Jumanne, 11 Februari 2014

KIKOMBE CHA BABU LOLIONDO NA KANISA LETU.

watu toka nchi mbalimbali wakipata kikombe cha dawa kwa babu

waheshimiwa watunga sheria wakipata tiba ya asili kwa babu

picha iliyotengenezwa ikimuonyesha babu akiwa katika kilele cha umaarufu kuliko mtanzania yeyote wa wakati wake


Kanisa la Tanzania limekuwa likipita katika majaribu mbalimbali ambayo yanaacha mafundisho mengi na maswali ambayo yanataka majibu sasa. Mojawapo ya majaribu yaliyotikisa kanisa na taifa kwa ujumla ni pale 
alipotokea mchungaji mstaafu wa KKKT Babu Mwasapile wa Samunge na dawa yake ya kutibu maradhi mbalimbali sugu ikiwa ni pamoja na

ukimwi,kisukari na kansa,hapo ndipo kanisa linatakiwa lijifunze kwamba bado halijasimama sawasawa katika kushughulika na imani za watu juu ya uponyaji wa imani. Hapo nina maana kwamba babu wa Samunge hakutumia uchawi katika kushawishi watu bali alitumia imani kwamba ameoteshwa na Mungu kuhusu tiba hiyo.

 na watu walikwenda kwa imani na wakapokea kwa imani na wakakili uponyaji kwa imani. Na kwa kweli wengi waliokwenda wakati ule waliporejea walionyesha mabadiliko Fulani katika afya zao kimwili. Pamoja na masharti ya babu kwamba hakuna kuchukuliana dawa hiyo na ni lazima akupe mwenyewe badohayo masharti  hayakuwafanya watumishi kujiuliza na ni wachache sana waliweka misimamo ya kuikataa huduma hii ya babu wa loliondo na kwa kufanya hivyo walionekana kama watu wenye wivu kwa mtumishi mwenzao ambaye sasa amestaafu vyovyote ilivyokuwa wote tunajua ile huduma ilikufa kifo cha kawaida,leo hii hakuna mtu anayekwenda tena kwa babu na wataalamu wameshindwa kuthibitisha kwamba


misururu ya magari mbali mbali iliyoleta wagonjwa na wasio wagonjwa kwenda kunywa dawa dawa ya Mugariga katika kijiji cha Samunge wilayani Loliondo, aliyooteshwa na Mzee Mwasapile mwaka 1991.


Mchungaji Ambikile Mwasapile akifuata dawa katika nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Samunge.Dawa hiyo ikishachemshwa huingizwa ndani na kuiombe kisha kuwanywesha wgonjwa.

Gari inayoonyesha namba za usajili SM, ni mali ya Manispaa ya Arusha. Gari hili ni moja ya magari ya Serikali yakiwa nayo yanasonga mbele kwenye foleni ya kunywa dawa inayogawiwa na mchungaji Mwasapile kwa kikombe abiria wakiwa humohumo ndani ya gari.

watu wakiwamo waasia mbalimbali kutoka Mkoa wa Arusha, Manyara na sehemu kadhaa za Tanzania na nje ya Nchi wakisubiri dawa ya Mugariga kwa ajili ya kujitibu.


*NI KWA MCHUNGAJI ANATIBU KISUKARI, PUMU, SARATANI NA UKIMWI

MAELFU ya watu, wakiwemo vigogo wa serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa nchini, walifurika katika Kijiji cha Samunge Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro kupata 'dawa ya maajabu ya Mungu' inayodaiwa kutibu magonjwa mengi sugu ikiwamo Ukimwi.


Helkopta za wafanyabiashara na magari zaidi ya 1,000 yakiwamo magari ya serikali, binafsi na mashirika ya kimataifa ikiwamo Umoja wa Mataifa (UN) na Jumuiya ya Afrika Mashariki, yalifurika katika kijiji hicho kilichopo umbali ya takriban kilometa 400 kutoka Jiji la Arusha.

Dawa hiyo, liy

okuwa inatolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (76), ambaye anasema alioteshwa na Mungu kuitumia kutibu tangu mwaka 1991.

Mchungaji Mwasapile ambaye alifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi Jumapili nyumbani kwake wakati akiendendelea kutoa dawa kwa wagonjwa wake, anasema ndoto hiyo aliendelea kuota mara kadhaa hadi Agosti 26 mwaka jana alipoanza rasmi kutibu.

Anasema dawa hiyo inatokana na mti aina ya mugariga na yeye pekee ndiye anaweza kukupatia na kunywa kikombe kimoja pekee na ukinywa tu inaanza kazi ya kutibu maradhi sugu ya ukimwi, kisukari, pumu na saratani.

Mchungaji Mwasapile anasema gharama za dawa hiyo ni Sh500 tu na dozi yake ni kikombe kimoja tu na hairuhusiwi kurudia kuinywa. Kabla ya kukamilika mchungaji huyo huiombea dawa hiyo na kuichemsha katika majisafi.

“Mungu ameniotesha kutoa dawa hii kwa Sh 500 aliponiambia hata mimi nilishangaa. Kwanza aliniambia niwape watu wapone saratani, kisukari, pumu na magonjwa mengine na baadaye akanionyesha kuwa dawa hii niwape hata wagonjwa wa ukimwi na watapona,“ anasema Mwasapile. Habari hii imeandikwa Mussa Juma na Daniel Sabuni, Loliondo.