Jumamosi, 4 Agosti 2012



 NYOTA WA MUZIKI WA INJILI AFRIKA YA KUSINI VUYO MOKOENA HATUNAYE TENA.
Marehemu Vuyo Mokoena kushoto akiwa na mke wake Tebogo katika siku ya mwisho ya uhai wake.
Kwa wapenzi wa muziki wa injili wa Afrika kusini jina la Vuyo Mokoena sio jina geni kabisa na unaweza usitofautishe na majina kama Rebeka Malope,Sipho Mukabane na akina Jabu              Afrika ya kusini ni nchi ambayo imebarikiwa sana katika suala zima la muziki pamoja na mambo mengine,taifa hili pia limepoteza waimbaji wengi wakiwemo wa muziki wa nje ya kanisa na ule wa kanisani na moja ya nyota iliyozimika katika muziki wa injili nchini humo ni Vuyo Mokoena ambaye alijulikana rasmi kwenye tasnia ya muziki nchini humo mnamo mwaka 1999 wakati aliposhiriki mashindano ya kuibua vipaji kisha akawa ni mtu wa kuitikia nyimbo na waimbaji(backup) katika kundi la Pure Magic kabla hajatoka rasmi kivyake mwaka 2003 kama mwimbaji wa kujitegemea.

Marehemu Vuyo wakati wa uhai wake.


Vuyo ambaye hakuchukua muda mrefu kwenye medani ya muziki kujulikana ameshiriki kikamilifu katika kundi la Joyous Celebration kwa takribani miaka saba na rafiki yake Jabu Hlongwane katika nyimbo mbalimbali,pia alikuwa rafiki wa karibu sana na malkia wa muziki wa injili barani Afrika Rebecca Malope ambaye kutokana na ukaribu walionao marehemu alimkabidhi mkewe aitwaye Tebogo wimbo ambao aliutunga yeye siku nne kabla hajafariki dunia na kumtaka mkewe kuukabidhi wimbo huo kwa Rebecca endapo jambo lolote litatokea(ikiwa kama atafariki) ili aje kumwimbia siku ya mazishi yake, jambo ambalo Rebecca alilifanya.




Mwimbaji huyo maarufu kwa wimbo wake ''Njalo'' ameacha mke na watoto wanne alifariki dunia mwaka 2008  kwa ugonjwa wa kansa ya damu,ugonjwa ambao ulimlaza kitandani mara nyingi kabla ya kifo chake,taarifa ya kifo hicho ilitolewa na kampuni yake ya muziki iitwayo Big Fish Music,ambapo katika mazishi yake waimbaji wengi walihudhuria wakiwemo kundi la Joyous,Rebecca Malope,rafiki yake Sipho Makhabane na waimbaji wengine wengi.Mwimbaji huyo kabla ya kufariki dunia tayari alishanyakua tuzo katika medani ya muziki wa injili nchini humo.
Baadhi ya waimbaji wa kundi la Joyous wakiimba kwenye jukwaa

Ibada ya mazishi ya mwimbaji huyo ilifanyika sehemu mbili katika kanisa la Grace Bible Church na  Duduza Multipurpose Centre na mazishi kufanyika katika makaburi ya Nigel huko huko Afrika ya kusini.Lakini pia kitendo cha kuhuzunisha kilichotokea katika ibada ya mazishi kanisa la Grace Bible ni kwamba licha ya ulinzi mkali wezi wapatao wawili waliiba gari aina ya Rav4 ya mwanamuziki mwingine maarufu nchini humo aitwaye Khanyo Maphumulo ambaye alikuwa akihudhuria ibada ya mazishi kanisani hapo


Moja ya jambo lililofanywa na rafiki zake wa karibu pastor Jabu,Lindelani pamoja na Rebecca Malope walishirikishwa kwenye makala maalumu ya maisha ya mwanamuziki huyo ambaye mpaka hii leo bado anakumbukwa nchini kwake na sehemu mbalimbali duniani kutokana na huduma yake njema aliyoifanya ya kumuinua Kristo duniani.Rebeka malope mwanamuziki mkongwe wa

                                                                                         nyimbo za injili Afrika Kusini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni