Jumatano, 22 Februari 2017

LAANA NI NINI?

LAANA NI NINI?

Laana ni mkusanyiko wa mabaya yote yanayompata mtu: misukosuko katika kazi au ndoa n.k. laana huleta mateso mengi.
Katika kumbukumbu imeandikwa 
Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo. 21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. 22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie. 23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. 24 Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie. 25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani. 26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza. 27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. 28 Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; 29 utakwenda kwa kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa. ). KUMBUKUMBU 28:20-29 
Haya ndiyo mambo yanayowatokea wanadamu hata sasa. Unapotumia maneno ya kinyume dhidi  yako, maneno hayo hugeuka na kuwa laana. Yale unayoyaona kwa sasa ni matokeo ya maneno uliyowahi kutamkiwa au  kujitamkia  mwenyewe: Hii ni  kwa sababu Biblia inasema "maneno ni roho". Na unapotaka kuwa huru dhidi  ya laana, anza kwa kushughulikia chanzo cha tatizo. Chombo cha kupokelea laana yoyote ile ni DHAMBI. Bila dhambi, laana haiwezi  kukupata, na hii ni kwa sababu Biblia inasema  
Kama shomoro katika kutangatanga kwake,  Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake;  Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.MITHALI  26:2
Laana ikikosa pa kwenda inamrudia yule anayeituma kwa maana ya aliyeinena. Unapaswa kuchukua hatua kwa kumwendea Bwana nje ya lango, na Bwana atawashikisha kishindo maadui zako kama ambavyo wale wakoma wanne nje ya lango walipoleta ufumbuzi wa tatizo la njaa kule Samaria.
Wapo watu waliojifungia ndani lakini wana matatizo mengi sana na ambayo chanzo cha hayo matatizo ni viumbe wa rohoni. Mtu unapokuwa na dhambi, laana hukaa. Inategemea na maamuzi unayochukua katika maisha yako. Kupitia ulimi wako unao uwezo wa kuamua hatima yako itakuwa je!!? Chagua leo kuwa na uzima ili uishi au uendelee kuwa na dhambi upate mauti, kwa kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti". Zipo laana za wanadamu, laana ya Mungu, laana ya wachawi, laana ya kumuibia Mungu zaka n.k.   
BIBLIA INATUFUNDISHA AINA MBALIMBALI YA LAANA:
 Laana ya kuchonga au kuifanya sanamu. 
 “Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina). KUMBUKUMBU 27:15

Laana ya Kuondoa mpaka. Wapo watu wanaoweza kuondoa mpaka wa maisha yako. 
(Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.) KUMBUKUMBU 27:17 

Kitendo cha kumpotosha mtu nayo ni laana.  
(Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.). KUMBUKUMBU 27:18

Laana ya Kutowaheshimu wazazi.  Hii huleta laana kwa maisha yako. 
(Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.).  KUMBUKUMBU 27:16...

Pia imeandikwa katika 
 (Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.). WAEFESO 6:1-3 

Wapo watu wengi sana wanajisahau wakeshafika mijini, na matokeo yake mabo yao hayawezi kunyooka.


Laana ya Kudhulumu haki ya mtu. 
(Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina. KUMBUKUMBU 27:19

Laana ya Kulala na mke wa Baba yako, 
Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.). KUMBUKUMBU 27:20 
Hii ni kama Reubeni alivyofanya, wakati huo mzee Yakobo alilaani kitendo kile cha Reubeni kuwa asiwe mkuu kwa kuwa aliuruka mpaka kama maji. Imeandikwa katika 
(Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. 4 Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.) MWANZO 49:3-4....

Laana ya Kulala na wanyama. 
(Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.) KUMBUKUMBU 27:21...

Laana ya Kulala na dada yako. 
imeandikwa 
(Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.). KUMBUKUMBU 27:22 
Mfano rahisi ni Amnoni mwanane Daudi aliyelala na dada yake Tamari, na mwishowe akaja kuuwa na nduguye aitwae Absalom.

Laana ya Kulala na mkwe wako (mama wa mke wako). Imeandikwa katika 
(Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.KUMBUKUMBU 27:23

Laana ya Kumpiga mwenzako kwa siri. Hii ni kama vile kumsema mwenzako, au kumsengenya. 
 (Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.) KUMBUKUMBU 27:24 

Laana ya Kuua mtu au kutoa mimba. Imeandikwa katika 
 (“Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.”) KUMBUKUMBU 27:25.... 


·                     Laana ya kutoshika sheria ya Mungu. Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 27:26Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina”).


·                     Laana ya Kumlaani aliyeokoka. Hata kama wewe ni mzazi, laana ya aina hii yaweza kukurudia kwa kuwa tayari wewe umebarikiwa.


·                     Kutenda kinyume na maneno ya watumishi wa Bwana. Wengi wa watu wameharibikkiwa hapa. Na hili linathibitishwa pale  ambapo mambo fulani unayotaka yaondoke katika maisha yako lakini hayaondoki. Kuhani ni daraja kati ya hiyo madhabahu na Mungu katika ulimwengu wa roho. Endapo utatenda kinyume na kuhani wako au kusema vibaya juu  ya kuhani  huyu ujue ni laana.



DALILI ZA MTU MWENYE LAANA

Tunajifunza kuusu hizi dalili ili kukusaidia wewe pale unapoona mtu mwenye dalili hizo au wewe mwenywe ujue kuwa utafanya kitu gani. Shetani ni mshataki wetu mbele za Mungu, lakini Biblia inasema katika UFUNUO 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.” Lengo la laana ni kumzuia mtu asiende pale ambapo Mungu amekusudia wewe kwenda.



Zifuatazo ni dalili za mwenye laana:



1.       Kutofanikiwa kwa kila uendako. Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 28:16 (Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.). Kwa nini inakuwa ngumu kwa mtu mwenye laana kufanikwa? Ni kwa sababu unalaaniwa mjini na unalaaniwa mashambani. Wapo wanaokimbia kufanya biashara zao mijini wakakimbilia vijijini, lakini hilo nalo halisaidii, kwa sababu hata huko laana inakufuatilia. Inapotamkwa baraka kwako, ni vizuri kujua ni Baraka ya aina gani anakutamkia. Kama ni kupata watoto, na aseme “Ubarikiwe upokee watoto” na wewe useme “Amen”.

 Yupo mtu mmoja katika Biblia ambaye alibarikiwa wakati wa kwenda na wakati wa kurudi. Huyu ni Yakobo. Wakati wa kuondoka alibarikiwa na Isaka babaye, na kupitia Rebeka mama yake akapata Baraka zilizokusudiwa kwa nduguye Esau.

2.      Kukosa mwelekeo (KUMBUKUMBU 28:33). Wapo watu wa aina hii, leo yupo Kanisa la Siloamu kesho yupo KKKT n.k. Hata hivyo, kokote unapodondokea, watu wanajua hakika huyu mtu anazo dalili za laana.

3.      Kutokupiga hatua katika maisha. Miaka nenda rudi,  mtu anabaki kuwayule yule. Ukiziona dalili kama hizi, achana na kitanda,  anza kuchukua hatua kwa kufanya maombi ya kushindana.

  (Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. 2 Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. 3 Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita4 Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao. 5 Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili.). YOSHUA 6:1-3 ... 
Tena imeandikwa katika YOSHUA 6:26 ... (Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.)... Ni  kwamba,  laana zimeodoka lakini asiwepo mtu wa kuujenga upya tena Yeriko. Laana zinapoondoka Baraka hutokea.  Na chapa ya mwanakondoo itawekwa kwenye paji la uso wako. 

 Utimilifu wa ile laana aliyotamka  Yoshua ipo katika 1WAFALME 26:34...(Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua  mwana wa Nuni.).

  
UKIRI
LEO TUNATAMKA,  NA KILA ATAKAYEKULAANI JAMBO LIWEPO  LA KUMPATA.
KWA JINA LA YESU, BWANA YESU NINAKUJA MBELE ZAKO, NINAOMBA UNISAIDIE.




Unachotakiwa sasa ni kutoruhusu chombo cha kupokelea laana kisipatikane kwako, yaani usiwe na DHAMBI. Usiwepo mlango wowote wa laana katika maisha yako. Wewe ambaye hujaokoka leo ni siku  muhimunsanakwako  kumpa Yesu maisha yako