Nafasi Ya Nabii
Nabii
ni mtu anayepokea mafunuo ya Mungu na kusema kwa upako wa Mungu. Kwa kawaida,
anatumiwa mara kwa mara katika karama ya kiroho ya unabii pamoja na zile karama
za ufunuo: neno la hekima, neno la maarifa, na kupambanua roho.
Mwamini
yeyote anaweza kutumiwa na Mungu katika karama ya unabii kama apendavyo Roho,
lakini hiyo haimfanyi kuwa nabii. Nabii kwanza kabisa ni mtumishi anayeweza
kuhubiri au kufundisha kwa upako. Kwa kuwa nafasi ya nabii inaonekana kuwa
mwito wa pili (ona orodha katika 1Wakor. 12:28) "Na Mungu ameweka wengine katika kanisa wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu...," hata mtumishi wa kudumu
asingeweza kutiwa katika nafasi ya nabii mpaka awe katika huduma kwa miaka
kadhaa. Inapofikia wakati wake kushika nafasi hiyo, atakuwa na vitendea kazi
vya kiroho vinavyoambatana na nafasi yenyewe.
Watu
wawili wanaotajwa katika Agano Jipya kuwa manabii ni Yuda na Sila. Tunasoma
katika Matendo 15:32
"Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha".
kwamba walitoa unabii mrefu kwa kanisa la Antiokia, kama
ifuatavyo:
Tena
Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno
mengi, wakawathibitisha.
Mfano
mwingine wa nabii kutoka katika Agano Jipya ni Agabo. Tunasoma hivi katika
Matendo 11:27-28:
Siku hizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia. Na
tulipokusanyika, akasimama mmoja wao jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa
Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo
ikatukia katika siku za Klaudio.
Ona
kwamba Agabo alipewa neno la hekima – kitu kuhusu wakati ujao kilifunuliwa
kwake. Agabo hakujua kila kitu ambacho kingetokea katika siku zijazo, ila
alifahamu yale tu ambayo Roho Mtakatifu alipenda kumfunulia.
Katika
Matendo 21:10-11, kuna mfano mwingine wa neno la hekima kufanya kazi katika
huduma ya Agabo. Hapa, ilitokea kwa ajili ya mtu mmoja, Paulo.
Basi,
tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka
kutoka Uyahudi. Alipotufikia, akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono,
akasema, “Roho Mtakatifu asema hivi, ‘Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu
watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa
Mataifa’.”
Je,
Maandiko yanaruhusu katika kipindi hiki cha agano jipya kutafuta ushauri binasi
kutoka kwa manabii? Hapana. Sababu ni hii: Waamini wote wana Roho Mtakatifu
ndani yao ili kuwaongoza. Nabii anachoweza kufanya ni kuthibitisha tu
kile ambacho mwamini tayari anajua ni mwongozo wa Mungu katika roho yake. Kwa
mfano: Wakati Agabo alipomtabiria Paulo, hakumpa mwongozo kwamba afanye nini.
Alithibitisha tu kile ambacho Paulo alikwisha fahamu kwa muda mrefu.
Kama
tulivyokwisha kusema mapema, Paulo alishika nafasi ya nabii (na mwalimu) kabla
ya kuitwa katika huduma ya utume (ona Matendo 13:1). Tunajua Paulo alipokea
mafunuo kutoka kwa Bwana kulingana na Wagalatia 1:11-12, na pia alipata maono
mengi tu (ona Matendo 9:1-9; 18:9, 10; 22:17-21; 23:11; 2Wakor. 12:1-4).
Kama
ilivyo kwa habari ya mitume wa kweli, hatupati manabii wa kweli katika kanisa
la uongo. Kanisa la uongo huwaepuka manabii wa kweli kama Sila, Yuda au Agabo.
Sababu ni kwamba manabii wa kweli wataleta ufunuo wa Mungu kutopendezwa na
kutokutii kwao (kama Yohana alivyofanya kwa makanisa mengi ya Asia Ndogo katika
sura mbili za kwanza za Ufunuo). Kanisa la uongo halipendi hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni