Ni
muhimu kila mwamini ajue kuimba nakumsifu Mungu kwa midomo yake, kusifu na kuabudu
si kwa watu fulani au kundi maalumu tu. Bali uimbaji ni wajibu wa kila mtu
ndani ya ibada. Ni muhimu iwepo tahadhari kwa kanisa kutojisahau jukumu la
kuimba kuiachia kwaya na wengine wakawa wasikilizaji na watazamaji, hilo ni
jambo la hatari na ni anguko mbele za Mungu. Kanisa lidumu katika sifa daima
kwa ujumla.
KWAYA: Ni chombo chema sana ndani ya ushirika. Kama tunavyoona katika neno la Mungu INyak 16:4 INyak 23:30, IINyak 5:12-14 Haya ni maandiko yanayoelezea huduma ya kwaya katika ibada ilivyo muhimu.
(INyak 16:4-7)
Walawi walitengwa
wamtumikie Bwana katika kumkumbusha Mungu na kutoa shukrani na sifa. Asafu
alikuwa kiongozi mkuu wa huduma hii hekaluni
(INyak 23:30-31)
Kazi ya kwaya
ilikuwa ni kutoa huduma ya sifa na shukrani katika ibada ya asubuhi na jioni
kila siku hekaluni. Ratiba hii ya huduma inatakiwa idumishwe hata leo. Ni
makosa kudhani kwamba kwaya ni ya siku maalum ama Jumapili tu, kwaya ipewe
kuhudumu katika kila ibada.
(2Nyak 5:12-14.)
Waimbaji walibaki
ndani ya hekalu wakiwa na roho moja, wakiimba sauti zao kwa mpangilio,
wakimsifu na kumshukuru Mungu, na kuimba sambamba na muziki wa vyombo wakimsifu
Bwana kwa wema na fadhili zake. Hekalu likajawa na utukufu wa Mungu, wingu la
uwepo wa Mungu likawafunika. Huduma ya kwaya ni muhimu kama tunavyoona hapo
juu, kushusha uwepo wa Mungu na kuliongoza kanisa kumsifu nakumshukuru Mungu
kwa wema wake.
Hii inamaanisha
kwaya ina jukumu la kutoa huduma ya sifa na shukrani, na kutunga nyimbo zenye
mfumo huo bila kusahau utakatifu wa maisha yao.
Utunzi wa nyimbo
uzingatie maadili ya kiroho, neno, mazingira, mahitaji ya kijamii, ubora wa
mashairi, usanifu wa kitaaluma, Uongozi wa Roho Mtakatifu.
Si vema kuibuka na
wimbo usiku mmoja na kuutumbukiza katika huduma. Wimbo unaweza kuutunga kwa
muda mfupi ama kwa muda mrefu kutegemeana na kuridhika kwako ukizingatia hayo
yaliyo tajwa hapo juu.
Ni
jambo muhimu pawepo na maongozi makini katika kwaya kama Asafu alivyoongoza
kwaya ya hekalu. Kwaya ni huduma haipaswi kuongozwa kwa mfumo wa kisiasa
(kupiga kura) bali kwa mfumo wa huduma na malengo ya kihuduma na hasa kumtukuza
Mungu ambapo kiongozi mkuu ni yule aliye na maono, na mbeba huduma ambaye ni
mwalimu. Mwalimu ni kiongozi Mkuu wa kwaya kwa mujibu wa maandiko.
Uongozi
wa aina hiyo pamoja na kamati zake utaendeleza huduma kama ilivyo katika neno.
Mwalimu hapaswi kupigiwa kura bali anakuwa mwalimu kwa kipawa alichopewa na
Mungu, hicho ndicho kinampa nafasi ya kuwa kiongozi wa kwaya.
Kila
kanisa la mahali pamoja lizingatie kwa makini kulea vipawa na kuwatambua Walawi
(waimbaji) waliopo kanisani na kuwasimika katika huduma hiyo kama mfalme Daudi
alivyofanya (INyak 16:1-7).
Mchungaji
awe karibu sana na kwaya katika utendaji wa siku kwa siku ili kudumisha
mshikamano wa huduma yake na kwaya na kanisa, na kutoa msaada matatizo
yanapotokea.
1.
ITEGEMEZE
KWAYA
Kanisa
zima liwe mdau mkuu wa kutegemeza kwaya kwa hali na mali ili iweze kusonga
mbele katika fani ya uimbaji pasipo kukwama. Kumbuka asilimia sabini na tano ya
shughuli za kanisa katika ibada ni kusifu (kuimba), kwa hiyo ni jambo jema
wakristo wakawekeza nguvu zao katika kwaya ya kanisa. Kwaya
zenye mafanikio ni zile ambazo nyuma yao iko nguvu ya kanisa kwa hali na mali,
na maombezi.
Kwaya
ina mvuto wa ajabu kwa watu, katika matukio mbalimbali ya kijamii. Kwa hiyo ni
vema ipewe nafasi ya kutoa huduma katika matukio hayo, kama vile mikutano,
semina, misiba, harusi, sherehe za kanisa na za kijamii maadamu kinachofanyika
hakipingani na imani yetu na hakimdhalilishi Yesu.
Matukio
ni uwanja mzuri kwa kwaya kumhubiri Yesu kupitia ujumbe wa nyimbo. Kama Kanisa
litailea kwaya vizuri litavuna matunda ya baraka yasiyo na kifani.
MAFUNZO
NI MUHIMU
Kanisa
liimarishe na kufanya juhudi za makusudi kuwawezesha waimbaji wote kwa kuwapa
mafunzo ya kusifu na kuabudu katika Roho na kweli, na kuhakikisha waimbaji wana
viwango vya uimbaji vinavyokubalika.
Ibada
ni kitu kitakatifu ambacho kinatakiwa kufanyika kwa utaratibu, hofu na
unyenyekevu na kwa tahadhari kubwa ili kumpa Mungu heshima inayomstahili, kwa
kila tendo na dhamira ya moyo iliyo safi.
Utaratibu
huu ulikuwepo katika ibada ya Agano la kale na unapaswa kuendelezwa katika
kanisa la leo.
(INyak 25:6-8, Zab 33:1-2)
Kila mwimbaji wa
sifa na kwaya lazima ajue kwamba huduma hii iko moyoni mwa Mungu, maana yeye
amezungukwa na viumbe pamoja na malaika milioni nyingi wanaomwabudu mchana na
usiku
(Uf 5:7-14).
Hivyo ni vema
kufanya huduma hii kwa kicho na kujitoa kwa dhati katika unyenyekevu wote, kwa
bidii, na ustadi wa hali ya juu. Ni vibaya kufanya huduma hii kwa lengo
binafsi, ama manufaa mengine mbali na kusudi la kumwadhimisha Mungu.
1.
ANGALIZO
KWA MWANAKWAYA
Ni
jambo la muhimu kwa mwanakwaya na muimbaji wa sifa aelewe kwamba, Mungu pekee
ndiye anayestahili kupewa sifa na kuinuliwa katika huduma hiyo.
Muimbaji
ajitambue kwamba ni chombo cha sifa kwa Bwana, kwa hiyo achunge sana kipawa
hicho kisitumike kwa Bwana mwingine. Nasema
hayo baada ya kuona waimbaji wengi walioinuka na kuwa juu, hawashikiki,
hawaambiliki na kufunikwa na roho ya kiburi.
Ni
jambo la kusikitisha sana kwamba, waimbaji wazuri waliotamba katika majukwaa ya
injili kwa kipawa cha uimbaji, leo wako katika majukwaa ya shetani wakitumia
kipawa hicho hicho kumsifu shetani.
Usisahau
kwamba Mungu aliyekuita katika huduma siku moja atakutaka utoe hesabu ya
utumishi wako, (2Wak 5:10.)
Simama na huduma mtu yeyote asikunyang’anye taji yako. Ukifahamu huduma hii ni
huduma ya mbinguni, wewe ni mtu unayeheshimiwa sana na Bwana, maana Bwana
anakaa katika SIFA. Jivunie heshima hii, jiendeleze, na kutumika bila masharti
kwa utukufu wa Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni