Kusifu
na kuabudu kama kutafanyika kama inavyopaswa, ni njia mojawapo kubwa inayoweza
kukuza kanisa kwa kasi kubwa ya ajabu.
Lakini
ni masikitiko makubwa sana kwamba maana hasa ya sifa imeanza kupotea kwa sehemu
kubwa katikati ya wana wa Mungu, na kwa waimbaji wa nyimbo za injili ndio hali
mbaya kabisa.
Wengi wao hawapo
kiroho, ila wapo zaidi kibiashara. Wapo tayari
wasimpendeze Mungu lakini wawapendeze wanadamu. Kwa maana hiyo
wanajali zaidi utukufu wa wanadamu, kuliko utukufu wa Mungu.
Na ili
wawafurahishe wanadamu, wanajaribu kuchukua kila kitu cha kimwili na kukifanya
kuwa ni cha kiroho. Matokeo yake ni
kuzidi kufifisha nuru ya Kristo katika kusanyiko la wana wa Mungu.
Kwa Mungu wetu sadaka hii
ya sifa hutolewa kwa hiari ya mtu bila kujali ana shida gani au yuko katika
hali gani.
- Ibada ya kusifu
na kuabudu inapofanyika ipasavyo husababisha mlipuko na ukuaji wa kanisa,
- kwani humpa
nafasi Roho Mtakatifu kutembea kwa wingi katikati ya watakatifu (2Wakorinto
6:16)
“tena pana patano
gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye
hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba nitakaa ndani yao, na kati yao
nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu”.
- Matendo ya Mungu huonekana na kanisa
huongezeka kiidadi.
Matokeo ya kusifu na
kuabudu
Kanisa huongezeka kwa kasi
kama ilivyokuwa siku ya pentekoste.
Kushusha uwepo wa Mungu na
nguvu za Mungu kusambaa Watu wasioamini huvutwa na
nguvu za uwepo wa Mungu na kufanana,
(1Samuel 19:18-21)
a.
Mfalme Sauli alikamatwa na
uwepo siku tatu
“Hivyo Daudi
akakimbia, akajiponya, akamwendea Samweli huko Rama, akamwambia hayo yote Sauli
aliyomtendea. Kisha yeye na Samweli wakaenda na kukaa katika Nayothi, Naye
Sauli akaambiwa, kusema Angalia yule Daudi yuko katika Nayothi, huko Rama. Basi
Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamii ya
manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, roho ya Mungu
ikawajilia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri. Naye Sauli alipoambiwa,
akatuma wajumbe wengine, wao nao pia wakatabiri kisha yeye mwenyewe akaenda
Rama, akafika kunako kile kisima kikubwa kilicho huko Seku akauliza, akasema
Je, wako wapi Samweli na Daudi? Na mtu mmoja akajibu. Tazama wako Nayothi huko
Rama. Basi akaenda Nayothi huko Rama; na roho ya Mungu ikamjilia yeye naye,
akaendelea mbele huku akitabiri, mpaka kufika Nayothi huko Rama, Naye akavua
nguo zake, akatabiri mbele ya Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha
siku ile. Kwa hiyo watu husema Je, Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?”
- Sauli mwenyewe alipokwenda
kumfuatilia Daudi Roho wa Mungu alimjilia yeye naye akakamatwa kwa siku tatu.
- Mtume Paulo anasema kwenye
(1Wakorinto 14:24b)
“Siri za moyo
wake huwa wazi na hivyo ataamua kumuabudu Mungu akianguka kifudifudi na kukiri
kuwa Mungu yu kati yenu bila shaka, matokeo yake mtu huyo ataokoka.”
- Watu wengi wenye
majini na mapepo wanapojihudhurisha au kupita karibu na maeneo ambayo watu wa
Mungu wanasifu na kuabudu, mapepo hushindwa kustahimili uwepo wa nguvu za Mungu
yanalipuka na watu hao wanafunguliwa na kumgeukia Mungu.
Mungu wetu hufanya kiti chake
cha enzi juu ya sifa za watu wake. (Zaburi 22:3) 2Nyakati 5: 13-14)
- Mahali pa ibada
hakuna atakayeondoka akiwa kama alivyoingia,
- bali ataondoka
akiwa na utiisho wa uwepo wa nguvu za Mungu uliojidhihirisha kwake.
- Watu waliookoka,
wahamiaji na wageni hudumu mahali penye uwepo wa nguvu za Mungu na wote
waingiao hudumu hapo angalia
b.
Makutano walishikwa na
uwepo wa Mungu,
(Mathayo 15:29-39)
“Yesu
akaondoka huko akafika kando ya bahari ya Galilaya, akapanda mlimani, akaketi
huko. Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na
wengine wengi, wakawaweka miguuni pake, Hata ule mkutano wakastaajabu,
walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na
vipofu wanaona. Wakamtukuza Mungu wa Israeli. Yesu akawaita wanafunzi wake,
akasema, nawahurumia makutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekuwa pamoja nami,
wala hawana kitu cha kula; tena kuwaaga wakifunga sipendi, wasije wakazimia
njiani. Wanafunzi wake wakamwambia. Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani hata
kushibisha mkutano mkuu namna hii? Yesu akawaambia mnayo mikate mingapi?
Wakasema saba na visamaki vicheche. Akawaagiza mkutano waketi chini. Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki
akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.
Wakala wote wakashiba. Wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, makanda saba,
yamejaa. Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto.
Akawaaga makutano, akapanda chomboni, akaenda pande za Magadani,”
Hapa unaweza kuona mambo
yafuatayo;-
- Makutano hawa
walidhoofu kwa sababu ya kuona njaa,
- lakini
hawakuondoka kwenye mafundisho ya Bwana Yesu kwa sababu ya nguvu kubwa ya uwepo
wa Mungu.
- Ukiona watu
kwenye ibada wakiangalia saa, wakihamaki ibada inapochelewa kwisha na wengine
kuamua kuondoka kabla ibada haijaisha,
- Hiyo ni ishara
tosha ya kufahamu kwamba mahali hapo hapana uwepo wa Mungu na nguvu zake,
- Bali panakwenda
kimazowea. Au pana namna ya mapokeo ya ibada za kidini.
c. Kwenye mlima wa ugeuko (Marko 9:5)
Petro
alimwambia Bwana Yesu kuwa ni vizuri sisi kuwepo hapa tufanye vibanda vitatu.
Maneno ya mtume Petro yalitokana na uwepo wa utukufu wa Mungu. Petro alisahau
kwamba alikuwa na familia na pia wanafunzi wenzao tisa waliowaacha walikuwa
wanawahitaji pia. Aliona ni vema na kutamani kukaa pale mahali penye utukufu wa
Mungu na uwepo wake. Mahali ambapo hapana watu wala mahitaji muhimu ya maisha
palionekana ni pazuri zaidi kuwepo kuliko mahali pengine popote, yeyote
anayeokoka au kuhamia katika kanisa lenye kushusha uwepo wa Mungu katika ibada
ya kusifu na kuabudu, hataondoka mahali hapo.
Matokeo ya kusifu na kuabudu
kwa watakatifu.
- Huleta hofu ya
Mungu katikati ya watakatifu.
- Huyeyusha mioyo
migumu katika kupokea mambo ya Mungu.
- Hulipua vizuizi
vya kuikulia neema ya Mungu
- Nguvu ya Mungu
huonekana.
- Utendaji wa Roho
Mtakatifu hujidhihirisha kwa karama kuchanua.
- Moto wa uamsho
hutembea na maelfu ya watu kuokoka.
Matokeo ya kusifu
na kuabudu kwa kanisa
(Yohana 4:1-23)
- Mungu hupewa sifa
na utukufu
- Ni ibada ya moyo
kwa moyo na Mungu (Yohana 4:24)
- Roho ya mtu au
yule mtu wa ndani ndiye awezaye kuabudu.
- Mungu ni Roho
anawatafuta watu kama hao wamwabudu.
- Watu hawa ni
wachache sana na adimu miongoni mwa wengi waziendeao nyumba za siku za
jumapili. Ndio maana Mungu anafanya kuwatafuta.
- Mungu wetu anayo
namna ya kuabudiwa kutoka katika roho ya mtu wa ndani, ni mtu wa ndani pekee
ndiye awezaye kumuabudu Mungu ipasavyo.
- Yeye ndiye mwenye
mahusiano na ushirika hai na Mungu.
- Mtu asiyeokoka
hawezi kuabudu Mungu kihalisi (Mt 15: 8-9)
- Asiye okoka
hawezi kuufikia ujuzi wa kweli katika kuabudu.
- Mtu aliyeokoka
ndiye pekee awezaye kuabudu halisi kwa kuwa mwelekeo wa kuabudu ni kutoka kwa
mwamini kwenda kwa Mungu
- Toka kwa mtu wa
ndani hadi mawazo kisha maneno.
- Maneno ni mawazo
yaliyovishwa sauti hatimaye kuingia kwenye vitendo (udhihirisho wa mwitikio wa
moyo)
- Twamsifu na
kumuabudu Mungu tukijieleza kwake.
- Upendo wetu,utii
wetu,kujitoa kwetu kwake twasema kuwa
§ Mungu ni nani
§ Amesema nini
§ Anafanya nini na
alifanya nini
- Asiyeamini mtu wa
litulgia hawezi kufanya yote haya yeye binafsi toka katika vilindi vya moyo
wake.
- Mungu hana
ushirika na kiumbe katika kuabudiwa.
- Katika maandiko
(Mt 4: 9-10) majibu ya Bwana Yesu kwa shetani yanaonyesha kuwa Mungu hana
mshirika katika kupokea ibada na kiumbe yeyote duniani, mbinguni au kuzimu
(kutoka 34:14) Mungu anasema kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu.
Wafilisti katika kitabu cha
(1Samweli 5:1-5) waliliteka sanduku la Mungu na kulitia katika nyumba ya dagoni
mungu wao. Wakaliweka sanduku la Mungu karibu na dagoni mungu wao,
- hii ilikuwa ni sawa na
kumlinganisha Mungu YEHOVA na dagoni.
- Kwa waisraeli lilipokuwa
sanduku la Mungu ilikuwa ni ishara kuwa YEHOVA yuko mahali hapo.
- Wafilisti walipoamka
asubuhi siku ya pili, kumbe sanamu lao dagoni limeanguka kifudifudi mbele ya
Mungu wa Israeli.
- Huku kichwa cha dagoni na
vitanga vya mikononi vimekatika vipo vimelala kizingitini dagoni imebaki
kiwiliwili.
YEHOVA Mungu wetu ni Mungu
mwenye wivu, na hatalinganishwa na chochote, maana yeye ndiye muumbaji.
- Iwe binadamu, malaika au
shetani na mapepo yake ambao awali walikuwa ni sehemu ya malaika wa Mungu kisha
wakaasi, hapo ndipo walipopoteza nafasi zao katika ufalme wa Mungu mbinguni.
- Kumbuka kwamba tumeumbwa
ili tumuabudu Mungu. Hii ndio moja ya sababu kubwa ya kuumbwa kwa jinsi
tulivyo. (Zab 103:1).
Kama vile wanadamu waundapo
magari na mitambo mbalimbali, wanaunda wakilenga kutosheleza uwezo wa kutendea
kazi iliyokusudiwa.
- Hali kadhalika ndivyo
ilivyo hata tunapoamua kujenga nyumba, barabara, n.k.
- vivyo hivyo kwa wanadamu kila
kiungo chetu kimekuwepo pia kutuwezesha kufikia makusudi ya Mungu ya kumwabudu
tuwapo katika dunia tuliyoumbiwa. (Tazama Isaya 45:12).
Viungo vyetu pia
hutuwezesha kuwa na mahusiano na dunia lakini tukishatoka duniani na kuvishwa
mwili mpya (1Wakorinto 15:40) tujapokuwa katika mwili mpya lakini katika umbo
la kibinadamu tutakuwa na;-
- Miguu inayoweza kucheza kwa
urahisi
- Magoti yanayoweza kujikunja
tuabudupo
- Kiuno na mgongo uwezao
kuinama na kuinuka
- Mabega yawezayo kucheza
- Mikono iwezayo kupiga
makofi kunyanyuliwa juu
- Kichwa kiwezacho kucheza
- Kinywa chenye kutoa sauti
zenye tuni mbalimbali.
Hakuna kiumbe aliyeumbwa
huru kutenda vitendo vingi kama binadamu tazama (Zaburi 139:15).
Sifa
za Bwana ni bubujiko la moyo (Yoh 4:10)
- Bwana alimfananisha Roho
Mtakatifu na maji yabubujikayo, ampokeaye humuondolea kiu milele.
- Maji hayo hububujika kutoka
utu wa ndani wa mtu hadi kudhihirika katika utu wan je (utu wa asili)
- Hali ya ukame kiu
haitakuwapo tena, hutasifu na kuabudu kwa dakika 2 na kujisikia kuchoka.
- Hutakuwa na moyo unaokerwa
na bubujiko la Roho Mtakatifu.
- Hutazuwia kunena kwa lugha
(1Wakorinto 14:39)
Kuna watu wanaodhani kuwa
utaratibu wao wa ibada ni sahihi,
- Watu hao hupanga kusifu na
kuabudu kwa dakika zisizozidi 10.
- Lakini matengenezo na
mipango yao ya kanisa hupangwa husemwa kwa dakika zaidi ya 30.
- Poroja za kusalimiana na
kutambulishana huchukua zaidi ya saa.
- Hapo wakisahau makusudi ya
Mungu kwa wanadamu.
Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandika kitabu
hiki kuhusu ibada.
Naamini kwamba bila ya himizo la Roho Mtakatifu ndani
yangu nisingeweza kukamilisha kazi hii.
Ni matumaini yangu kwamba kila atakayesoma atapata msaada
na kukua kiroho.
Wito wake kwa Kanisa la Kristo ni kuwataka waamini waijue
ibada ya Kiroho na ya Kweli yenye upako wa Roho Mtakatifu. Ambapo waabuduo
watamwabudu Mungu katika Roho na Kweli, na kurejesha maana ya sifa, ibada na
kuabudu kulikopotea hekaluni mwa Bwana. Ibada ya kweli italeta furaha ya Roho
Mtakatifu maishani mwa waamini na kurejesha tumaini la utukufu mioyoni mwao
maana tayari wameona uwepo wa Mungu katikati yao, kisha kujenga imani zao, na
shauku yao kwenda kuwa pamoja na Bwana Mbinguni.
IBADA NI NINI?
Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu linalofanywa na
mtu kwa kiumbe aliye mkuu katika mazingira yake yote, kiroho na kimwili na
kiumbe huyo akaaminiwa kuwa ni MWENYE ENZI asiyefananishwa na kiumbe kingine
mkamilifu katika matendo yake.
Kuabudu Mungu katika Roho na Kweli kunaweza kukafanywa
wakati wowote na mahali popote mradi lengo ni kumfanyia Mungu IBADA.
- Jambo la
muhimu ni yule tunayemwabudu kuliko mahali tunapofanyia ibada
- ingawa mahali tunafanyia ibada ni kitu chema ,lakini
pasipewe nafasi mioyoni mwetu na kuheshimiwa kama sehemu ya ibada.
- Pamoja na hoja hiyo mahali pa ibada pasipuzwe na
kudharauliwa maana pamewekwa wakfu kwa huduma ya Mungu pametakaswa.
- Mtu akionyesha dharau au kuto paheshimu anaweza kupata
madhara,
- hivyo ni muhimu kila mtu ajue jambo hili na kuenenda kwa
utaratibu na kwa heshima mahali hapo.
Kwa vile Ibada ni shughuli ambayo inashikamana sana na
mfumo wa maisha ya mwanadamu, na kwamba ibada hutofautiana sana katika maana na
mitazamo kulingana na imani ya mtu juu ya Mungu anayemwabudu, ni vema tukaelewa
kwa usahihi ibada ninini kwa mujibu wa Biblia ifundishavyo.
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa
huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya
kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msifuatishe namna ya dunia
hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya
Mungu yaliyo mema , ya kupendeza, na ukamilifu”. (Rumi 12:1-2)
Tendo la Ibada ni tendo la kujitoa kama dhabihu, lakini
ibada ya kweli lazima dhabihu hiyo iwe hai na takatifu, Mwili, Roho na ufahamu
viwe na lengo moja lakumfanyia Mungu Ibada takatifu basi, ambapo ibada nje ya
utakatifu si ibada inayompendeza.