Ufunguo
mkuu katika eneo hili ni shauku, au kiu ya kumsifu Mungu,
“Kama ayala aionevyo shauku mito
ya maji, vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu wangu. Nafsi yangu inamwonea
kiu Mungu, Mungu aliye hai, lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi
yangu yamekuwa chakula change mchana na usiku, pindi wanaponiambia mchana kutwa
yuko wapi Mungu wako?” (Zaburi 42:1- 3)
Inapatikana?
”Nafsi yangu kwa nini kuinama na
kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, aliye afya
ya uso wangu, na Mungu wangu.
Nafsi yangu imeinama ndani yangu
kwa hiyo nitakukumbuka, toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha
Mizari.
Kilindi chapiga kelele kilindi
kwa sauti ya maboromoko ya maji yako, gharika zako zote na mawimbi yako yote
yamepita juu yangu.
Mchana Bwana ataagiza fadhili
zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, naam maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.
Nitamwambia Mungu, mwamba wangu,
kwa nini umenisahau? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?”
Watesi wangu hunitukana mithili
ya kuniponda mifupa yangu pindi wanaponiambia mchana kutwa Yuko wapi Mungu
wako?
Nafsi yangu, kwa nini kuinama,
na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; kwa maana nitakuja kumsifu, aliye
afya ya uso wangu na Mungu wangu. (Zaburi 42:5-11)
Kwenye
nafsi Zaburi 63:1-11;66: 1-7, Mithali 16:3, Marko 12:30 kusifu kunaweza kuwa;-
a.
Kusifu kwa kutumia sauti,
-
Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana
Zaburi Zaburi 145:21.
-
Maana fadhili zako ni njema kuliko
uhai, midomo yangu itakusifu (Zaburi 63:3
-
Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi
yote, imbeni utukufu wa jina lake. (Zaburi 66: 1-2)
-
Mpigieni Bwana vigelegele. (Zaburi
33:1a)
b.
Kusifu kwa vitendo.
-
Enyi watu wote mpigieni makofi. (Zaburi
47:1a)
-
Msifuni kwa mvumo wa baragumu,
-
msifuni kwa kinanda na kinubi
-
msifuni kwa matari na kucheza
-
msifuni kwa zeze na filimbi,
-
msifuni kwa matoazi yaliayo,
-
msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
(Zaburi 150:3-5)
-
Kwa jina lako nitainua mikono yangu.
(Zaburi 63:4)
“Ndivyo Israeli wote
walivyopandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa sauti ya
tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga kwa sauti kuu kwa vinanda
na vinubi.
Hata ikawa, sanduku la agano la
Bwana lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani,
akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia, akamdharau moyoni mwake”.
MATENDO MBALIMBALI YA KUABUDU
-Kushukuru kwa midomo yetu (kuimba au
kusema kwa midomo yetu.
-
Kutenda mema kwa kushirikiana.
-
Kuanguka mbele za BWANA ili
kunyenyekea.
-
Kupiga vyombo mbalimbali,
-
Shangwe na upigaji wa vyombo
-
Kuinua mikono.
-
Kupiga magoti mbele za Bwana
-
Kucheza kwa nguvu zote
-
Kwa kucheza.
-
Muziki na kucheza.
-
Makofi.
-
Kelele za shangwe
-
Kufanya mapenzi ya BWANA
-
Kwa kutoa matoleo (zaka)
Ukimya na mengine
mengi. Kutoa kwa moyo wa ukunjufu, upandacho ndicho utakachovuna. Acheni mjue ya kuwa mimi ni Mungu, nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika
nchi.
Ili uabudu
lazima uwe na sababu.
1.
Mungu ni nani.
2.
Mungu amefanya nini.
3.
Kiini cha kuabudu (chanzo) Roho
wa Mungu au neno la Mungu.
4.
Mwitikio (matokeo) lazima kuwe
na udhihirisho udhihirisho huleta kusherehekea.
5.
Matokeo uwepo wa Mungu
unaachiliwa (dhihirika) nguvu za Mungu zinaachilia.
6.
Ni lazima iwe kitu unachokifanya
sio unachofanyiwa.
7.
Ikiwa hivyo hakuna atakayetoka
bila kuguswa maana amejihudhurisha mbele za Bwana binafsi.
8.
Tunafanya hivyo kwa kushangaa jinsi
alivyotuumba na anavyotutendea.
9.
Mungu anatafuta watu
watakaofungulia (SHEKINA) utukufu na nguvu zake ili zitiririke, Yeye ni kama
ngombe anaelia kwa kujaa maziwa akamuliwe.
10.
Zaburi 139:1-18 kwa
kujipendekeza kwake Zaburi 139:21-22 tukisema Baba nakupenda sina Baba mwingine
aliye mzuri kama wewe, baba uwe mfano mzuri, ili picha nzuri iwe.
11.
Naye atakwambia nakupenda
mwanangu hata bila kikomo (Zaburi 45:1-7, 17).
12.
Ndio maana shetani anapiga vita
ushirika huu. Isaya 49: 15-16,
MATOKEO
YA KUABUDU.
-
Zakaria aliguswa. Luka 1: 18-20
“Zakaria akamwambia malaika,
nitajuaje Neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku
nyingi. Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli nisimamaye mbele za
Mungu, mimi nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. Na tazama!
Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu
hukuyasadiki maneno yangu nayo yatatimizwa kwa wakati wake.”
Sifa na kuabudu katika roho na
kweli. Angalia katika kitabu cha 1nyakati 16:1-36. Azimia kuthamini (kuabudu) utaona
milango imefunguka Marko 16: 1-8
Kuna nguvu za ajabu sana angalia
katika kitabu cha Matendo 16:25-34 utaona nguvu iliyowatokea Paulo na Sila hadi
misingi ya gereza ikatikisika. Kuna pendo la ajabu, uponyaji,
wokovu, Luka 7:36-50 mwanamke Malaya aliuona upendo wa ajabu wa Yesu akampaka
mafuta yenye marashi. Kuna utukufu wa Mungu (nguvu, fahari
yake, uweza wake, uzuri wake n.k) Ufunuo 7:9-12.
Kuna utakaso, utakatifu Isaya 6:1-7.
Kuna kumfahamu Mungu 2Nyakati 20:14-30 Mungu hupata fahari yake (utashi wake)
Ezekieli 28:11-15
KUABUDU.
Katika kamusi ya kiyunani LATREIA kumtolea Mungu (sadaka)
Warumi 12:1, Waebrania 9:6 Kumtumikia kwa hiari kama mtumishi AU PROSKYREA ni
kujinyenyekesha kwa kujitoa,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni