Ibada ni kumshangaa Mungu. Kwa ufahamu tulio nao na akili
ya kibinadamu tuliyo nayo hatuwezi kumwelewa Mungu kikamilifu tukamfahamu.
Isaya 55:8-9:,
“Maana mawazo yangu si mawazo yenu,
wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo
juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na
mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”
Mungu ni mkuu kuliko uwezo wa ufahamu wa mwanadamu na yuko juu sana kuliko mawazo ya mwanadamu na yuko juu sana kuliko njia za mwanadamu
kwahiyo hatuwezi kumfahamu vyema. Hivyo basi siku zote
tutakapokusanyika pamoja au mtu akiwa peke yake kumwabudu na kukutana naye
atamshangaa (tutamshangaa).
Hutaweza kukaa mbele za Mungu ukimwabudu katika Roho na
Kweli ikawa jambo la kawaida maana Mungu huyo ni Mfalme Mkuu lazima utamshangaa Mfalme
huyo. Utukufu wake utakushangaza na kutamani kumwangalia.
Wafalme wa dunia japokuwa ni wanadamu, raia wao hutetemeka
na kuwaheshimu wanapojitokeza mbele na kila mtu hutamani kumwona na kumshangaa,
na kukusanyika mahali pamoja ili wamsikilize Mfalme wao. Mungu ni Mfalme wa
ajabu anayejihudhurisha kati ya watu wake wanapomfanyia ibada kwa kumwabudu na
kuwashangaza waabuduo ambapo na wao wanazama katika mshangao. Zab. 47:7, 66:3,
68:35, 71:16, 89:7
Ibada inayokubalika
Si kila Ibada inayofanywa na mwanadamu ni halali na
kukubalika na Mungu, hapana. Mungu ni Mungu wa utaratibu na mipango mikamilifu.
Mungu amesema wazi ni ibada ipi anaikubali na kuipokea
akaisikiliza. Lakini kwa kuwa ulimwengu ni mpana na wenye tofauti za watu walio
na itikadi tofauti na ibada za walimwengu pia ni tofauti.
Mungu wa kweli ni mmoja na njia ni moja ya kumfikia
ambayo ni Yesu. Yohana 14:1-6, ITim 2:15.
Ni katika Yesu ambaye ni mpatanishi wetu na Mungu na
ambaye ni kweli, njia na uzima tutasikilizwa na kukubaliwa,
Yesu anasema mtu yeyote hawezi kwenda kwa Mungu isipokuwa
kwa njia yake, hakuna njia ya mkato kwenda kwa Mungu, bali ni kwa njia ya Yesu
tu. Kwa hiyo ibada lazima iwe,
a. Ibada katika Roho na Kweli yenye kumtambua Yesu kuwa
kiini na mlengwa wa Ibada hiyo Mdo 4:11-12 Waef 2:4-8
b) Si ibada ya mdomoni wala makusanyiko ya kidini na taratibu za kibinadamu zilizobuniwa kwa umahiri na wala si mapokeo ya mila na desturi za watu. Mdo17:22-27
c) Ibada ambayo haimchanganyi Mungu aliyejifunua katika maandiko na miungu mingine, japokuwa miungu hiyo inaabudiwa na mamilioni ya watu pamoja na vitu vilivyotukuzwa kiasi cha kukubalika kuwa Mungu. Zab 115:4-8
Sanamu zao ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya
wanadmu. Zina vinywa lakini havisemi, zina macho lakini haioni. Zina masikio
lakini hazisikii, zina pua lakini hazisikii harufu. Mikono lakini hazishiki,
miguu lakini haziendi, wala hazitoi sauti kwa koo zake. Wazifanyao watafanana nao,
kila mmoja anayezitumainia.
Sasa ili tujiridhishe na ibada ya kweli inayokubaliwa na
Mungu hebu tuangalie ibada ya mbinguni ilivyo, na jinsi viumbe wa mbinguni
wanavyomwabudu Mungu.
IBADA KUU MBINGUNI Ufunuo 5:6-14
Biblia inafunua ibada kuu inayoendelea
mbinguni ambayo washiriki wa ibada hiyo ni wenye uhai wanne na wazee ishirini
na nne,
-
Wenye vinubi na vitasa vya dhahabu vyenye maombi ya watakatifu, wakiwa
mbele za kiti cha enzi cha Mungu.
-
Viumbe hawa wapo hapo kufanya ibada maalum ili kumwabudu na kumpa sifa
Mwanakondoo,
-
wanafanya hivyo kwa kuimba wimbo
mpya wenye sifa kwa Mwanakondoo kisha malaika wengi, elfu kumi mara elfu kumi,
elfu mara elfu, ambao wamekizunguka kiti cha enzi wanajiunga katika SIFA hizo.
Uf 4.8-11
-
Hapa ndipo ibada hii kuu inaanzia, ambapo wenye uhai wanne wasiopumzika
mchana na usiku wanamsifu Mwanakondoo wakisema Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu
na kusababisha wazee ishirini na nne kuanguka chini na kumsujudia aliye Hai milele
na milele,
-
huku wakivua taji zao na kuzitupa mbele ya kiti cha Enzi, wakisema,
Umestahili wewe Mungu kupokea utukufu na heshima na uweza kwakuwa ndiwe
uliyeviumba vitu vyote kwa sababu ya mapenzi yako vilikuweko navyo vimeumbwa.
Kisha kwa sauti ya pamoja wanasema: Anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu, na Baraka Mwanakondoo aketiye kwenye kiti cha enzi.
Kisha kwa sauti ya pamoja wanasema: Anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu, na Baraka Mwanakondoo aketiye kwenye kiti cha enzi.
Maneno haya saba ni sifa kuu kwa Yesu ambaye ni Mwanakondoo wa Mungu.
Hatimaye baada ya ngurumo hizo za sauti ya sifa, kila
kiumbe kilichoko mbinguni, duniani, na baharini vikamsifu Mwanakondoo,
- na wote wakaanguka wakamsujudia Mwanakondoo. Sifa hii ikatikisa
ulimwengu,
- ulimwengu mzima ukamwabudu Mwanakondoo, Ibada hii haifanywi kwa mtume,
nabii, malaika ,miungu wala kwa mwanadamu bali Ibada hii inamlenga Yesu
Mwanakondoo.
- Ibada inayofanywa kwa mtu mwingine mbali na Yesu siyo Ibada ya kweli na
Mungu haisikilizi.
- Inasikitisha kuona Ibada za mamilioni ya watu hazisikilizwi na Mungu kwa
kuwa zinafanywa nje ya kumwabudu Yesu.
- Katika Zaburi 98:1-9 na 96:1-8 Mfalme Daudi anatoa mwaliko wa kumwabudu
Bwana kwa wimbo mpya kwa sababu Bwana Ametenda mambo ya ajabu,
- Daudi anasema, “Inueni sauti, imbeni kwa furaha,
- Nayo mito ipige makofi, na kulibariki jina lake,
- Na kutangaza wokovu wake,
- Kwa kuwa Bwana ni mkuu na mwenye kusifiwa sana.
Wito huu ni wito wakumwabudu BWANA peke yake.
Paulo naye anatia mkazo wa kumwabudu Mungu kwa kutoa mwongozo jinsi ya kufanya ibada katika roho ya uimbaji anasema
Paulo naye anatia mkazo wa kumwabudu Mungu kwa kutoa mwongozo jinsi ya kufanya ibada katika roho ya uimbaji anasema
“Neno la Kristo likae kwa wingi mioyoni
mwenu (ndani yenu) katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na
nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkimwimbia Mungu kwa Neema mioyoni mwenu.
Mkisemazana kwa zaburi na tenzi, na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na
kumshangilia Mungu mioyoni mwenu, nakumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo
yote katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo” (Kol
3:16-17),
Ef 5:19-20.
- Ibada ya kweli ni ile inayomlenga Yesu na si vinginevyo.
- Unaweza kuona jinsi mwanadamu anavyotoa muda wake, nguvu na mali katika
ibada hewa kwa viumbe na sanamu, badala ya kumfanyia Mungu ibada katika Kristo
Yesu,
- wito huu ungali na nguvu ile ile kwetu kumgeukia Mungu na kujiunga na
viumbe hawa wa mbinguni kumfanyia ibada sahihi Mwanakondoo.
- Mungu ni mtakatifu na wa haki hana kigeugeu na habadiliki, ni mwadilifu.
- Hawezi kuweka njia tofauti tofauti za kumwabudu kwa kila mtu.
- Hiyo ingekuwa sawa na wasafiri wawili waendao mji mmoja lakini kwa njia
tofauti zinazoweza kuwafikisha pale waendapo,
- hilo haliwezekani kwa Mungu maana ni Mtakatifu, kwa utakatifu huo, Mungu
ameweka njia moja ya kumwabudu ambayo ni Yesu Kristo.
IBADA NA UIMBAJI
“Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Mwimbieni BWANA, nchi yote.” (Zaburi 96.1)
“Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa
kuume wake mwenyewe, mkono wake mtakatifu umetenda wokovu.” (Zaburi 98:1)
Mungu anapenda uimbaji na anapenda kuimbiwa wimbo mpya kama tuonavyoona katika zaburi hizi,
- Kwa asili yake yeye ni mpya kila siku hajawahi kuzeeka wala kuchakaa,
- basi kwa asili hiyo hupenda vitu vipya, ni muhimu kuwa na nyimbo mpya na
pambio mpya katika ibada zetu.
- Ibada inayofanywa katika Roho na Kweli haiwezi kuendeshwa bila ya
kumwimbia Mungu nyimbo za sifa na za kumwabudu.
- Huu ndio utaratibu na mfumo wa ibada ya kiroho, kuanzia mbinguni mbele
ya kiti cha enzi na katika Agano la kale na Agano jipya mpaka leo.
- Asilimia sabini na tano ya shuguli za kanisa ni kuabudu,
- na asilimia tisini ya kuabudu ni uimbaji yaani kuimba. Nyimbo
zinazoimbwa ziimbwe katika Roho na akili pia,
- zikielekezwa kwa Mungu, zikikoleza maombi na sala zetu,
- zikiibua sifa za dhati toka moyoni nakunyosha misisimiko ya nafsi,
fikra, mwili isipotoke kwenda nje ya ibada ya kweli,
- kwa hiyo nyimbo zisiimbwe kwa lengo la burudani, bali ziimbwe kwa lengo
la kumsifu Mungu, kumshangilia, kumshukuru, kufariji,
kutia moyo, kumkaribisha Mungu, kusaidiana, kuonyana nakujengana na kuachilia neema ya Mungu
iwafunike wanaomwabudu mahali hapo.
Matokeo ya Ibada kama hii ni makubwa,
2Nyakati 5:11-14.
“Wakamfanyia Bwana ibada kuu, Bwana
akaijaza nyumba utukufu, makuhani wakashindwa kufanya kazi zao maana Bwana
ameshuka katikati yao na kuwabariki”.
Ibada inayoendeshwa bila uimbaji ni ibada bubu na haitaleta matokeo
mazuri kwa waabuduo.Kwa kuwa Mungu ni mpenzi wa uimbaji ndani ya ibada zetu, hivyo ni muhimu
mno kuimba kwa sauti zilizopangiliwa vizuri ili tumbariki.
UIMBAJI NDANI YA IBADA
Ni vigumu kutenganisha uimbaji na ibada, uimbaji umetawala matendo ya mwanadamu kwa asilimia kubwa, kiasi kwamba uimbaji ni lugha inayomuwezesha mtu kujieleza alivyo,
- ni kama chakula cha lishe chenye virutubisho vya aina zote kwa afya ya
mwanadamu.
Uimbaji unagusa maeneo yote ya utu wa mtu na mahitaji ya
mwanadamu, kiroho na kimwili. Uimbaji ni chakula kilicho bora kabisa kukidhi
matamanio ya mtu mzima.
- Mtu akiwa na huzuni, msiba, ataimba ili afarijike na kujiliwaza au
ataimba ili aomboleze,
Katika sherehe umetawala, dhifa, mikutano ya aina zote ya
kiroho na ile ya kisiasa, matambiko, kazi, hata katika vita, matangazo ya
biashara, vyombo vya habari, matukio yote haya hutanguliwa na uimbaji na
kumaliziwa na uimbaji.
- Uimbaji huleta uponyaji wa Roho na mwili na huondoa mkandamizo na msongo
wa mawazo.
- Hii ndiyo nguvu iliyomo katika uimbaji. Ni vema basi kila mmoja wetu
akaelewa uimbaji ni nini,
- na unafanyikaje ili aweze kutumia katika kumwabudu Mungu wakati wa
ibada.
- Si jambo jema kuimba ovyo bila mpangilio ama bila kujua nakuelewa.
NYIMBO NA
AINA YA IBADA
Kila ibada ni muhimu na ina malengo yake na madhumuni, ama
makusudi ya kufanya ibada hiyo. Kwa hiyo ni lazima kila ibada ipewe nafasi
katika nyimbo zinazoimbwa katika ibada hiyo.
- Iwapo nyimbo zinazoimbwa haziendani na lengo, kusudi au madhumuni ya
ibada, basi ibada hiyo imevurugika na watu watashindwa kuabudu kuelekea lengo
la ibada hiyo.
- Mwisho watu watachanganyikiwa na kuwa watazamaji na kuwaondoa kabisa
katika ibada inayoendelea hapo Ingawa kimwili watakuepo.
Si vema kuimba wimbo wa maombolezo katika ibada ya arusi
au wimbo wa pasaka katika ibada ya krismasi ama wimbo wa uinjilisti katika
ibada ya meza ya Bwana.
- IBADA si jambo la mzaha bali ni tendo la kumuabudu MUNGU,
- Kwa hiyo ni lazima ufanyike upangaji na uchambuzi makini wa nyimbo zipi
ziimbwe katika ibada ipi ili kukidhi hitaji la ibada husika
Ufuatao ni mchakato wa aina ya ibada.
Ibada ya kuabudu ziimbwe nyimbo za kuabudu,
Ibada ya kuabudu ziimbwe nyimbo za kuabudu,
- Ibada ya SIFA, Ibada ya uinjilisti, Ibada ya maombi na kujitoa, Maisha
ya Kikristo kwa ujumla wake.
Imbisha nyimbo zinazoendana na ibada hizo.
Nyimbo za Matukio. Hakikisha unaimba nyimbo zinzokwenda na matukio hayo.
Nyimbo za Matukio. Hakikisha unaimba nyimbo zinzokwenda na matukio hayo.
Meza ya Bwana, Krismas, Pasaka, Arusi, Maziko na Maomboleza, Siku kuu,
Mwaka mpya, Watoto, Mwaliko wa mtu kwa Yesu, Nyimbo za taarifa au ushuhuda wa
matendo makuu ya Mungu, Utakaso na Kutia moyo na IMANI, Ujasiri, Mashambulizi
kwa shetani au Vita ya kiroho, Roho Mtakatifu na nyimbo zenye ujumbe maalum kwa
matukio maalum kama vile, uzinduzi wa nyumba ya IBADA, au jambo lolote
linalogusa kanisa au jamii.
Ni muhimu
kuimba nyimbo zinazogusa ujumbe wa matukio hayo. Huu ni mwongozo wa jinsi ya
kuendesha ibada na uimbaji utakaoleta Baraka na kutufikisha katika kusudi la
ibada husika.
Uimbaji ni somo pana
lenye kuwa na mielekeo tofauti tofauti kulingana na matumizi ya mtu anavyotaka.
- Ingawa kanuni za muziki (uimbaji) ni zilezile kwa kila
mwelekeo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni