Mwl Furaha Amon
Ndoa Katika Torati Ya Musa
Unaposoma Biblia kwa uangalifu, huwezi kuona habari za watu
kupeana talaka na kuoa tena baada ya talaka, mpaka unapofikia kitabu cha tatu
cha Biblia kinachoitwa Mambo ya Walawi. Katika Torati ya Musa kulikuwa na agizo
la kuwakataza makuhani kuona wanawake walioachwa.
Wasimwoe
mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke
aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake (Walawi
21:7).
Hapo bila ya kupepesa tunaweza kusema wazi kwamba agizo hili
linawahusu zaidi watu wenye huduma zinazotambulika na kanisa. Na hii ni kwa
sababu hakuna popote katika Torati ya Musa penye katazo la namna hiyo kwa watu
wengine wa Israeli ambao sio watumishi kwa ujumla. Tena, andiko hilo linabeba mambo
yafuatayo:
(1)
Walikuwepo wanawake waliokuwa wameachika
katika Israeli, na
(2)
Kusingekuwepo kosa lolote kwa
wanaume Waisraeli ambao si makuhani kuoa wanawake waliokuwa wameachika.
Sheria inayotajwa katika mstari huo inawahusu makuhani tu na
wanawake walioachika, wanaotaka kuolewa na makuhani. Hapakuwa na ubaya wowote
katika Torati ya Musa kwa mwanamke yeyote aliyeachika kuolewa tena, mradi tu
hakuolewa na kuhani.
Na hakukuwa na kosa lolote kwa mwanamume, kuoa mwanamke
aliyeachika, mradi si kuhani.
Kuhani mkuu (pengine kwa sababu ni mfano wa Kristo)
alitakiwa kuishi kwa viwango vya juu zaidi kuliko hata makuhani wa kawaida.
Yeye hakuruhusiwa hata kuoa mjane. Mistari kadhaa baadaye tunasoma hivi
katika Walawi:
Asitwae mjane,
wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba;
lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe (Walawi 21:14).
Je, andiko hili linathibitisha kwamba ilikuwa dhambi kwa
wajane wote wa Israeli kuolewa tena, au kwamba ilikuwa dhambi kwa
wanaume wote wa Israeli kuoa wajane? Hapana! Mstari huu unasema – tena
kwa nguvu sana – kwamba isingekuwa dhambi kwa mjane yeyote kuolewa na
mwanamume yeyote, mradi si kuhani mkuu. Tena unasema mwanamume mwingine
yeyote alikuwa huru kuoa mjane, mradi si kuhani mkuu. Maandiko mengine
yanathibitisha uhalali wa wajane kuolewa tena (ona Warumi
“Kwa maana mwanamke aliye na
mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule
mume amefunguliwa ile sheria ya Mume” Warumi 7:2-3;
“Basi napenda
wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto wawe na madaraka ya nyumbani; ili
wasimpe adui nafasi ya kulaumu.” 1Timo. 5:14).
Mstari huo vile vile unaonyesha kwamba kusingekuwa na kosa
lolote kwa mwanamume yeyote Mwisraeli kuoa mwanamke aliyeachika, au hata
mwanamke ambaye hakuwa bikira – “aliyenajisika katika ukahaba” – mradi si
kuhani au kuhani mkuu.
Hoja hiyo inaungwa mkono na Walawi 21:7 pia “Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo
aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyechwa na mumewe; kwa kuwa yeye
kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake.”. Tena, unasema kwamba katika Torati ya
Musa, hapakuwa na kosa lolote kwa mwanamke aliyeachika kuolewa tena, au
mwanamke “aliyenajisika katika ukahaba” kuolewa, mradi tu asiolewe na kuhani.
Kwa neema sana, Mungu aliwapa wazinzi na walioachika nafasi nyingine, japo
alikuwa kinyume kabisa na uzinzi na talaka.
MWISHO
WA SEHEMU YA TANO
Tukutane
katika sehemu ya sita ya somo hili; kwa msaada zaidi tunaweza kuwasiliana 0677
609056
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni