Jumapili, 20 Agosti 2017

MAANA YA KUSIFU



Sifa maana yake ni nini?
Sifa ni neno linalotumika katika, kuinua, kuadhimisha na kutukuza kitu au mtu, kwa heshima ya maneno na matendo aliyofanya. Sifa zetu ni kwa Mungu, katika kumtukuza, kumwinua na kumwadhimisha kwa matendo yake makuu aliyoyafanya katikati yetu.

Biblia inatupa mifano mingi ya sifa kama ifuatavyo. waliokombolewa toka dhiki kuu ya mpinga kristo. Sifa ni shughuli kuu mbinguni, angalia waliokombolewa kutoka katika dhiki kuu wanavyompa sifa Mungu.
Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kandokando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana Kondoo, wakisema, ni makuu na ya ajabu matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenye Enzi: ni za haki na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa. Ni nani asiyekucha Ee Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako uu Mtakatifu: kwa maana mataifa yote yatakuja nakusujudu mbele zako kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa. (Ufunuo 15:2-4)

a.         Sifa za mfalme Daudi

(1Nyak 29.10-13) Pia Mfalme Daudi anatoa sifa za hali ya juu sana kwa Mungu Kwa hiyo Daudi akamhimidi Bwana mbele za mkutano wote, naye Daudi akasema,

“Uhimidiwe ,Ee Mfalme baba yetu milele na milele,Ee Bwana ukuu ni wako, na uweza,na utukufu, na kushinda, na Enzi, maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako, ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, U mkuu juu ya vitu vyote, Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote, na mkononi mwako mna kuwawezesha wote”. (1Nyak 29.10-13)

Sifa hizi zinatoka katika moyo wenye kuguswa na kazi za Mungu, zinazopita ufahamu wa mwanadamu. kisha mwanadamu kumwinulia Mungu Sauti yenye kujaa maneno ya mshangao wa ukuu wa Mungu! na kumimina maneno matukufu yenye kumpa sifa Mungu.

b.         Sifa za wana wa Israeli bahari ya Shamu

Mfano mwingine mzuri wa sifa, zenye maneno makuu kwa Mungu, ni sifa za wa Wana Israeli walizompa Mungu kwa muujiza mkuu alioutenda wa kukausha bahari ya Shamu. Mungu aliwavusha wana Israeli mpaka nga’mbo, na kuwaokoa na mkono wa jeshi la Farao na hatimaye kusababisha jeshi lake lote likazama baharini ukiangalia kitabu cha (Kutoka 15:1—21)

Mistari ifuatayo inasema sifa hizo. (Mstari 1-12)
 Nitamwimbia Bwana kwa maana ametukuka sana, Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu, Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo Jina lake, Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini……………………….”,

Mstari 17-18 unasema,

“Utawaingiza (ISRAELI) na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Maahali pale ulipojifanyia Ee Bwana ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, Bwana, kwa mikono yako. Bwana atatawala milele na milele.

Kusifu ni kumkubali Mungu katika uwezo wake na nguvu, adhama, ukuu, enzi na mamlaka, utukufu na heshima,
katika kutenda kwake kusikokuwa na mfano wala mipaka.

katika mambo yasiowezekana kwa kadiri ya asili yake ya Uungu ilivyo, na hivyo kuleta utoshelevu na kuridhika kwa ufahamu wetu, na kumpa sifa na kumwinua, kumheshimu na kumtambua alivyo wa thamani. Mungu wetu ni mkuu na wa kutisha na alivyo mwema na wa kupendeza mzuri pasipo mfano.

Kusifu ni kumkubali Mungu bila shaka yoyote, juu ya tabia zake kwamba Mungu ni wa haki, wa rehema na huruma zake ni za milele.

-     Amejaa upendo, mwaminifu na wa kweli na habadiliki milele.
Kusifu kunaweza kutafsiriwa kwa kina cha ufahamu wa mtu anavyoguswa na ukuu wa Mungu, na akajikuta analipuka kumpa sifa Mungu kwa viwango vyake kama tunavyoona katika Zaburi.

Sifa zikitolewa na watakatifu wa kale, kufuatana na mapito yao jinsi Mungu alivyoingilia kimiujiza kuwaokoa na kuwaponya.

“BWANA kama wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, ili wewe uogopwe”.(Zaburi 130:3-4)

Kwa Mungu wetu, hii sadaka ya sifa hutolewa kwa uhiyari wa mtu bila kujali ana matatizo gani au yuko katika hali gani. Bali shauri la moyoni mwake ni kwamba ameazimia kumsifu Mungu, na kumwinua jinsi alivyo kutegemea na  anavyomfahamu Mungu ni nani na yukoje. (Matendo 16:24-34).

Huduma ya kuabudu
Kuabudu ni huduma ya hali ya juu ya mkristo, na ndio msingi wa huduma nyingine zote za kiroho. Siku zote Mungu wetu asili yake ni kuwa na uhusiano wa ndani sana na watoto wake, ambao amewanunua kwa damu yake ya thamani. 
-     Anapenda watoto wake wamtambue kuwa yeye ni Baba yao tena anataka awaguse  na kuwaliwaza

“Na sasa, kwa sababu mmezifanya kazi hizi zote asema BWANA, nami nikasema nanyi, nikiamka mapema na kunena, lakini hamkunisikia; nami nikawaita wala hamkuniitikia,” (Yeremia 7:13)”,

“Basi nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita mbona hapakuwa na mtu wa kunijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi hata nisiweze kukukomboa? Au Je! Mimi sina nguvu za kukuponya? Tazama kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wananuka kwa sababu hapana maji nao wafa kwa kiu” (Isaya 50: 2)

Angalia pia Isaya 66:12 -14.    

Anapenda tutambue wokovu wetu aliouleta ili tushirikiane naye na kumfurahia ,1Nyakati 16:4-36 Kumbukumbu 31:30,

BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama nitawaokoa watu wangu nami nitawaleta nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli. (Zekaria 8:7-8)

a.         Mungu wetu anakaa juu ya sifa.

“Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli” (zaburi 22:3)

Uhusiano wako na Mungu na mwendelezo wa mafunuo juu yake (Udhihirisho wake kwako) vimefungwa ndani ya kumwabudu yeye. Daudi alijua ukweli huu kutokana na uzoefu wa maisha yake, ndio maana akasema.

“Nafsi yangu kwa nini kuinama na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu;” (Zaburi 42:5).
Ndio maana anatoa ushauri huu kwa mwanaye mpendwa Sulemani, angalia (1Nyakati 28:9)
Na ukiangalia Biblia katika Zaburi 37:4 inasema
“Nawe utajifurahisha kwa Bwana, Naye atakupa haja za moyo wako”.
Yesu anatangaza kwa kusema hivi,
“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” Yohana 4:23
Watu watakaompenda BWANA kwa mioyo yao yote Biblia inasema:-
“Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.Tazama nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele yangu daima”. (Isaya 49:15-16).

(Isaya 66:10-12)
Ambao wataungamanishwa naye katika mapenzi ya kupendana. Bila kujali mambo yanayotuzunguka tuko katika hali gani, tunapaswa kumwabudu Mungu kwa kumpa thamani yake halisi jinsi alivyo. kwa utayari huo tutaona maajabu yake na vifungo vyetu kufunguliwa.

Soma Zaburi 139:1-18,

Atoaye dhabihu za sifa ndiye anayenitukuza Mimi, nitamwonyesha wokovu Zaburi

“Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” (Zaburi 51:17)

Sifa za namna hii hazimpiti Mungu kwa sababu popote zinapotolewa, wazee walioko mbele ya kiti cha enzi huanguka kuzipitisha zimwendee anayestahili,
“Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi wakisema. Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.”(Ufunuo 4:9-11).

Sifa za kweli, zinapatikana kwa wale waliokombolewa, (malaika wana sifa za kupangwa). Ndilo tunda pekee ambalo Mungu analifaidi toka katika moyo wa binadamu. Biblia inasema:-
“Nikasikia sauti kutoka mbingini ikisema; Andika heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam asema Roho wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao,” Ufunuo 14:13.

Mungu anawatafuta watu watakaokuwa na jukumu la kujitolea kikamilifu kumtii yeye, watu wenye shauku ya kumtafakari yeye.

“Ee Mungu wangu, nitakutafuta mapema, nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku, katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, nizione nguvu zako na utukufu wako, maana fadhili zako ni njema kuliko uhai, midomo yangu itakusifu. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai,………..”(Zaburi 63: 1-8).
(Zaburi 108: 1-4) , Zaburi 48:9-10.
Watu watakaojihusisha kwa kuwajibika wa kumtanguliza katika kila jambo na ya kuwa yeye ndiye kiini cha yote. Sio washiriki au wachangiaji.

Zaburi 50:23,
“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; (1Petro 2:9)

Ezekieli 28:11-15 hii ndiyo asili yake. Anajifanyia yote haya kwa sababu zake mwenyewe. (kwa ajili yake mwenyewe).

“Tazama nitawaokoa watu wangu nami nitawaleta nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli na katika haki”. Zakaria 8:7-8.

Wokovu hudai sifa,
“Baada ya hayo nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa na lugha. Wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi. Na mbele ya mwanakondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na mwanakondoo. Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, (Ufunuo 15:3-4)

Wimbo unaimbwa na watu waliouthibitisha wokovu wa Mungu (wanamtambua Mungu na kazi zake au jinsi alivyo).


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni