Jumatano, 4 Mei 2016

VITA VYA KIROHO : SEHEMU YA KWANZA



 

Biblia inasema.

10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

11 Vaeni silaha zote za Mungu,mpate kuweza kuzipinga hila za shetani

12 kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu,mpate kuweza kushindana siku ya uovu,na mkiisha kuyatimia yote kusimama.

14 Basi simameni hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa darii ya haki kifuani,

15 nakufungiwa miguu utayari wa injili ya amani.

16 Zaidi ya yote mkitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya Yule mwovu

17 tena ipokeeni chepeo ya wokovu, na upanga wa roho ambao ni neno la Mungu

18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika roho.  

Ili tuwe kulewa vizuri na kwa urahisi somo hili ni muhimu kuanza na mistari hii ya Biblia ili kujenga msingi wa somo hili.

Tunasoma hapa mtume Paulo anawaelezea Waefeso aina ya vita tunayopigana na namna ambavyo tunatakiwa kupigana kwa mbinu, maana vita si lelemama kwa hiyo ili tuweze kushinda tunahitaji kujifunza mbinu za kivita. Maisha ya wokovu sio maisha mepesi kama tunavyoaminishwa na baadhi ya wainjilisti kwamba kwa Yesu ni tambarare, hiyo sio kweli ukishaambiwa kuna vita na unatakiwa kupigana basi ni lazima ujue kwamba wewe sio raia bali ni askari. Na kwa kawaida askari ni raia aliyepewa mafunzo maalumu ya kupigana vita kwa kutumia zana mbalimbali za kivita. Ndio maana inakuwa muhimu sana kujifunza aina ya vita na mbinu ambazo zitatusaidia kupata ushindi. katika mstari wa 12 Mtume Paulo anasema  

12 kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Katika mstari huu Biblia inatujulisha kuhusu aina ya vita tunayopigana, tunapigana na nani, lakini pia ametufahamisha kuhusu aina mbili za ulimwengu, kwamba kumbe kuna ulimwengu wa damu na nyama ambao ndio dunia hii ambayo sisi tunayoishi.

Lakini pia kuna ulimwengu wa roho ambao sisi kwa macho na kwa akili za kawaida hatuwezi kuuona wala viumbe vinavyokaa katika ulimwengu huo hatuwezi kuviona katika macho ya kawaida, ulimwengu huo ndio ambao nataka tuuangalie kwa undani.

Inawezekana tukawa tunajua mambo machache kuhusu ulimwengu wa roho, lakini kwa uchache ulimwengu wa roho ndio ulimwengu halisi na dunia ni kivuli cha ulimwengu wa roho, ulimwengu huo ulikuwepo kabla ya dunia kuwepo na Mungu wakati anaiumba hii dunia alikuwa anaiumba akiwa katika ulimwengu wa roho.

Kwa kifupi ni kwamba ulimwengu wa roho ndio wenye nguvu kubwa sana kiasi cha kwamba dunia yetu pamoja na uzito wake wa mabilioni ya tani imeshikwa na nguvu kidogo sana kutoka katika ulimwengu wa roho, na inajizungusha yenyewe kwa masaa ishirini na nne kupata usiku na mchana. Lakini pia inalizunguka jua kwa siku 365 au 366 ili kupata mwaka bila kupoteza majira na mwelekeo wake. Watu wanaosoma elimu ya unajimu wanajua kwamba nguvu iliyoko katika ulimwengu wa roho inatawala maisha ya wanadamu walioko katika dunia hii tunayoishi.

Tangu zamani, wanadamu wamechunguza miendo hususa ya nyota na sayari katika mbingu za usiku na pia mahali tofauti-tofauti ambapo nyota na sayari hizo zinakuwa kulingana na majira.

Mungu akasema, na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndio dalili na majira na siku na miaka;        (Mwanzo 1:14)

Hata hivyo, iwe tunajua au hatujui, mienendo ya nyota na sayari ina uvutano wa moja kwa moja katika maisha yetu. Dunia huzunguka jua ambalo ni nyota inayotusaidia kujua urefu wa siku na mwaka. Mwezi ni “kwa ajili ya nyakati zilizowekwa,” au ‘kutupimia majira.

Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, jua latambua kuchwa kwake (Zaburi 104:19;

Nazo nyota ni mwongozo unaotegemeka katika usafiri, na hata wanaanga wanaweza kutumia nyota wanapoongoza vyombo vyao vya angani. Kwa hiyo, wengi wangependa kujua kama nyota zinaweza kufanya mengi zaidi ya kutuonyesha wakati na majira, na kutusaidia tuthamini kazi za uumbaji za Mungu. 

Je, nyota zinaweza kutusaidia kujua wakati ujao au kutuonya kuhusu majanga na misiba? Najaribu kukuchambulia nguvu ambayo iko katika ulimwengu wa roho.

Unajimu, ambao ni mazoea ya kutazama mbingu ili kutafuta ishara za kuongoza maisha yetu duniani, ulianzia Mesopotamia ya kale, yaelekea katika miaka ya 2000 K.W.K. Wanajimu wa kale walitazama mbingu kwa makini.

Elimu ya nyota ilianzishwa na juhudi zao za kuchora miendo ya nyota na sayari, kujua mahali kila nyota ilipo, kutengeneza kalenda na kutabiri kupatwa kwa jua au mwezi. Lakini wanajimu hawachunguzi tu uvutano wa mwezi na jua katika mazingira yetu. Wanajimu wanadai kwamba mpangilio wa jua, mwezi, sayari, nyota, na makundi ya nyota, una uvutano juu ya matukio makuu duniani na pia juu ya maisha ya kila mtu.

Wanajimu fulani wanatazama nyota na sayari ili wajue mambo au hatari za wakati ujao. Na watu wanaouelewa wanaweza kuutumia ujuzi huo na kunufaika nao kwa njia mbalimbali. Wengine wanahisi kuwa unajimu unaonyesha kile ambacho kimeamuliwa mapema tufanye. 

Sasa kwa sababu hiyo mtume Paulo anatuonya kwamba tusijaribu kushindana katika mwili maana kwa kufanya hivyo tunakuwa tumechelewa, kwa sababu mambo yote yanakuwa tayari yameshaamriwa katika ulimwengu wa roho na ni mpaka ujue namna ya kuingia katika ulimwengu wa roho na kupata habari hapo ndio unaweza kushindana. 

ninayo mambo mengi sana ya kushuhudia jinsi mambo ambayo niliyaona mapema katika ulimwengu wa roho yalikuja kutimia baada ya majuma au miezi kadhaa.

Watu wasiomjua Mungu unajimu unaweza kuwasaidia kujua wakati unaofaa wa kushiriki katika utendaji fulani au kuanza kufanya mambo fulani. 

Inasemekana kwamba habari hizi zinaweza kujulikana kwa kutazama mpangilio wa nyota au sayari fulani na kuchunguza uhusiano kati ya nyota na sayari hizo na pia uhusiano wake na dunia. 

Inasemekana kuwa uvutano wa nyota na sayari juu ya maisha ya mtu binafsi unategemea mpangilio wake wakati wa kuzaliwa kwa mtu huyo.

Wanajimu wa kale walifikiri kuwa dunia ndiyo kitovu cha ulimwengu, na kwamba sayari na nyota zilikuwa zimefungiwa katika miviringo ya kimbingu ambayo iliizunguka dunia. 

Pia walifikiri kwamba jua linasafiri angani kati ya makundi ya nyota likifuata njia fulani hususa katika mzunguko wa kila mwaka.

Waliigawanya njia hii ya jua ya kila mwaka katika sehemu au maeneo 12. Sehemu hizo zote zilikuwa na makundi ya nyota, na kila sehemu ilipewa jina kulingana na kundi la nyota ambamo jua lilipitia.

Sehemu hizo zikawa zile ishara 12 za nyota na kuitwa “nyumba za mbinguni,” kwa sababu zilionwa kuwa makao ya miungu. Hata hivyo, wanasayansi waligundua baadaye kuwa jua haliizunguki dunia bali dunia ndiyo inayozunguka jua. Uvumbuzi huo ulithibitisha kuwa unajimu si sayansi yenye kutegemeka.

Kutoka Mesopotamia ulikoanzia, unajimu ulienea hadi karibu sehemu zote za dunia na ukatumiwa kwa njia moja au nyingine katika maeneo yote yenye ustaarabu mkubwa duniani. Baada ya Uajemi kushinda Babiloni, unajimu ulienea hadi Misri, Ugiriki, na India. 

Kutoka India, wamishonari Wabudha waliueneza hadi Asia ya Kati, China, Tibet, Japani, na Asia ya Kusini-Mashariki. Yaonekana kuwa unajimu uliopo leo ulianzishwa huko Misri wakati wa utawala wa Ugiriki, na umeathiri sana maoni ya Wayahudi, Waislamu, na watu wa dini zinazojidai kuwa za Kikristo. 

Bado hata sasa  katika nchi nyingi watu hawatoki majumbani kwao bila kujua nyota yake inasemaje kuhusu siku hiyo, kwa hiyo ni lazima wapate magazeti yenye kurasa maalumu za watabiri wa nyota.

Wakati wa utawala wa Mfalme Nebukadneza wa Babiloni, makuhani na wanajimu walishindwa kufasiri ndoto ya mfalme. Danieli, nabii wa Mungu wa kweli, alionyesha sababu zilizofanya washindwe kufasiri ndoto hiyo aliposema:

“Siri ambayo mfalme anauliza, watu wenye hekima, wala wafanya-mazingaombwe, wala makuhani wenye kufanya uchawi wala wanajimu hawawezi kumwonyesha mfalme. Hata hivyo, kuna Mungu mbinguni ambaye Ni Mfunuaji WA siri, naye amemjulisha Mfalme Nebukadneza mambo yatakayotokea katika siku za mwisho.” 

(Danieli 2:27, 28)

Danieli alimtumaini Mungu ambaye ni “Mfunuaji wa siri”— bali si jua, mwezi, au nyota—na akamweleza mfalme maana ya kweli ya ndoto yake.—Danieli 2:36-45

Kwa maana nyingine ni kwamba Mamlaka ya Mungu katika ulimwengu wa roho ilikwisha amua juu ya hatma ya ufalme wa Nebukadneza, kwa hiyo Nebukadneza hata angejitahidi kupambana wakati anguko lake linatokea angekuwa anapigana katika damu na nyama. 

ndipo mtume Paulo anakataa kwamba hatutakiwi kupigana katika damu na nyama. Ni sawa na kwamba tumesha chelewa.

Neno la Mungu linafunua wazi kwamba ‘matendo yenye nguvu na ishara za uwongo na mambo ya ajabu,’ ni “utendaji wa Shetani.”—2 Wathesalonike 2:9.

Kama vile ambavyo kuvuta bangi kunaweza kumfanya mtu awe mtumwa wa walanguzi wa dawa za kulevya, kujihusisha na unajimu kunaweza kumfanya mtu atawaliwe na yule mdanganyifu mkuu, Shetani. 

Hivyo basi, wale wanaompenda Mungu na kweli, wanapaswa kuukataa kabisa unajimu na badala yake kutii shauri hili la Biblia: “Chukieni yaliyo mabaya, pendeni yaliyo mema.”—Amosi 5:15.

Unajimu umeenea sana kwa sababu watu wanatamani kujua mambo ya wakati ujao. Je, inawezekana kujua mambo hayo? Ikiwa ndivyo, tunaweza kuyajua jinsi gani? Biblia inasema kwamba hatuwezi kujua ni nini ambacho kitampata kila mmoja wetu kesho, mwezi ujao, au mwaka ujao. (Yakobo 4:14)

Hata hivyo, Biblia inatufunulia mambo ambayo yatawapata wanadamu kwa ujumla wakati ujao. Inatuambia kwamba karibuni, Ufalme utakuja, kama tunavyoomba katika Sala ya Bwana.

Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu nao utasimama milele na milele 

(Danieli 2:44);  

Basi ninyi salini hivi: Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe,ufalme wako uje,mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni. 

Mathayo 6:9, 10)

 Pia inatuambia kwamba kuteseka kwa binadamu kutaisha hivi karibuni na hatutasumbuka tena.

 Maana tazama, mimi naumba mbingu mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. (Isaya 65:17;

tutaendelea 0713 461593

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni