Mitume Wa Kweli Na Wa Uongo
Inaonekana
kwamba baadhi ya watumishi siku hizi, kwa kutamani kuwa na madaraka juu ya
makanisa, ni wepesi kujitangaza kwamba wameitwa kuwa mitume. Lakini wengi wao
wana matatizo makubwa. Kwa kuwa hawajaanzisha makanisa (au labda wana moja au
mawili) na hawana karama wala upako wa kiBiblia wa utume, inawabidi watafute
wachungaji wepesi kudanganyika watakaowaruhusu wao kuwa na mamlaka juu ya
makanisa yao. Kama wewe ni mchungaji, usidanganywe na hao mitume wa uongo wenye
kujitukuza wenyewe na wenye njaa ya mamlaka. Wao kwa kawaida ni mbwa mwitu
waliovaa mavazi ya kondoo. Mara nyingi wanachotafuta ni fedha tu. Maandiko
yanaonya kuhusu mitume wa uongo yanasema;
Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo (2Wakor. 11:13)
Nayajua matendo yako, na taabu yako, subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana nawatu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; (Ufunuo 2:2). Kama inabidi
wakwambie wao ni mitume, basi ni ishara kwamba wao si mitume. Matunda yao
yanapaswa kuzungumza.
Mchungaji
anayeanzisha kanisa na kuendelea kulichunga kama mchungaji kwa miaka mingi si
mtume. Pengine wachungaji aina hiyo wanaweza kuitwa “wachungaji wa
kitume” kwa kuwa walianzisha makanisa wenyewe. Pamoja na hayo, wasishike nafasi
ya mtume kwa sababu mtume huendelea kuanzisha makanisa.
“Mishenari”
aliyetumwa kweli na Mungu na kutiwa mafuta – ambalo ndilo jina la mitume siku
hizi – mwenye wito wa kuanzisha makanisa, anaweza kusimama kama mtume. Lakini,
wamishenari wanaofanya kazi ya kuanzisha shule za Biblia au kuwafundisha
wachungaji si mitume bali waalimu.
Huduma
ya kweli ya mtume huonekana kwa ishara na maajabu, ambavyo ni vyombo
vinavyosaidia kuanzisha kanisa. Paulo aliandika hivi:
Kwa sababu sikuwa duni ya mtume
walio wakuu kwa lolote, nijapokuwa si kitu. Kweli ishara za mtume zilitendwa
katikati yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza (2Wakor.
12:11b-12).
Kama
mtu hana ishara na maajabu katika huduma yake, yeye si mtume. Basi, mitume wa
kweli si wengi, na hawapatikani katika kanisa bandia, lisilo takatifu, lenye
kuhubiri injili bandia. Sana sana wanapatikana katika maeneo mapya kabisa
duniani ambayo hajapata Injili bado.
CHEO CHA JUU CHA MTUME
Katika
orodha zote za karama za huduma katika Agano Jipya, nafasi ya mtume hutajwa
kwanza, kuonyesha kwamba ndiyo wito wa hali ya juu zaidi Biblia inasema "Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; (Waefeso 4:11)
"Na Mungu amewaweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha". (1Wakor. 12:28).
Hakuna
mtu aanzaye huduma yake kama mtume. Mtu anaweza kuwa na wito wa mtume, lakini
hataanza katika nafasi hiyo. Ni lazima kwanza ajithibitishe kuwa mwaminifu kwa
miaka mingi katika kuhubiri na kufundisha, kisha hatimaye atasimama katika
nafasi ambayo Mungu amemwandalia. Paulo aliitwa kuwa mtume toka tumboni mwa
mama yake, lakini alifanya huduma kwa miaka mingi kabla ya kuingia katika
nafasi hiyo hatimaye (angalia Wagalatia 1:15 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake"
Wagalatia– 2:1)
"Kisha baada ya miaka kumi na minne, nalipanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami".
Alianza kama mwalimu na nabii
Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Mfalme Herode, na Sauli (ona Matendo 13:1-2),
ndipo baadaye akapandishwa cheo na kuwa mtume, wakati
alipotumwa na Roho Mtakatifu
(ona Matendo 14:14).
"Walakini mitume Barnaba na Paulo, walipopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakapiga kelele."
Tunaona
wengine wakitajwa kama mitume licha ya Paulo na wale Thenashara, katika Matendo
1:15-26; 14:14; Warumi 16:7; 2Wakor. 8:23; Wagalatia 1:17-19; Wafilipi 2:25 na
1Wathes. 1:1 na 2:6. (Neno mtenda kazi katika 2Wakor. 8:23 na Wafilipi
2:25 katika Kiyunani ni apostolos.) Hii hupingana na dhana iliyoko siku
hizi kwamba nafasi ya mtume ilikuwa kwa ajili ya watu kumi na mbili tu.
Ila,
ni mitume kumi na mbili tu wanaoweza kuhesabiwa kuwa “Mitume wa Mwanakondoo,”
na ni hao kumi na mbili tu ndiyo watakaokuwa na nafasi ya pekee katika utawala
wa Kristo wa miaka elfu moja (tazama Mathayo 19:28; Ufunuo 21:14). Hatuhitaji
tena mitume kama Petro, Yakobo na Yohana ambao walivuviwa kipekee ili kuandika
Maandiko, kwa sababu ufunuo wa Biblia umekamilika. Ila, sku hizi bado
tunahitaji mitume watakaoanzisha makanisa kwa nguvu za Roho Mtakatifu, kama
walivyofanya akina Paulo na wengine, kulingana na tunavyosoma katika Kitabu cha
Matendo ya Mitume.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni