Jumatano, 15 Agosti 2012

MAOMBI KUPITIA HEMA YA JANGWANI


HEMA YA JANGWANI(soma Kutoka sura 25 na 26)






Mungu alitaka kuwe na mahali maalumu ambapo Mungu atakutana na watu wake Israel. Mungu akamuagiza Musa atengeneze maskani ambayo itatumika maalumu kwa shughuli za kumwabudu. Hii maskani ilikuwa ni ya hema. Ilikuwa ni ya hema kwa sababu Waisraeli walikuwa safarini kutoka Misri kwenda Kanaani, hivyo nyumba zao zilikuwa za mahema ambayo walipiga na waliposafiri waliyabeba. Hii ndiyo maana hata hiyo maskani ambayo waliitengeneza ilikuwa ya hema. Hiyo hema inajulikana kwa jina maarufu la HEMA YA JANGWANI. Hema ya jangwani ni somo lefu na pan asana. Hatutajifunza somo lote katika Blog hii bali tutajifunza mambo machache sana ambayo yatatusaidia kuelewa kuomba katika Roho Mtakatifu na kupata mpenyo.
Hema ya janngwani ilikuwa ni kama ifuatavyo

Hema hii ilikuwa na sehemu tatu. Patakatifu pa patakatifu ndiko kulikuwa kunakaa sanduku la Bwana. Juu ya sanduku kulikuwepo kiti cha rehema. Upande huu wa kiti na upande wa pili kila upande kulikuwepo makerubi mmoja waliotazamana. Sehemu ya pili yaani
Patakatifu kulikuwepo madhabahu ya kufukizia uvumba ambao ulitakiwa uwake daima, kulikuwa na taa ya vinara saba  ambayo ilitakiwa iwake daima na kulikuwa na meza ya mikate ya wonyesho,mikate ambayo ilitakiwa ibadirishwe kila siku siku kuwekwa mikate mipya. Ua wan je kulikuwa na madhabahu ya kuteketezea sadaka . Patakatifu pa patakatifu aliruhusiwa kuingia kuhani mkuu peke yake,mtu mwingine angeingia angekufa papohapo.
Patakatifu waliingia makuhani wote kwa ajili ya huduma mbalimbali za mahali hapo. Makuhani wadogo hawakuruhusiwa kuingia patakatifu pa patakatifu. Waisraeli wengine wote waliruhusiwa kuingia ua wanje pekee. Makuhani wadogo walikuwa wanafanya shughuli mbalimbali zinazohusiana na ibada, patakatifu na ua wan je.
Mungu alikuwa anakutana na kuhani mkuu,patakatifu pa patakatifu. Kuhani mkuu alikuwa anaingia patakatifu pa patakatifu akiwa amebeba damu ya mwana kondoo kwenye bakuli, ili kuzifunika dhambi zake na za Waisraeli wote. Angeingia bila hiyo damu angekufa. Kuhani aliingia na kukaa kwenye kiti cha rehema. Mungu alizungumza naye pale. Baada ya kuhani mkuu kukaa kwenye kiti cha rehema Mungu alikuwa anashuka hapo kwa udhihirisho wa uwepo wa Mungu uliokuwa ni utukufu wa Mungu wa wingu lililowaongoza wana wa Israeli,usiku nguzo a moto mchana nguzo ya wingu,wingu hilo maarufu kwa jina la Shakina Glory.
Mungu alikuwa hawezi kuzungumza na kuhani mkuu mahali popote pale bali alizungumza na kuhani mkuu patakatifu pa patakatifu tu. Hakuzungumza na kuhani kwenye ua wan je,patakatifu au nyumbani kwa kuhani na mahali popote pale  pengine. Na baada ya kuhani mkuu kuondoka patakatifu pa patakatifu ule uwepo wa Mungu nao uliondoka.
Waisraeli baada ya kufika Kanaani waliendelea na kumwabudu Mungu hapohapo kwenye hema kwa muda wa miaka sana,hadi wakati wa mfalme Sulemani alipojenga hekalu kwa mfano uleule wa hema. Hivyo sanduku la Bwana na vitu vyote vya ibada vilihamishiwa kwenye hekalu. Huduma zote zilizokuwa zikifanywa na makuhani zilihama kutoka katika hema na kuhamia hekaluni humo. Hapo ndipo kukawa mwanzo wa hekalu.(soma 1Wafalme 8:14-21)
Kuanzia hapo ndipo kukaanza kutumika jina la hekalu badala ya Maskani au hema ya jangwani. Wakati wa huduma hii ya makuhani na hekalu,waisraeli wote katika nchi nzima walitakiwa kwenda kupata huduma za maombezi kwenye hekalu hilo. Ambalo lilijengwa Jerusalemu. Hivyo Israeli hawakuruhusiwa kuedesha shughuli za kuabudu mahali popote isipokuwa hekaluni Jerusalemu. Hivyo watu wote waliokuwa na mahitaji yanayohusu ibada,maombezi na huduma zingine zozote za Mungu, iliwabidi waende Jerusalemu,hekaluni waonane na makuhani. Makuhani ndiyo waliokuwa wanazungumza na Mungu kwa niaba ya Waisraeli wote. Huduma hii ya makuhani na hekalu iliyofanyika agano la kale iliishia pale msalabani wakati Yesu alipokufa msalabani. (Luka 23:44-47)
Kama tulivyoona Waisraeli hawakuruhusiwa kuingia patakatifu wao waliishia ua wan je, kama angeingia ambaye si kuhani angekufa hapohapo.  Katika  mlango kulikuwa na pazia la unene wa inchi nne,ambalo halingeruhusu mtu ambaye siye kuhani achungulie ndani hata kama ni kwa bahati mbaya. Baada ya Yesu kufa msalabani Biblia inasema paia la hekalu lilipasuka katikati kiasi cha kwamba mtu yeyote hata ambaye si kuhani aliweza kuona ndani au kuingia hadi patakatifu pa patakatifu na kukaa bila madhara yeyote. Hata kuhani mkuu aliingia patakatifu pa patakatifu na kukaa kwenye kiti cha rehema wala shakina Glory haikushuka. Tangu siku hiyo Mungu hakushuka tena kwenye hekalu.
Tangu siku hiyo Yesu alifanyika kuhani mkuu,yuko  mbinguni ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba anatuombea badala ya kuhani mkuu wa agano la kale. Pamoja na hivyo Mungu alikataa kuendelea kukaa kwenye hekalu la jengo.(angalia Isaya 66:1)
Hekalu la sasa hivi ni watu wa Mungu. Mungu anakaa ndani ya watu wake. Baada ya mtu kumpokea Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yeke,Mungu huja kukaa ndani yake.(Yohana 14:23) kwa hiyo wewe mtu wa Mungu ni makao ya Mungu,wewe ni hekalu (1Wakorintho 3: 16-17) Agano jipya ni kivuli cha agano la kale. Agano jipya ni kivuli cha agano la kale. Agano la kale lilikuwa linaiandaa njia halisi ya kumwabudu Mungu. Hekalu la zamani linafanana na hekalu la sasa.



HEMA YA JANGWANI                                                                            MTU WA MUNGU
(hekalu la zamani                                                                                  (hekalu la sasa)
Ua wan je.                                                                                               Mwili.
Patakatifu                                                                                                Nafsi
Patakatifu pa patakatifu                                                                       Roho
Hekalu la sasa lina sehemu tatu,Mwili,Nafsi na roho. Mwili ni ua wa nje,Nafsi ni patakatifu na roho ni patakatifu pa patakatifu. Agano la kale kuhani alikuwa mtu na hekalu lilikuwa jengo. Hekalu la sasa ni wewe mtu wa Mungu na kuhani ni wewe mwenyewe pia huyohuyo. Hivyo wewe ni vitu viwili katika kimoja. Kuhani wa agano la kale akitaka kuongea na Mungu alikuwa anaianza safari hiyo kutokea nyumbani kwake ,baadae anafika ua wan je, Patakatifu na baadae aliingia patakatifu pa patakatifu. Mtu wa Mungu, wewe mwenyewe ni kuhani na unatakiwa uingie hekaluni mwako kwa imani. Kuhani wa agano la kale alikutana na Mungu patakatifu pa patakatifu tu.hangeweza kukutana na Mungu patakatifu,Ua wan je,nyumbani kwake au mahali pengine popote pale. Wewe mtu wa Mungu ni kuhani pia ni hekalu la leo,patakatifu pa patakatifu pako ni rohoni. Huwezi kukutana na Mungu kwenye nafsi, mwilini au mahali pengine popote pale.(Zaburi 63:1-2) huyu ni Daudi mfalme anajieleza jinsi ambavyo yeye alivyokuwa anamtafuta Mungu mapema akiamka asubuhi sana.kumtafuta Mungu ni kumuomba Mungu. Daudi alikuwa anaamka alfajiri na mapema kabla ya shughuli nyingine yeyote,kwanza alikuwa anamwomba Mungu. Daudi katika maombi yake anasema kuwa,alikuwa na malengo ya kumtafuta Mungu hadi azione nguvu za Mungu na utukufu wa Mungu. Wakati wa agano la kale mambo ya kuabudu yalikuwa hayafanyiki kwa imani kama hivi sasa. Zamani waliabudu kwa vitendo na kwa kuona. Waisraeli walizowea kuona utukufu wa shekina ukishuka wakati kuhani mkuu alipokuwa ameingia patakatifu pa patakatifu. Hivyo kuhani mkuu hangeweza kuwaambia waisraeli kwamba leo ameongea na Mungu wakati shekina haikuonekana. Kutokana na hili tunaona Daudi katika kuomba kwake ili ahakikishe kuwa ameongea na Mungu,alihakikisha ameuona ameuona uwepo wa Mungu, huo ulikuwa uwepo wa shekina.
Wakristo waleo wanaomba bila malengo kama hayo ya Daudi wanaomba bila kuhakikisha kuwa Shekina imejidhihirisha,Mungu hujidhihirisha. Ni sawa na kuhani mkuu alipokuwa anaongea na Mungu, alipokaa kwenye kiti cha rehema Mungu ili kuonyesha kuwa yuko pale alikuwa anajidhihirisha kwa wingu (Shakina Glory) Daudi naye alikuwa anaomba hadi akutane na Mungu. Mungu alikutana na Daudi alikuwa akijidhihirisha kwa nguvu nguvu na utukufu wake hivyo Daudi alipokuwa akimtafuta Mungu,alikuwa akijidhihirisha kwa nguvu na utukufu wake. Wakristo wa leo wanaomba bila malengo hayo. Wao wanaomba kwa kubahatisha bila kujua kuwa je Mungu amekutana nao? Wanafikiri kila kuomba kutawakutanisha na Mungu. Hii imesababisha wakristo hawapati majibu japokuwa wanaomba. Kuhani mkuu alipokaa kwenye kiti cha rehema patakatifu pa patakatifu utukufu wa Mungu ulijidhihirisha kuonyesha kuwa Mungu yupo. Bila ya utukufu kuonekana hiyo ilikuwa na maana kuwa kuhani Mkuu hajakutana na Mungu.
Safari ya kuhani mkuu kwenda kwenye maombi kutoka nymbani kwake  ilikuwa ni ya miguu. Mkristo wa leo wewe ukiwa ni kuhani safari yako ya kuingia hekaluni ni ya imani wewe ni kuhani wewe ni hekalu,unaingia hekaluni kwa njia ya maombi. Unapoanza kuomba hiyo ndio safari ya kuingia hekaluni. Kuhani akitokea nyumbani kwake alikuwa anapitia sehemu kuu tatu.
1.     Sehemu ya kwanza ni kutoka nyumba kwake hadi ua wa nje sehemu pili ni patakatifu. Na sehemu ya tatu ni patakatifu pa patakatifu. Katika sehemu ile ya kwanza yaani kutoka nyumbani kwake hadi ua wan je,kuhani alitoka nyumbani kwake alikuwa anakutana na watu na mambo mbalimbali yaliyokuwa yanamzunguka kama vile, watoto wakicheza michezo mbalimbali watu wakifanya biashara n.k. hadi kuhani alipoingia katika ua wan je bado alikuwa anakutana na watu mbalimbali ambao wamekwenda hekaluni kupata huduma mbalimbali za kimungu kutoka kwa makuhani hekaluni. Kuhani alipoingia patakatifu hakuendelea kuona hayo mambo tena. Ukiwa patakatifu huwezi kuona mambo yaliyo nje ya patakatifu,bali utaona shughuli za kimungu ambazo makuhani wadogo huzifanya mahali patakatifu. Pia huwezi kuona mtu yeyote patakatifu isipokuwa makuhani peke yake. mtu wa Mungu unapoanza kuomba,katika hatua yako ya kwanza kabisa ya kuomba,huwa ni sehemu ngumu sana kwa kuomba. Mwambaji hujisikia au huhisi kama anapanda mlima mrefu. Kuongea maongezi ambayo si kuomba unaweza hata saa kumi bila ugumu wowote. Maongezi ya kawaida huwa hayana upinzani wa shetani,maombi huwa yana upinzani kutoka kwa shetani ndio maana huwa kunakuwa na ugumu mfano wa kujisikia kama unapanda mlima. Sehemu hiyo ya kwanza kabisa katika maombi ni sawa na sehemu ya kwanza ya kuhani wa agano la kale alipotoka nyumbani kwake hadi kwenye ua wan je wa hema. Kuhani alikuwa anakutana na mambo mbalimbali yaliyokuwa yanamzunguka. Mkristo unapoanza maombi japokuwa utakuwa umefumba macho,pamoja na kuwa umefumba macho,kuna vitu ambavyo huwa vinaendelea kuonekana katika fahamu zako. Vitu hivyo huwa ni vitu ambavyo viko karibu sana katika maisha ya muhusika vitu vinavyotuzunguka,kama vile watoto,mume,mke,mali,elimu,kazi.n.k kuhani aliviona vitu vinavyomzunguka wakati akienda hekaluni kwenye sehemu ya kwanza. Yaani kutoka nyumbani hadi ua wan je,aiona watu mbalimbali aliokuwa akikutana nao njiani,pengine aliona watu wakicheza, n.k. hivi ni vitu ilikuwa ni lazima avione maana vilikuwa njiani,vilikuwa vimemzunguka. Ni hivyohivyo hata wewe  unapoingia kwenye maombi. Sehemu ya kwanza ya hekalu lako ni mwili hivyo ni lazima uvione vitu  vya kimwili vinavyokuzunguka. Pamoja na kuviona vitu mbalimbali pia unaweza kuona dhambi fulanifulani. Dhambi unazoziona mara nyingi huwa ni dhambi ambazo zinakuotea kukushambulia. Pengine unaweza kuiona dhambi ambayo uliitenda zamani na ulishaitubu na ilishasamehewa,lakini shetani anaweza kuileta ili akuchanganye. Wakristo wengi wanapoona hivyo hukatisha maombi yao na kuanza kukemea ili vitu kama hivyo visiendelee kuonekana. Lakini nakwambia hivi hata ukemee hiyo hali isiendelee kuonekana hiyo hali haiwezi kuondoka kwa kukemewa,bali itaendelea kuonekana maana ni vitu ambavyo vimekuzunguka ni lazima uvione kwa sababu uko mwilini.
2.     Sehemu ya kwanza ya wewe kuingia ni mwilini. Hivyo kipindi chote utakachokuwa mwilini ni lazima uendelee kuviona vitu hivi,hivyo usipambane navyo kwa kuvikemea kwa sababu ni lazima vionekane. Hivyo usipambane navyo kwa kuvikemea kwa sababu ni lazima vionekane. Hivyo wewe utakapoona vitu hivyo vinakuja kwenye fahamu zako wakati ukianza maombi wewe endelea na maombi yako vitu hivyo vinavyoonekana kwenye fahamu zako wakati wa mwanzo mwanzo wa maombi ndivyo husababisha ugumu na uzito katika maombi. Vitu hivi huitwa miungu. Kitu chochote ambacho ukikiweka  kiwe cha kwanza,Mungu ukamuweka awe wa pili basi kitu hicho kinakuwa miungu. Vitu hivi vinaweza kuwa ni baadhi ya Baraka mbalimbali ambazo ametupa Mungu,sasa wewe unapoviweka vya kwanza halafu Mungu anakuwa wa pili,basi kitu hicho kinakuwa miungu kwako. Vitu viile mume,mke,wazazi,watoto,rafiki,kazi,elimu,mali,dini tabia mbaya,ubinafsi,n.k. vitu hivi shetani huvitumia kuvuruga uhusiano wetuna Mungu kwa kuvifanya vichukue nafasi ya kwanza na Mungu awe nafasi ya pili. Hivyo unapokuwa unaomba vinapoonekana mbele yako kwenye fahamu zako japokuwa umefumba macho hiyo ina maana kwamba vinakuzuwia usiongee na Mungu,vinakuzuwia usimfikie Mungu katika maombi yako.
3.     Mungu huanza kuwashughulikia hao miungu kwa kuwatoa wasikae mbele katika fahamu zako hivyo unapokuwa unaona kitu fulani mbele yako wakati ukianza kuomba,basi ujue kuwa Mungu anakuonyesha miungu anaoushughulikia kwa wakati huo. Wewe unatakiwa uendelee kuomba tu. Usijishughulishe kwa lolote kuhusu miungu hiyo,wala usisimamishe maombi na kuanza kuikemea.kushughulikiwa kwa hiyo miungu tunaweza kusema kuwa ni kuiangusha chini ili itoke kwenye nafasi ya kwanza na kumpisha Mungu achukue nafasi ya kwanza. Fahamu kwamba miungu hiyo ndiyo inayokuzuwia kumuona Mungu,inakuzuwia kuwasiliana na Mungu,hadi miungu hiyo itoke ndipo utaweza kumfikia Mungu katika maombi,kushghulikiwa kwa miungu ni kuuawa kwa hiyo miungu. Mungu anaiua hiyo miungu,bila miungu kufa huwezi kupata mpenyo katika maombi yako.huwezi kumfikia Mungu wala huwezi kuwasiliana na Mungu.miungu ni kikwazo katika mawasiliano na,kama ingekuwa zamani tungeweza kusema kwamba miungu ndio kutu katika nyaya za simu ya mbinguni kuna miungu ya aina nyingi mingine unaweza usiione katika maombi,lakini inaonekana katika macho ya mwili ikijidhihirisha katika matendo ya wakristo. Baadhi ya miungu hiyo ni tabia zisizo za kiutu,mila mbovu,mapokeo ya kipagani,ukabila,hasila,wivu,chuki n.k. wakristo waliookoka wamengagania vitu hivi kama hawatamruhusu Mungu akaiua hii miungu,hawatakwenda mbinguni. Kuwa na miungu hii ni kuiabudu na yeyote anayeabudu miungu hawezi kumona Mungu. Wakristo wengi wameweka kazi,biashara,elimu,watoto,mke,mume,n.k. view vya kwanza Mungu wamemuweka awe wa pili.huo ni kuvifanya vitu hivyo viwe   

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni