Nafasi Ya Mwinjilisti
Mwinjilisti
ni mtu aliyetiwa mafuta kuhubiri Injili. Jumbe zake zimepangwa kuwaongoza watu
watubu na kumwamini Bwana Yesu Kristo. Zinaambatana na miujiza yenye kuvuta
usikivu wa wasioamini na kuwafanya kuamini ukweli wa ujumbe wake.
Bila
shaka walikuwepo wainjilisti wengi sana katika kanisa la kwanza, lakini ni mtu
mmoja tu anayetajwa katika kitabu cha Matendo kama mwinjilisti. Jina lake ni
Filipo. Tunasoma hivi: “…Tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa
Injili aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake” (Matendo 21:8. Maneno.
Filipo
alianza huduma yake kama mtumishi tu (au tuseme, “shemasi”) ambaye kazi yake
ilikuwa kusimamia meza (ona Matendo 6:1-6). Akapandishwa kufikia nafasi ya
mwinjilisti wakati wa mateso ya kanisa yaliyotokana na kuuawa kwa Stefano. Kwa
mara ya kwanza alihubiri Injili huko Samaria.
Filipo
akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. Na makutano kwa nia
moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara
alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao,
wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza na viwete, wakaponywa. Ikawa
furaha kubwa katika mji ule (Matendo 8:5-8).
Ona
kwamba ujumbe wa Filipo ulikuwa mmoja tu – Kristo. Lengo lake lilikuwa kuanza
kufanya watu kuwa wanafunzi, yaani, wafuasi watiifu wa Kristo. Basi,
alimtangaza Kristo kama mtenda miujiza, Mwana wa Mungu, Bwana, Mwokozi na
Hakimu anayerudi upesi. Akawashauri watu watubu na kumfuata Bwana wake.
Ona
pia kwamba Filipo aliwezeshwa kwa ishara na maajabu, vilivyothibitisha ujumbe
wake. Mtu anayesimama katika nafasi ya mwinjilisti atatiwa mafuta kwa karama za
kuponya na zingine za kiroho. Kanisa la uongo lina wainjilisti wa uongo ambao
wanahubiri injili ya uongo. Dunia imejaa wainjilisti wa namna hiyo, na ni
dhahiri kwamba Mungu hathibitishi mahubiri yao kwa miujiza na uponyaji. Sababu
ni kwamba hawahubiri Injili Yake. Hawamhubiri Kristo. Kwa kawaida, wanahubiri
kuhusu mahitaji ya watu na jinsi Kristo anavyoweza kuwapa uzima tele, au
wanahubiri mfumo wa wokovu ambao hautaki toba. Wanawaongoza watu katika uongofu
bandia wenye kupooza hatia yao bila kuwaokoa. Matokeo ya mahubiri yao ni kwamba
watu hata hawana nafasi za kuzaliwa mara ya pili, kwa sababu hawaoni haja ya
kupokea kitu ambacho wanafikiri wanacho tayari. Wainjilisti aina hiyo
wanamsaidia Shetani kujenga ufalme wake.
Nafasi
ya mwinjilisti haiko kwenye ile orodha ya karama zingine za huduma katika
1Wakorintho 12:28, kama inavyotajwa katika Waefeso 4:11. Ila, kwa kuwa inatajwa
“miujiza na karama za kuponya”, hizo zinahusika na nafasi ya mwinjilisti kwa
sababu zilikuwa kawaida katika huduma ya uinjilisti ya Filipo, nazo zinatoa
uthibitisho wa Mungu kwenye huduma yoyote ya mwinjilisti.
Wengi
wanaotembea kutoka kanisa hadi kanisa na kujiita wainjilisti si wainjilisti
kweli kwa sababu wanahubiri katika makanisa, tena kwa Wakristo. Kisha hawana
ule uwezo wa karama za kuponya wala miujiza. (Kuna wanaojifanya kuwa na karama
hizo, lakini wanawadanganya wajinga tu. Miujiza yao mikubwa ni kuwaangusha
watu, tena kwa kuwasukuma.) Hao watumishi wanaosafiri wanaweza kuwa waalimu au
wahubiri au wenye kuonya (ona Warumi 12:8), lakini hawako kwenye nafasi ya
mwinjilisti. Ila, inawezekana Mungu kuanza huduma ya mtu kwa kumfanya mwonyaji
au mhubiri na baadaye kumpandisha hadi nafasi ya mwinjilisti.
Kwa
maelezo zaidi kuhusu nafasi ya mwinjilisti, soma Matendo 8:4 – 40, ambayo ni
taarifa ya huduma ya Filipo. Ona hapo jinsi karama za huduma zinavyotegemeana
na umuhimu wake (hasa mstari wa 14 hadi 25) na jinsi Filipo alivyohubiri Injili
kwa watu lakini pia akaongozwa na Mungu kuwahudumia watu binafsi (ona Matendo
8:25-39).
Inaonekana
kwamba wainjilisti wameagizwa kuwabatiza waongofu wao, lakini hawajapewa agizo
la kutoa ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa waamini wapya. Hilo kimsingi ni jukumu
la mitume au wachungaji/wazee/waangalizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni