Lakini kila mmoja wetu alipewa neema
kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo … Naye alitoa wengine kuwa mitume,
na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na
wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la
kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo
ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana
Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha
utimilifu wa Kristo (Waefeso 4:7, 11-13).
Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume,
wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama
za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina
za lugha (1Wakor. 12:28).
Wito wa karama
za kufanya huduma kama zinavyojulikana, ni tendo la
kuitwa kwa waamini fulani na kupewa uwezo ili kusimama katika nafasi kama
mtume, nabii, mwinjilisti, mchungaji au mwalimu. Hapa muhimu ni kuelewa kuwa hakuna mtu awezaye kujiweka mwenyewe katika nafasi hizo, kama ambavyo tunaona siku hizi kila mtu akijitwalia tu hizi nafasi ili kutengeneza umaarufu, na kukusanya kondoo waliokosa wachungaji. Ni lazima mtu aitwe na apewe karama hiyo na Mungu.
Inawezekana
kwa mtu mmoja kushika nafasi zaidi ya moja kati ya hizo, lakini ni kwa makundi
fulani fulani. Kwa mfano: Inawezekana mwamini mmoja akaitwa kushika nafasi ya
mchungaji na mwalimu, au nabii na mawalimu. Lakini si rahisi kwa mtu kuitwa
kushika nafasi ya mchungaji na mwinjilisti kwa sababu, huduma ya mchungaji
inamtaka kwamba abaki mahali pamoja akihudumia kusanyiko la mahali pamoja. Hivyo, hawezi kufaa kwa wito wa uinjilisti ambao unamtaka mtu kusafiri mara kwa mara.
Japo
hizo nafasi tano zote ni karama tofauti kwa makusudi tofauti, zimetolewa kwa
kanisa kwa kusudi moja kubwa la jumla – kuwawezesha watakatifu kwa ajili ya
kazi ya huduma” (Waefeso 4:12,).
Lengo
la kila mtumishi linapaswa kuwa kuwawezesha watakatifu kwa ajili ya kufanya
huduma. Lakini, mara nyingi, wale walio
katika huduma hujifanya kana kwamba wameitwa kuwastarehesha watu wa kimwili
wanaofika kanisani – si kuwawezesha watakatifu kuwa tayari kwa huduma. Kila mtu
aliyeitwa katika nafasi mojawapo kati ya hizo zilizotajwa anapaswa kutathmini
mara kwa mara mchango anaotoa kwa habari ya “kuwawezesha watakatifu kwa ajili
ya kufanya huduma”. Kama kila mtumishi angefanya hivyo, wengi wangeondoa
shughuli nyingi mbalimbali ambazo zinahesabiwa kwa sasa kwamba ni “huduma”.
somo litaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni