Mamlaka Ya Kutumika
Kwa
kuwa Mungu anampa mchungaji mamlaka ya kiroho na kusimamia kanisani mwake, hili
halimpi haki ya kutawala kwa nguvu kundi lake. Yeye si Bwana wao – Bwana wao ni
Yesu. Wao si kundi lake – ni kundi la Mungu.
Lichungeni
kundi la Mungu lililo kwenu na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari
kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala
si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa
lile kundi. Na Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya
utukufu, ile isiyokauka (1Petro 5:2-4).
Kila
mchungaji atatoa hesabu ya huduma yake siku moja, mbele ya kiti cha hukumu cha
Kristo.
Tena,
kwa habari ya fedha, mchungaji/mzee/mwangalizi asifanye kitu peke yake. Kama
kuna fedha zinakusanywa kila mara au mara kwa mara kwa sababu yoyote ile,
wengine katika kusanyiko wawajibike ili kusiwe na kutoaminiana kuhusu matumizi
ya fedha (ona 2Wakor. 8:18-23). Hao wengine wawe kundi lililochaguliwa au
kuteuliwa.
Kulipa Wazee
Maandiko
yanaonyesha wazi kwamba wazee/waangalizi/wachungaji wanapaswa kulipwa, maana ni
watenda kazi wa kudumu wa kanisa. Kwa habari hii, Paulo aliandika kama
ifuatavyo:
Wazee
watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hawa wao wajitaabishao
kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, ‘Usimfunge kinywa ng’ombe
apurapo nafaka.’ Na tena, ‘Mtenda kazi astahili ujira wake.’ (1Timo. 5:17, 18).
Mada
iko wazi kabisa – na Paulo anatumia neno ujira. Maneno yake yasiyokuwa
wazi sana kuhusu wazee watawalao vema wahesabiwe kustahili heshima maradufu
yanaeleweka kirahisi wakati mantiki inapotazamwa. Katika mistari kabla ya hii,
Paulo anaandika waziwazi kuhusu jukumu la kanisa kuwasaidia kifedha wajane ambao
wasingepata msaada kwa njia nyingine, na anaanza kwa maneno yale yale:
“Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli” (ona 1Timo. 5:3-36). Basi, katika
mantiki hii, “kuheshimu” maana yake ni kuwasaidia kifedha. Wazee wanaotawala
vema wahesabiwe kustahili heshima mara mbili, yaani, wapokee mara mbili ya
kiasi ambacho wajane wanapewa, na hata zaidi kama wana watoto wanaowategemea.
Makanisa
jengo katika dunia nzima huwategemeza kifedha wachungaji wao (hata katika
mataifa maskini), lakini inaonekana makanisa mengi yanayokutania nyumbani
duniani kote – hasa nchi za Magharibi – hayafanyi hivyo. Hii ni kwa sababu ya
ukweli kwamba makusudi hasa ya watu wengi katika nchi za Magharibi ya kujiunga
na makanisa ya nyumbani ni uasi moyoni, nao wanatafuta na wamepata Ukristo usio
na masharti mengi. Wanasema walijiunga na kanisa la nyumbani kwa sababu
walitaka kuepukana na kifungo cha kanisa jengo, lakini ukweli ni kwamba
walitaka kuepukana na aina yoyote ya kujitoa kikamilifu kwa Kristo. Wamepata
makanisa yasiyotaka watu wajitolee kifedha, makansia yenye kwenda kinyumke
kabisa na kile ambacho Kristo anatazamia kwa wanafunzi Wake. Hayo, mungu wao ni
fedha, na wanathibitisha hilo kwa kujilundia hazina zao duniani badala ya
mbinguni. Hao si wanafunzi wa kweli wa Kristo (ona Mathayo 6:19-24; Luka
14:33). Kama Ukristo wa mtu hauathiri anachofanya na fedha zake, huyo si
Mkristo kabisa.
Makanisa
yanayokutania nyumbani yenye kudai kwamba ni ya KiBiblia yanapaswa kuwatunza
wachungaji wao kifedha, na kuwasaidia maskini na kusaidia kazi ya utume. Kwa
kutoa na katika mambo yote yakifedha, wanapaswa kuzidi sana makanisa jengo,
maana wao hawana majengo ya kulipia wala watumishi wengi wa kulipa mishahara.
Wanahitajika watu kumi tu ambao watatoa zaka ili kumtunza mchungaji mmoja. Watu
kumi wanaotoa asilimia ishirini ya mapato yao wanaweza kumtegemeza vizuri sana
mchungaji mmoja na mishenari mmoja atakayeishi kwenye kiwango kile cha
mchungaji wao.
Wachungaji Hufanya Nini?
Fikiri
kwamba unamwuliza mshirika wa kawaida kanisani swali hili: “Je, ni kazi ya nani
kufanya yafuatayo:- kuwashuhudia watu ambao hawajaokoka? Kuishi maisha
matakatifu? Kuomba? Kuonya, kushauri na kusaidia waamini wengine? Kutembelea
wagonjwa? Kuweka mikono juu ya wagonjwa kwa ajili ya uponyaji? Kubeba mizigo
yaw engine? Kutumia karama zake kwa ajili ya kusanyiko? Kujikana, akijitoa kwa
ajili ya ufalme wa Mungu? Kufanya wanafunzi na kuwabatiza, na kuwafundisha
kutii amri za Kristo?”
Washirika
wengi wa kanisa, bila ya kusita, wangejibu kwa kusema, “Hayo yote ni majukumu
ya mchungaji.” Lakini, ni sawa?
Kulingana
na Maandiko, kila aaminiye anapaswa kuwashuhudia watu ambao hawajaokoka.
Mwe
tayari sikuzote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani
yenu; lakini kwa upole na kwa hofu (1Petro 3:15).
Kila
aaminiye anawajibika kuishi matisha matakatifu.
Bali
kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika
mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, ‘Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni
mtakatifu’ (1Petro 1:15, 16).
Kila
mwamini anatakiwa kuomba.
Furahini
sikuzote. Ombeni bila kukoma (1Wathes. 5:16, 17).
Kila
aaminiye anatazamiwa kuonya, kutia moyo na kuwasaidia waamini wengine.
Ndugu,
twawasihi, waonyeni wale wasiokaa
kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na
watu wote (1Wathes. 5:14. Maneno mepesi kukazia).
Kila
aaminiye anatakiwa kutembelea wagonjwa.
Nalikuwa
uchi, mkanivika. Nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama. Nalikuwa kifungoni,
mkanijia (Mathayo 25:36).
Majukumu Zaidi
Lakini,
si hayo tu. Kila aaminiye anapaswa kuweka mikono juu ya wagonjwa na kuwaponya
pia.
Na
ishara hizi zitafuatana na hao waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo;
watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha
hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona (Marko
16:17, 18).
Kila
aaminiye anapaswa kubeba mizigo ya waamini wenzake.
Mchukuliane
mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo (Wagalatia 6:2).
Kila
aaminiye anatazamiwa kutumia karama zake kwa ajili ya wengine.
Basi,
kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa
unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma
yetu; mwenye kufundisha katika kufundisha kwake; mwenye kuonya katika kuonya
kwake; mwenye kukirimu kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii; mwenye
kurehemu kwa furaha (Warumi 12:6-8).
Kila
mwamini anapaswa kujikana mwenyewe, na kujitoa kwa ajili ya Injili.
Akawaita
mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, ‘Mtu yeyote akitaka kunifuata na
ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye
kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili
yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha’ (Marko 8:34, 35).
Tena,
kila mwamini anatazamiwa kufanya watu kuwa wanafunzi, na kuwabatiza, na
kuwafundisha kutii amri zote za Kristo.
Basi
mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watu
hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na
kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni (Mathayo 5:19.
Maneno mepesi kukazia).
Kwa
maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji
kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa
mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu (Waebrania 5:12).
Basi
enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina
la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote
niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata
ukamilifu wa dahari (Mathayo 28:19, 20)
Majukumu
hayo yote yametolewa kwa kila aaminiye, lakini washirika wengi wa kanisa
hufikiri kwamba yametolewa kwa wachungaji tu! Pengine sababu ni kwamba
wachungaji wengi pia hufikiri kwamba hayo ni majukumu yao peke yao.
Basi, Wachungaji Wanapaswa Kufanya Nini?
Kama
majukumu hayo yote yametolewa kwa kila aaminiye, wachungaji basi wanatakiwa
kufanya nini? Kirahisi tu ni kwamba, wao wameitwa kuwawezesha hao waaminio
watakatifu kufanya mambo hayo yote (ona Waefeso 4:11, 12). Wameitwa
kuwafundisha hao waaminio watakatifu kutii amri zote za Kristo (ona Mathayo
28:19, 20) kwa kuonyesha mfano pamoja na kufundisha (ona 1Timo. 3:2;
4:12, 13; 5:17; 2Timo. 2:2; 3:16 – 4:4; 1Petro 5:1-4).
Maandiko
hayawezi kuwa wazi kuliko hivyo. Nafasi ya KiBiblia ya mchungaji sio kukusanya
watu wengi kiasi anachoweza Jumapili asubuhi kwenye ibada kanisani. Ni “kumleta
kila mtu mtimilifu katika Kristo” (Wakolosai 1:28). KiBiblia, wachungaji
hawatekenyi masikio ya watu (2Timo. 4:3). Wanafundisha, wanaonya, wanakemea,
wanakaripia, na kurekebisha, na yote hufanywa kwa msingi wa Neno la Mungu (ona
2Timo. 3:16 – 4:4).
Paulo
aliorodhesha baadhi ya sifa za mtu anayetaka kusimama katika nafasi ya
mchungaji, katika barua yake ya kwanza kwa Timotheo. Sifa kumi na nne kati kumi
na tano zinahusu tabia yake, kuonyesha kwamba mfano wa maisha yake ndicho kitu
cha muhimu zaidi sana.
Ni
neno la kuainiwa [kwamba] mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi
imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na
busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea
ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye
kupenda fedha; mwenye kusimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika
ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje
Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibuni, asije akajivuna
akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu
walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi (1Timo. 3:1-7).
Ukifananisha
sifa hizi na zile ambazo mara nyingi hutolewa na makanisa yanapotafuta
mchungaji mpya utagundua tatizo la msingi katika makanisa mengi. Wao hutafuta
meneja wa kusimamia wafanyakazi/mtu wa kustarehesha watu/mtoa hotuba
fupi/msimamizi/mwanasaikolojia/mkurugenzi wa shughuli na mipango/bingwa wa
kuchangisha fedha/rafiki wa kila mtu/farasi au punda wa kazi. Wanataka mtu “wa
kuendesha huduma ya kanisa.” Lakini, mwangalizi KiBiblia, zaidi ya yote lazima
we mtu mwenye tabia nzuri na aliyejitolea kwa Kristo, awe mtumishi wa kweli kwa
sababu lengo lake ni kujizaa mwenyewe. Lazima aweze kuwaambia washirika wake,
“Niigeni mimi, kama na mimi ninavyomwiga Kristo” (1Wakor. 11:1).
Kwa
maelezo zaidi kuhusu nafasi ya mchungaji, soma pia maandiko yafuatayo: Matendo
20:28-31; 1Timo. 5:17-20; na Tito 1:5-9.
Nafasi Ya Shemasi
Mwisho,
hebu tutazame kidogo habari za shemasi. Nafasi ya sehmasi ni nafasi nyingine
katika kanisa la mahali ambayo si miongoni mwa zile karama tano za huduma.
Mashemasi si kama wazee – wao hawana mamlaka ya kiutawala katika kanisa. Neno
la Kiyunani diakonos ambalo limetafsiriwa shemasi maana yake ni
“mtumishi” au “atoaye huduma”.
Wale
watu saba waliochaguliwa kwa ajili ya kazi ya kuwalisha wajane wa kanisa la
Yerusalemu kila siku ndiyo huhesabiwa kuwa mashemasi wa kwanza (ona Matendo
6:1-6). Walichaguliwa na kusanyiko na kupewa kazi na mitume. Wawili wao –
Filipo na Stefano – walipandishwa cheo na Mungu, wakawa wainjilisti wenye nguvu
sana.
Pia,
mashemasi wanatajwa katika 1Timo. 3:8-13 na Wafilipi 1:1. Tena, inaonekana
nafasi hii inaweza kuchukuliwa na mwanamume au mwanamke (ona 1Timo. 3:11).
Hiyo
ni njia nyingine ya kusema hivi: “Kwa ajili ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa
Yesu Kristo.”
Kama
wanafunzi wa Yesu walitazamiwa kuwafundisha wanafunzi wao kutii kila kitu Yeye
alichowaamuru, basi bila shaka wangewafundisha wanafunzi wao jinsi ya kufanya
wengine kuwa wanafunzi pia, na kubatiza na kuwafundisha kuyashika yote ambayo
Yesu aliamuru. Hivyo, kufanya wanafunzi, kubatiza na kufundisha wanafunzi
ingekuwa amri inayoendelea, na inayofanya kazi kwa kila mwanafunzi aliyefuata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni