Mwl Furaha Amon
Hebu kwa muhtasari tuone yale ambayo tumejifunza mpaka hapa.
Hata ingawa Mungu alitangaza kwamba anachukia talaka, hakuonyesha kabla au
wakati wa agano la kale kwamba kuoa na kuolewa tena ni dhambi, isipokuwa katika
haya mawili yafuatayo: (1) mwanamke aliyeachika mara mbili – au aliyeachika
mara moja na kufiwa na mume wa pili – kuolewa na mumewe wa kwanza, na (2)
mwanamke aliyeachika kuolewa na kuhani. Tena, Mungu hakuonyesha kwamba kumwoa
aliyeachika ni dhambi kwa yeyote, isipokuwa makuhani.
Hayo yanaonekana kupingana na yale Yesu aliyosema juu ya
watu walioachika wanao-oa tena, na wale wenye kuoa walioachika. Yesu alisema
watu kama hao wanazini (ona
“ Lakini
mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya
kuwa mzinzi ; na mtu akimwoa yule
aliyeachwa, azini.”Mathayo 5:32).
Basi, yaonekana tumemwelewa vibaya Yesu au Musa, au pengine
Mungu alibadilisha sheria Yake. Mimi nadhani tunaweza kuwa tunatafsiri vibaya
yale aliyofundisha Yesu, kwa sababu ni ajabu kwa Mungu kutangaza ghafula kitu
kuwa dhambi kiadili, kilichokuwa kinakubalika kwa miaka elfu na mia tano katika
Torati ambayo Yeye aliitoa kwa Israeli.
Kabla ya kukabiliana na hili kwa upana zaidi, hebu pia tuone
kwamba ruhusa ya Mungu kwa watu kuoa tena katika agano la kale haikuwa na
masharti yoyote yaliyotokanana sababu za talaka ya mtu, au kiwango cha hatia
ambacho mtu alipata kwa sababu ya talaka husika. Mungu hakusema kwamba watu
fulani walioachika hawaruhusiwi kuoa au kuolewa kwa sababu talaka yao haikuwa
halali. Hakusema kwamba kuna watu fulani wanaoruhusiwa kuona kwa sababu ya
uhalali wa talaka zao. Lakini mara nyingi wachungaji wa siku hizi wanajaribu
kufanya maamuzi hivyo, kutokana na ushuhuda wa mtu mmoja. Kwa mfano: Mwanamke
aliyeachika anajaribu kumshawishi mchungaji wake kwamba anastahili kuruhusiwa
kuolewa kwa sababu yeye ni mwathirika wa talaka. Mume wake wa kwanza ndiye
alimwacha – si yeye. Lakini, kama huyo mchungaji atapewa nafasi ya kusikiliza
upande wa mume naye, anaweza kumhurumia kwa namna fulani. Pengine huyo mama
alikuwa mkorofi na anastahili lawama kiasi fulani.
Tunaweza kuwadanganya watu, lakini hatuwezi kumdanganya
Mungu. Kwa mfano: Mungu anamwonaje mwanamke ambaye anamnyima mumewe huduma za
kitandani kila wakati, kisha anamwacha kwa sababu amekosa uaminifu kwake? Je,
hahusiki na hiyo talaka kwa sehemu?
Lile jambo la mwanamke aliyeachika mara mbili katika
Kumbukumbu 24 halisemi chochote kwamba talaka zake zote mbili ni halali. Mume
wake wa kwanza aliona “neno ovu” kwake. Kama hilo “neno ovu” ni uasherati,
angestahili kufa kulingana na Torati ya Musa (Walawi 20:10). Basi, kama
uasherati tu ndiyo sababu halali ya talaka, pengine mume wake wa kwanza hakuwa
na sababu nzuri ya kumwacha. Kwa upande wa pili, pengine alikuwa amezini, naye,
akiwa mtu mwenye haki kama Yusufu wa Mariamu, “aliazimu kumwacha kwa siri”
(Mathayo 1:19). Hapo kuna mengi yanayowezekana.
Mume wa pili anasemekana “akimchukia”. Hapa tena, hatujui wa
kulaumiwa ni nani, au hata kama wote wanastahili kulaumiwa. Lakini bado haiweki
tofauti. Neema ya Mungu ilitolewa kwake kwamba aolewe na yeyote ambaye
angekubali kujaribu bahati yake kwa mwanamke aliyeachika mara mbili, isipokuwa
mume wake wa kwanza.
MWISHO
WA SEHEMU YA SITA
Tutakutana
katika sehemu ya saba ya somo hili Mungu akuinue kwa kufuatilia somo hili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni