Alhamisi, 29 Novemba 2012

JOSE CHAMELEONE BILIONEA ALIYEJARIBU WOKOVU



ninaweza kusema hivyo kwa sababu ilishawahi kutangazwa sana katika vyombo vya habari kwamba gwiji wa nyimbo za duniani mganda Jose chameleone ameokoka. hii ilikuwa ni baada ya kupata maradhi ya kuweweseka katika usingizi na hatimaye kujitupa chini kutoka katika ghorofa ya pili katika hotel aliyokuwa amepanga mjini Arusha. Baada ya tukio hilo bingwa huyu akatangaza kuja kwa Yesu. Lakini hakuendelea zaidi na sijui siri ya moyoni mwake,lakini Biblia inatufundisha kumtambua mtu aliye na Yesu,naamini bado muda upo na nafasi bado iko na Bwana anatamani amtumie wakati huu na sio wakati akiwa amechoka au amekuwa dhaifu kiafya. Najua unajiuliza kwa nini ninamwita Bilionea!




Ndiyo, kwa asiyeamini, hebu angalau baadhi ya mambo yanayothibitisha utajiri wa nyota huyo. 
Anamiliki jumba la kifahari katika vilima vya Sekuku jijini Kampala, pia ana nyumba huko Arizona, Marekani, achilia ile ya Kigali, Rwanda aliyoinunua hivi karibuni kwa mamilioni ya shilingi. 



Ukiachilia mbali gari la kisasa aina ya Cadillac Escalade lililomgharimu zaidi ya Sh milioni 100, Chameleone ambaye ni baba wa watoto watu, pia anamiliki Mercedes Benz, BMW na aina nyingine za magari. 
Kwa ujumla, anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Sh bilioni 1.5 kwa fedha za Tanzania. Na anasema bado anazisaka, kwani bila ya kuwa na tamaa ya kusaka mafanikio zaidi, ndoto huenda zisitimie. 



Anayasema hayo akisisitiza kuwa, baada ya nyumba, magari na akaunti nono benki, sasa ana ndoto za kumiliki helikopta yake, baada ya kuwa amekuwa akikodi mara kadhaa ama kwenda katika matamasha au kama alivyofanya wakati anamuoa mkewe Daniela Atim.
pia ana jumba lipo karibia na ufukwe wa ziwa victoria kwa upande wa uganda,pia ana apartments kibao huko uganda,hilo cardillac ni zaidi ya million 250 za kitanzania,Ukija kina Bobby winne na Bebe Cool wanamiliki hadi meli na Hummer hizi wanazotembelea kina 50 cent.anakumbuka akiwa na Bebe Cool na Redsun alipata fursa ya kutumbiza katika shindano la kumsaka mrembo wa Kenya. Anakiri hapo ndipo milango ya neema ilipoanza kufunguka. anasema Dorotea ,baada ya kuzoeana alimshawishi ahamie nyumbani kwake badala ya kuendelea kulala studio,ushawishi ambao ulimchukua zaidi ya wiki moja kumkubalia.




 “Nilipohamia tulikuwa marafiki, lakini mengine yaliibuka tukiwa katika nyumba moja. Mara nyingi kila akitoka, alinikuta nimetulia naandika nyimbo, huku akihoji ni lini nitarekodi. Nilikosa jibu kwa kuwa siku wa na fedha. 

Siku moja akiwa safarini huko Afrika Magharibi aliniachia bahasha yenye dola za Kimarekani 1,000 (karibu Sh milioni 1.8 za Tanzania kwa sasa), akaniambia niingie studio ana. 


“Huo ukawa mwanzo wa kibao Mama Mia na sikuamini kama fedha ile ingebadilisha maisha yangu na kunifikisha hapa nilipo. Mengine yanabaki kuwa historia,” anasema. 

Pamoja na utajiri aliovuna kupitia muziki, nyota huyo anasema historia ya kushuhudiwa `Live’ na watu zaidi ya bilioni 9 akitumbuiza wakati wa Kombe la Dunia kwake ni kitu cha kipekee. 

“Mtoto wa Afrika tena Afrika Mashariki kupewa heshima ile haikuwa kitu kidogo. Najiona mwenye bahati na ni mastaa wachache wanaweza kuingia katika kundi la bahati hata wangeishi kwa miaka 1000.” 

Anasema kutokana na baraka alizopata maishani, ameamua kuanzisha taasisi ya Chameleone ili aweze kuwasaidia wasiojiweza. 

“Nikiwa mdogo sikuwa na maisha mazuri, sikutoka katika familia bora, kwa hiyo ninajiona mwenye wajibu wa kuwasaidia wengine wakianzia katika misingi mizuri ya kielimu. “Nimeshanunua eneo kwa ajili ya kujenga kituo. 

Nataka jamii siku moja inikumbuke kwamba niliwika na kuitangaza nchi yangu, lakini pia sikuwa mchoyo, bali niliyatumia vyema matunda ya muziki. 


Kwa kufanya hivi, naamini ipo siku nitawashawishi wengi kufanya mambo makubwa kwa ajili ya jamii wanayotoka.” 

Huyo ndiye Joseph Mayanja ambaye pamoja na misukosuko ya maisha tangu akiwa shule hadi sasa akiwa staa, bado nyota yake inang’ara. 


Je, atazidi kupata mafanikio? Bila shaka ni jambo la kusubiri na kuona, hasa ikizingatiwa kuwa, mwenyewe amejijengea falsafa ya kutolewa sifa, bali kazi kwa kwenda mbele. 

Pamoja na yote, Chameleone anapaswa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengi wa Kitanzania ambao huvuma kwa muda mfupi, lakini 

wakishazikamata fedha hupotelea kwenye ulimwengu wa anasa na baadaye kujikuta wakiwa `choka mbaya’, tena wakiwa hawana akiba benki wala hawajawekeza.


Chanzo: kutoka katika mitandao mbalimbali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni