapoongelea haki kama kitu muhimu katika kuupata ufalme wake. Maana yake ni lazima wakati wote tusimame katika kweli na haki ndipo ambapo tutakuwa tunaishi katika ufalme wa Mungu. Na  hii inamhusu mtu binafsi jinsi anavyoyatawala mazingira yake, familia yake, jamii yake, mji na Taifa kwa ujumla. Kitu cha kwanza ambacho kinaashiria kwamba ufalme wa Mungu uko ndani yako, ni jinsi ambavyo wewe unaamua mambo mbalimbali katika familia yako, kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani zako, sehemu yako ya kazi, kwa watu walio juu yako na kwa watu walio chini yako.
Ni namna gani unavyoamua mambo yao. Je unaamua kwa haki au kwa woga na upendeleo? Je wewe mwenyewe unapokosea upo tayari kukiri kosa lako? Kama unaamua kwa haki, na unatimiza mambo yote, basi uko ndani ya ufalme wa Mungu na utakuwa na nguvu katika kutawala mahali popote utakapokuwa katika ulimwengu wa roho na mwili.

“Na alipouzwa na mafarisayo, ufalme wa Mungu utakuja lini? aliwajibu akawaambia ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;. Wala hawatasema tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama ufalme wa Mungu umo ndani yenu” (Luka 17:20-21)

Ufalme wa Yesu hautaonekana kwa kila mtu. Yesu alikuja na kuleta ufalme wake na akasema ufalme wa Mungu upo hata sasa ila ni siri kuujua na ukiugundua utaishi maisha ya kifalme bila kujali mazingira utakayopitia.
Mambo yanayohusu ufalme wa Mungu ni mambo ya siri. Na ni muhimu kujifunza masomo kama haya ili uweze kupata ufunuo wa siri ambazo ziko kwenye maandiko. Ndio maana Yesu anawaambia wasifikiri ufalme wa Mungu utaonekana waziwazi au tutautazama toka mbali.

Wakati ninatafakari mambo haya nikaona nitafute mtu mmoja ambaye alipitia maisha magumu lakini bado alijitahidi kuhakikisha anaishi akiwa ndani ya ufalme wa Mungu.
Hebu tuangalie kidogo maisha ya Yusufu mtoto wa Yakobo. Huyu alipata bahati ya kupendwa na baba yake kama ambavyo Biblia inasema;-
“Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia wala hawakuweza kusema naye kwa amani”. (Mwanzo 37:3-4)
Ukifuatilia kwa makini kisa hiki cha kusisimua unaweza kujifunza mambo mengi sana aliyopitia Yusufu ambayo yanasikitisha na kuumiza sana nafsi hata ya msomaji, wengi tunajua kuwa kulikuwa kuna tabia ya upendeleo katika taifa na tunajua kwamba hata isaka alimpenda sana mwanae wa kwanza Esau na Rebeka akampenda zaidi Yakobo, inawezekana kwa sababu ya tabia zao, maana Esau alikuwa mwindaji aliyeleta nyama nyumbani na Yakobo yeye alikuwa kama mtoto wa mama akishinda nyumbani kumsaidia mama kazi. Tunajua uadui ambao ulitokea kwa Esau na Yakobo ambapo ilibidi Yakobo akimbie maana ndugu yake aliapa kumuua. Lakini cha kushangaza Yakobo naye anafanya kosa kama hilo la baba yake la kuonyesha kumpenda Yusufu kuliko watoto wake na hivyo kusababisha chuki kwa ndugu zake ambao yeye aliwapenda na kujisikia yupo salama akiwa karibu nao, lakini matokeo yake walitaka kumuua na hatimaye kuishia kumuuza kwa potifa akida wa jeshi la farao. Biblia inasema;-
“Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao waishmaeli waliomleta huko. Bwana akawa pamoja na Yusufu naye akasitawi naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, Yule Mmisri. Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake. Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake. Na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake. Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo. Bwana akabariki nyumba ya Yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba. Akayaacha yote aliyokuwa nayo mikononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu chochote chake, ila hicho chakula alichokula tu.” (Mwanzo 39:1-6)

Katika maandiko haya tunaona kwamba pamoja na ugumu wa mazingira ya maisha ya Yusufu, kutoka kwa baba  yake mzazi aliyempenda na kumshonea kanzu ndefu na kuwa mtumwa wa mkuu wa majeshi katika nchi ya kigeni, hapo inahitaji uwe na moyo safi usio wa kawaida ili uweze kumuona Mungu na kuuvuta ufalme wake.
Prof G K Nywage KLPT Tanga
Lakini tunaona Yusufu aliweza kutulia na kutawala katika nyumba hiyo ya potifa, alikabidhiwa kila kitu kasoro mke wa Potifa na chakula cha potifa, hapo kwenye chakula nafikiri ni kwa sababu ya usalama kwa sababu huyu Potifa ni mkuu wa majeshi na huyu kijana ni raia wa kigeni kwa hiyo kiusalama hawezi kumwandalia chakula. Lakini mambo mengine yote alikuwa anaamua yeye, akiamua kuchinja ng’ombe, kuku, bata n.k.
Lakini baadae linatokea tena balaa lingine mke wa bosi wake anaanza kumtamani azini naye, sharia hiyo ni kinyume na sharia za ufalme wa Mungu, huyu mama alikuwa anataka kuizima nuru ya ufalme wa Mungu na haki yake Yusufu akaona sio sawa akaamua kukimbia. Tunafundishwa katika hili kwamba dhambi ya zinaa inakimbiwa usijadiliane nayo. Baada ya kitendo hicho hatimaye Yusufu anajikuta yupo jela, mazingira yamebadilika tena kutoka mtumwa aliyekabidhiwa kila kitu na kuwa mfungwa jeuri asiye na adabu anashitakiwa kwa kosa la kutaka kumbaka mke wa bosi wake, Biblia inasema;-
“Ikawa baada ya mambo hayo mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia lala nami. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu? (Mwanzo 39: 7-9)
Kwa hiyo Yusufu akajikuta matatani tena lakini bado pamoja na kuwa jela akajikuta ameupeleka tena ufalme wa Mungu kiasi kwamba biblia inasema;-
“Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu akamhifadhi. Akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza. Mkuu wa gereza akawatia mikononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya. Wala mkuu wa gereza hakuangalia neno lililoko mkononi mwa Yusufu kwa kuwa Bwana alikuwa pamoja naye. Bwana akayafanikisha yote aliyoyafanya”. (Mwanzo 39:21-23)
Hapa tunaona Yusufu anajikuta anaishi tena kama mfalme ndani ya gereza! watu wote wamewekwa chini yake, kwa hiyo na mipango yote ya kazi juu kazi gani zifanyike na nani azifanye alikuwa anapanga yeye. Mtu mwingine anaweza akafikiria kwamba ilikuwa kazi rahisi sana, lakini matukio yote mawili yaliyompata yalikuwa yanaiharibu kabisa nafsi yake, kumbuka waliotaka kumuua ni kaka zake ambao kwa kawaida walipaswa kuwa walinzi wake yaani kujihisi kuwa salama ukiwa nao, na hakuwa na kosa kwa sababu sio yeye aliyemwambia baba yake mzazi ampendelee, mbele za Mungu alikuwa na haki.
Rev Semsey
Fikiria inavyouma kutenganishwa na baba yako ambaye unajua kwamba yeye ni kipenzi chako, wakati mwingine unaweza usijifikirie wewe zaidi bali ukafikiria ugumu wa zile taarifa atakazopatiwa kuhusu wewe na uchungu atakaokuwa nao akikaa huku anaamini kwamba umekufa. Biblia inatuambia mzee Yakobo aliomboleza kwa siku nyingi sana na akajiapiza kwamba mpaka siku anakufa atakuwa anahuzunika kwa ajili ya mtoto wake aliyempenda sana. Halafu anafika ugenini mambo yameanza kukaa sawa halafu linkuja balaa ambalo unazushiwa jambo na mtu ambaye ndio kama mama mlezi wake, harafu anakuwa huwezi kujitetea, kisha anatupwa kwenye gereza ambalo sio la kawaida tunaambiwa ni gereza wanalofungwa wafanyakazi wa mfalme na viongozi wengine wakuu, magereza ya namna hii ni magereza wanayofungwa wahaini. Maana kuwakosea viongozi ni sawa na kuasi, haya matukio mawili pekee yalitosha kabisa kumkatisha tamaa, na pengine ingemfanya atumie muda mrefu sana kutuliza maumivu na majeraha aliyoyapata kutokana na majanga aliyopata. Lakini yeye alikubaliana na mazingira yote aliyopitia na kuhakikisha anautafuta ufalme wa Mungu na haki yake. Ambayo hatimaye alijikuta Mungu amemuinua kutoka gerezani hadi kuwa waziri mkuu. Hii ni habari ya ajabu sana. Yusufu anakuja kuivusha dunia katika kipindi kigumu cha miaka saba ya njaa. Na tunaona jinsi anavyoungana na ndugu zake katika namna ambayo inasisimua sana.
Mr & Mrs Mboya
Kiasi ambacho unaona kabisa anavyowapenda kiasi cha kutoka machozi. Kuna wakati fulani Mungu anatulazmisha kukaa kimya hata tunapozuliwa mambo magumu sana. Shetani yuko kila mahali na kwa viwango tofauti. Shetani anayeishi kanisani anakiwango kikubwa kuliko shetani anayeishi vilabuni na kwenye madangulo. Wakati mwingine uongo unaotengenezwa ndani ya makanisa unakuwa ni mbaya zaidi kuliko unaotengenezwa vilabuni na kwenye madangulo. Mtumishi mmoja rafiki yangu alikuwa na neema kubwa sana kanisani kwake, kiasi kwamba washirika wengi walikuwa wanakwenda kwake kuombewa na kufanyiwa huduma zingine za kiroho, na wengine walimwalika maeneo mengine mbalimbali majumbani kwao, hali hii haikumfurahisha shetani na wajumbe wake wakasema yeye ni nani anataka kujifanya zaidi ya mchungaji, wakaamua kutengeneza fitina wakajipanga vizuri na kuweka ushahidi wa uongo kwamba huko anakokwenda kufanya huduma anazini na wakaweka watu kiasi cha kwamba neno hilo lilipofika kwa mchungaji mchungaji akaamua kuitisha kikao cha wazee na kusikiliza ushahidi ule wa kupangwa na wakaamua kufanya maamuzi ya kumfukuza Yule mtumishi kanisani kumtangaza katika makanisa yote katika jji lile ili asipokelewe na kumtumikia Mungu kwa namna Yeyote. Waswahili wanasema watu watakunyima chakula lakini hawakunyimi neno.
Habari zikamfikia Yule mtumishi juu ya kila kilichoongelewa na uamuzi ambao umechukuliwa dhidi yake, alikasirika na kukata tamaa kabisa akapania kwamba wakimwita kwenye hicho kikao, ndio watajua kwamba kukaa kwake kimya sio kwamba hajui kusema. Kwa hiyo alipania kwenda kupambana nao kwa akili zake yaani kuwapa vidonge vyao. Siku iliyofuata wakati huo hakuna simu alitumwa mjumbe kuja kumwita aende kanisani kukutana na mchungaji, anasema wakati analetewa huo ujumbe alikuwa yupo kitandani lakini hana usingizi bali anapangilia maneno magumu atakayokwenda kuwapaka wabaya wake mbele ya wakuu wake wa dini. Kwa hiyo baada ya kupata huo ujumbe huku akiwa na hasira kiasi kwamba hata wakati anavaa nguo alikuwa anatetemeka kwa hasira. Wakati anatoka chumbani kwake kwenda sebuleni ilia toke kwenda nje ndipo akaona kitndo ambacho sio cha kawaida. Vile anafungua tu mlango anakutana na mtoto wake ambaye alikuwa ni mdogo sana hajui hata kuongea, anakaribia miaka mitatu hivi akasimama halafu akamwambia kwa sauti ya ukali, huku amemnyooshea kidole “wewe nakwambia usiende kuja juu kanisani, umesikia, nasema usiende kuja juu kanisani” huyu mtumishi akashituka inakuwaje mtoto ambaye hajui hata kusema aongee kwa ukali namna hii! Akamwita kwa jina lake akamuuliza kwa upole unasemaje mwanangu, akaona yuko kimya wala haelewi hata anachoulizwa. Ndipo akajua kuwa hiyo ni sauti ya Mungu na ikabidi kutii huku machozi yanamtoka.
Mrs F Mwakasege

Alipofika kwenye kikao alionekana mtulivu sana maana maneno yaliyokuwa akiambiwa alikuwa anayajibu kwa utlivu na hekima ya hali ya juu. Mwisho Askofu wake anamwambia kwa kweli tulikuwa tumepanga kukufukuza na kutwanya barua nchi nzima ili usipokelewe, lakini kwa jinsi ulivyoongea kwa ushirikiano hatuoni kosa lako, lakini pamoja na hayo mimi nakuruhusu uende kesho uniletee jina la kanisa lingine unalotaka kwenda, maana hapa umeshachafuka sana. Akwajibu basi sawa. Sasa kivumbi kikatokea wakati wanasema tuombe kwa ajili ya kufunga kikao, anasema ilishuka nguvu kubwa na kila mtu alianguka chini na kunena kwa lugha kama watu wanaoomboleza na hawakuacha mpaka mama mmoja alipopata ufunuo na kuwaambia jamani hili jambo liishe na huyu mtumishi asiondolewe hapa kanisani, ndio wakapata nguvu na kutawanyika. Na baada ya siku si nyingi wale watu waliopanga uovu huo wakaeleza ukweli kwamba walipanga maneno.
Mwisho napenda kukushauri ndugu yangu utafute kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na mengine yote utazidishiwa.

MUNGU AKUBARIKI. 

Tunaweza kuwasiliana na mimi kwa namba ya simu 0677  

609056








Furahisha gospel is expected to be an inspiring site for Christians and non christian where a word of God shall be shared and to be a platform for discussions on different christian affairs. Be free to give your views and contributions for the benefits of body of Christ.

HARUSI YA ELIZABETH YOHANA
huyu ni dada Elizabeth Yohana Allen akiwa katika vazi rasmi siku ya kubariki ndoa yake,kwa hakika ilikuwa ni siku ya furaha kwake na kwa marafiki zake baada ya kufanikisha siku hii.
Elizabeth akiwa na mpambe wake wakijiandaa kuelekea kanisani KLPT Majani mapana

mpambe wa Elizabeth Mrs Sakala akiwa na furaha katika kutekeleza jukumu lake kwa ufanisi

Wasindikizaji wakiwatoa bwana harusi mbarikiwa kuingia katika gari la maharusi






Furaha