Tutazame Kwa Karibu Nafasi Ya Mtume
Neno
la Kiyunani linalotafsiriwa mtume ni apostolos na maana yake
halisi ni “aliyetumwa”. Mtume wa kweli wa Agano Jipya ni mwamini anayetumwa na
Mungu kwenda mahali fulani au maeneo fulani ili kuanzisha makanisa. Anaweka
msingi wa kiroho wa “jengo” la Mungu, na anafananishwa na fundi ujenzi mkandarasi.
Paulo, yeye mwenyewe akiwa mtume, aliandika hivi:
Maana
sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu. Ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la
Mungu. Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi kama mkuu wa wajenzi
wenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake (1Wakor.
3:9-10a).
“Mkuu
wa wajenzi” husimamia mpango mzima wa kujenga – yeye anaona jengo
lililokamilika. Si mtaalamu kama vile fundi seremala au mwashi. Anaweza kuwa
na uwezo wa kufanya kazi ya fundi seremala au mwashi, lakini pengine hataifanya
vizuri kama wao wenyewe. Vivyo hivyo, mtume anao uwezo wa kufanya kazi ya
mwinjilisti au mchungaji, lakini kwa muda tu wakati anapoanzisha makanisa.
(Mtume Paulo kwa kawaida alikuwa anakaa mahali kwa miezi sita hadi miaka
mitatu.)
Mtume
anafaa sana kuanzisha makanisa, kisha kuyasimamia ili kuhakikisha yanaendelea
kama Mungu anavyotaka. Mtume anawajibika kuweka wazee au wachungaji au
wasimamizi ili kuchunga kila kundi analoanzisha Biblia inasema "Hata nilipokwisha kuhubiri injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini". (Matendo 14:21-23)
Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuwaweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;Tito
1:5).
somo litaendelea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni