Mwl F Amon
Utangulizi;
Neno la Mungu ni mwamba, na
mtu aliyejengwa kwenye mwamba hata kama majaribu makubwa yatakuja atayashinda.
Neno la Mungu ambalo ni mwamba ni Rhema sio logos. Neno la Mungu ambalo linao uwezo
wa kumuimarisha na kumjenga mtu ni Rhema. Rhema ndilo neno ambalo humbadilisha
mtu hii ndilo neno la ufunuo. Biblia inasema;-
“Basi
kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye
akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha mafuriko yakaja, pepo
zikavuma zikaipiga nyumba ile isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya
mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asifanye, atafananishwa na mtu
mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Mvua ikanyesha, mafuriko
yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile ikaanguka, nalo anguko lake likawa
kubwa” (Mathayo 7:24 27)
wakati mtu anasikiliza neno
la Mungu likihubiriwa wakati huohuo ndani yako huwa kuna sauti ya Mungu
inayolifafanua hilo neno linalohubiriwa. Ufafanuzi huu hulenga mahitaji ya
muhusika. Hii hutokea hata wakati unapokuwa unasoma Neno la Mungu. Sauti hii
ndio ambayo huwa inafafanua neno la Mungu ndani ya mtu. Hii ndiyo Rhema huo
ndio ufunuo wa neno la Mungu
”kufafanusha
maneno yake kuwatia nuru, na kumfahamisha mjinga” (Zaburi 119: .)
Wakati unasoma neno au
unasikiliza mahubiri, ingawaje mhubiri atakuwa anahubiri katika somo fulani
jingine, wakati huohuo Mungu anakuwa anazungumza na wewe juu ya jambo jengine
tofauti moyoni mwako.
Mungu hutumia maneno yanayohubiriwa kuzungumza na wewe
kwa kulipua ufunuo mwingine kupitia neno hilo linalohubiriwa. Lile
linalofunuliwa kwako, hilo ndilo Mungu analolitaka kwako. Hilo ndilo neno
linalobadilisha, ndilo linalokujenga na kukuimarisha. Hili ndilo unatakiwa
ujengwe kwake. Hiyo ndio sauti ya Mungu kwako ikisema na wewe moja kwa moja,
hilo ndilo neno unalotakiwa ulizingatie na kulishika. Hilo neno ni Roho, lina
uwezo lina nguvu. Mtu anayelishika hilo neno na kulitenda huyu ndiye
atakayesitawi na kuwa sawa na mbegu iliyopandwa katika udongo. Huyu ndiye
ambaye amejengwa katika mwamba.
biblia haijui shida
zako,wala muhubiri hazijui shida zako. Mungu pekee ndiye anayezijua. Anataka
kukutana nazo,hivyo Mungu anazungumza na wewe wakati neno la Mungu
linahubiriwa. Atazungumza na wewe kwa njia ya ufunuo,mkristo hujengeka kiroho
kupitia ufunuo.ufunuo ni sauti ya Mungu ni neno la Mungu. Ufunuo ni Yesu Kristo
mwenyewe.
wakristo wameshindwa kukua
kiroho na shida zao zimeendelea kuwepo japokuwa wanahudhuria kanisani kila leo.
Ni kwa sababu hawajasikiliza nini Mungu anachosema nao. Bali wamechukua kauli
za viongozi wao wa dini kuwa ndilo neno la Mungu. Wamechukua mahubiri pekee
wakauacha ufunuo unaolipuliwa ndani yao wakati neno linapohubiriwa. neno la
mungu kwako ni ile tafsiri inayotolewa na roho mtakatifu ndani yako. Ni lile
neno la Mungu unalolisikia ndani yako kupitia sauti ya Mungu wakati ukisikiliza
neno linahubiriwa. Sina maana kuwa mahubiri si chochote si lolote, hapana!
Mahubiri ni kibebeo cha neno la Mungu. Ndani ya mahubiri ndiko kuna neno
lenyewe halisi la Mungu. mfano mpunga huwezi kuula ni mpaka ukobolewe kwanza
ili utoke mchele ambao ndio hupikwa na kuliwa. Kwa maana hiyo huwezi kupika
mpunga halafu ule. Hivyo hivyo kuna tofauti kati ya mahubiri na ufunuo.
Mahubiri ni chakula ambacho hakijakobolewa, ufunuo
ni chakula ambacho kipo tayari kwa kuliwa. wakristo wengi wamekuwa sio
waangalifu. baada ya unabii kutolewa na watumishi
wa Mungu kuhusu eneo fulani la maisha yao, wao wameuchukua unabii huo moja kwa
moja kama Mungu amesema nao. Wengi wao baadaye mambo yao hayakwenda kama unabii
ulivyosema, wameathirika kiroho na kukatishwa tamaa kwa hilo.
Baada ya unabii uliotolewa
kuusikia, je, wewe muhusika sauti ya Mungu ndani yako imesemaje? Hata kama
baada ya kusikia kauli za viongozi wa dini au kupitia unabii uliotolewa, wewe
nenda ukateketeleze uliyoyasikia kutoka kwa Mungu kupitia unabii huo au kupita
kauli hizo za viongozi wadini. Pindi majaribu yakija Mungu mwenyewe atapigana
na majaribu hayo, maana ni yeye ndiye aliyekuagiza kufanya.
Mungu ana kawaida ya
kuyapigania aliyoyasema yeye mwenyewe. Hivyo ukiwekeza katika yale uliyoyasikia
kutoka kwa Mungu utakuwa umejenga katika mwamba kwa jinsi hii ni lazima
ufanikiwe.
Kuna wakristo wanaooana kwa
kauli za viongozi wao wa dini, majaribu yanapokuja kwenye ndoa zao huwa
wanashindwa kustahimili. Wengine wanafanya biashara kwa kauli za viongozi wao
wa dini n.k. Majaribu yatakapokuja hawawezi kustahimili. Sikiliza ufunuo
unaolipuliwa ndani yako kupitia hizo kauli, mahubiri na nabii, ufunuo huo ndio
uufanyie kazi.
Majaribu huja ili yakutoe
katika mpango wa Mungu. Kama unafanya au kama uko mahali ambapo si mpango wa
Mungu, majaribu yakija yatakutoa na kukuweza. Kama unachofanya au kama pale
ulipo uliagizwa na Mungu, majarbu yakija hayawezi kukutoa kwenye mpango huo. Maana
huo mpango umejengwakwenye neno la Mungu ambalo ndilo mwamba.
Majaribu yanapokuja,
dhoruba, misukosuko huwachanganya watu kiasi wanaanza kuona kuwa huenda Mungu
hakuongea nao wafanye hilo jambo. Lakini iwapo Mungu alizungumza na wewe hata
kama yakija majaribu mazito ni lazima utashinda, lakini iwapo hukusikia kutoka
kwa Mungu ni lazima utashindwa na majaribu hayo, maana Mungu hatakuwa pamoja na
wewe.
MUNGU WANGU AKUBARIKI SANA
Somo litaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni