Hebu tufikiri kuhusu watu wawili. Mmoja ana ndoa, ni mtu wa
dini, anayedai kumpenda Mungu kwa moyo wake wote, ambaye ameanza kumtamani
mwanamke kijana anayekaa jirani. Muda si muda anamwacha mkewe na haraka anamwoa
yule msichana aliyemvutia.
Yule mwingine si mtu wa dini. Yeye hajawahi kusikia hata
Injili, na anaishi maisha mabaya ambayo hatimaye yanaharibu ndoa yake.
Miaka kadhaa baadaye, akiwa peke yake tu, anaisikia Injili,
anatubu, na anaanza kumfuata Yesu kwa moyo wake wote. Miaka mitatu baadaye
anampenda mwanamke mwenye kumpenda Mungu sana anayekutana naye kanisani. Wote
wawili wanatafuta mapenzi ya Mungu na ushauri wa wengine kwa bidii, kisha
wanapanga kuoana. Wanakuja kuonana, na wanakuwa waaminifu kwa Bwana na wao kwa
wao mpaka kifo.
Mr & Mrs Mziray |
Sasa – hebu tudhanie kwamba wote wawili wametenda
dhambi kwa kuoa tena. Katika hao wawili, ni yupi mwenye dhambi kubwa zaidi?
Bila shaka ni yule wa kwanza. Yeye ni sawa na mzinzi tu.
Lakini – vipi kuhusu yule mtu wa pili? Je, ni kwamba
ametenda dhambi? Je, tunaweza kusema kwamba yeye hana tofauti na mzinzi
– kama yule wa kwanza? Hapana. Je, tumwambie yale ambayo Yesu alisema kuhusu
watu wanaoachana na kuoa tena, na kumjulisha kwamba sasa anaishi na mwanamke
ambaye Mungu hakumwunganisha naye kwa sababu anamhesabu bado ana ndoa na mke
wake wa kwanza? Je, tumwambie kwamba anaishi katika zinaa?
Majibu yako dhahiri kabisa. Uzinzi hutendwa na watu ambao
wameoana, wanaomwona mwingine asiyekuwa mwenzi wao. Kwa hiyo, kuachana na
mwenzako kwa sababu umepata mrembo zaidi ni sawa na uzinzi. Lakini, mtu ambaye
hajaoa hawezi kufanya uzinzi kwa sababu hana mwenzi wa kumkosea
uaminifu, na mtu ambaye ameachika hawezi pia kutenda uzinzi kwa sababu hana
mwenzi wa kumkosea uaminifu. Tukielewa mantiki ya kihistoria na kiBiblia kuhusu
maneno ya Yesu, hatuwezi kufikia maamuzi yatakayopotosha watu, na yenye
kupingana na Maandiko yote.
Wanafunzi waliposikia itikio la Yesu kwa jibu la Mafarisayo,
walijibu hivi, “Kama mahusiano ya mwanamume na mke wake yako hivyo, ni afadhali
kutokuoa” (Mathayo 19:10). Tambua kwamba walikuwa wamekulia chini ya mafundisho
na ushawishi wa Mafarisayo, na katika utamaduni uliokuwa umeathiriwa sana na
Mafarisayo. Hawakuwahi kudhani kwamba ndoa ni kitu cha kudumu kiasi hicho.
Ukweli ni kwamba, muda mfupi uliopita, hata wao waliamini ni halali kwa
mwanamume kumwacha mkewe kwa sababu yoyote. Basi kwa haraka wakaamua kwamba
ingekuwa bora kuepukana na ndoa kabisa, ili kuepuka hatari ya kuachana na
kuingia kwenye uzinzi. Yesu alijibu hivi:
Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena
wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi
waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea
neno hili, na alipokee (Mathayo 19:11-12).
Yaani – kinachoamua ni ile hamu ya kushirikiana kimwili
aliyo nayo mtu, au uwezo wake wa kuitawala. Hata Paulo alisema hivi: “NI
afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa” (1Wakor. 7:9). Wale waliozaliwa wakiwa
matowashi au wale wanaofanywa matowashi na watu (kama ilivyokuwa zamani: watu
waliwafanya wanaume wengine kuwa matowashi, ili wawape jukumu la kuwalinda wake
zao) hawana hamu ya kushirikiana na mwanamke kimwili. Wale “wanaojifanya
wenyewe kwa ajili ya ufalme wa mbinguni” ni wale ambao wamejaliwa na Mungu
kipekee kuwa na uwezo wa kujitawala zaidi. Ndiyo maana “si wote wawezao
kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa” (Mathayo 19:11).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni