Kusudi la Mungu
kumuumba mwanadamu ni ushirikiano
(fellowship) Biblia inasema,
“Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu
;wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na wanyama, nan chi yote
pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa
mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”
(Mwanzo 1:26-27).
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi
ya uhai; mtu akawa nafsi hai”. (Mwanzo 2:7).
“Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha
akatwaa ubavu wake mmoja, akaufunika na nyama mahali pake”. (Mwanzo 2:21)
“Kisha wakasikia sauti ya Bwana mungu akitembea bustanini wakati wajua
kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu
asiwaone BWANA Mungu akamwita Adamu Akamwambia, uko wapi? Akasema Nalisikia sauti yako bustanini,
nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha (Mwanzo 3:8-10)
Katika ushirikiano
huo ndiko tunapata chimbuko la ibada ya mwanadamu. Mungu hawezi kufanya
Ushirika na mwanadamu katika asili ya mwili moja kwa moja, hii ni kwa sababu
Mungu yeye ni ROHO. kwa hiyo Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake. Na mfano
huo upo katika ROHO. Ushirika wetu na Mungu uko katika ROHO, na kwaRoho
tunafanana na Mungu.
“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani
pumzi yenye uhai, mtu akawa nafsi hai”. (Mwanzo 2:7.)
Mwili ni nini?
-
Mwili
ni nyumba au makao, ya roho.
Roho ni nini?
-
Roho
ni pumzi ya Mungu yenye uhai,
Ili kwa huyo Roho
Mungu ajidhihirishe kwa ulimwengu katika ufahamu wetu. Yaani mwili ambao ni
mavumbi. Katika msingi huo kusudi la Mungu kutuumba linatimia. Yapo makusudi
makuu mawili ambayo ni:-
1.
Kumtumikia
2.
Kumwabudu.
Mwanadamu awaye yote
asiyefanya mambo hayo mawili amekosea lengo na kusudi la asili ya kuumbwa
kwake.
Katika mambo haya
mawili, wajibu wa kwanza ni kuabudu, yule unayemwabudu hatimaye unamtumikia na
kuyakubali matakwa yake kwa kumtumikia.
Wajibu wa kwanza wa
Adamu ulikuwa ni kuabudu na siyo kuhubiri ama kufanya huduma zingine, Mungu
alikuja katika ibada wakati wa jua kupunga jioni ili kufanya ushirika nao.
-
Kuhubiri
neno ni matokeo ya anguko la Adamu kumuasi Mungu na kuacha wajibu wake wa ibada
na Mungu.
-
Msingi
mkuu wa mahusiano ni Ibada. (Mwanzo 3:8) unasema wakasikia sauti ya
Mungu akitembea bustanini.
Hii inaonyesha
kwamba Adamu alikuwa na ushirika na Mungu kiasi cha kuzijua hatua za Mungu
alivyotembea ikiwa ni ushahidi wakutosha kwamba walikua na ushirika mzuri.
Asili
ya kuabudu
Kuabudu asili yake ni mbinguni, Kuabudu
kulikuwepo kabla ya Adamu kuumbwa. Maana walikuwepo viumbe kabla ya Adamu huko
mbinguni waliomwabudu Mungu.
Ibada ina asili katika Mungu mwenyewe, Uungu
una asili ya kuabudiwa kwa hiyo chanzo cha ibada ni Mungu.
“Ulikuwa
wapi nipoweka misingi ya nchi? Haya! Sema kama ukiwa na ufahamu. Ni nani
aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nanialiyenyoosha kamba juu yake?
Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la
pembeni. Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu
walipopiga kelele kwa furaha?”. (Ayubu 38:4-7)
Pia ukiangalia kitabu cha Zaburi 148:2-14.
Unaweza kuaona malaika wanamwabudu na kumsifu Mungu. Mstari wa 5 zaburi
148 unaonyesha agizo la Mungu akiagiza viumbe vyote kumwabudu na kumsifu kutoka
mbinguni mpaka duniani, kuanzia viumbe vyenye uhai na visivyo na uhai kama
ifuatavyo:-
Malaika na
jeshi lake, Jua , mwezi na nyota zote, Mbingu na maji ya mbingu. Mstari wa 5
viumbe visivyoonekana Nchi yaani uumbaji wake wa dunia Samaki wa baharini Moto,
mvua, theluji na mvuke, upepo na dhoruba Milima, na miti , wanyama wa porini na
wakufugwa, Wadudu na ndege wa angani. Wafalme na watu wakubwa kwa wadogo wazee
na watoto
Hawa wote wanaamuriwa kulisifu Jina la
Bwana, Jina Pekee lililotukuka lenye adhama juu ya mbingu na nchi. Hii ni amri
ya milele ambayo haitapita.
Midundo ya shangwe za malaika na mirindimo
ya ibada hiyo ikaijaza mbingu wakati Mungu alipoumba ulimwengu. Malaika
waliimba na kushangilia kazi ya uumbaji.
Imekuwa ni shauku ya Mungu kutaka
ushirikiano huu wa ibada na viumbe vyake alivyoviumba, tangu hapo na mpaka
milele katika mbingu mpya na nchi mpya, ambayo ni masikani yake pamoja na
mwanadamu.
“Nikasikia
sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema Tazama, maskani ya Mungu
ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani pamoja nao.” (Ufunuo. 21:3)
Jambo hili linafunuliwa na kufafanuliwa kwa ufasaha na Yesu alipomwambia mwanamke msamaria pale kisimani
“Lakini
saa inakuja nayo sasa ipo ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika Roho
na kweli” kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu, Mungu ni Roho nao
wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na Kweli”. (Yohana 4:23-24).
Mungu
anamtafuta mtu atakayemwabudu
Kwa nini?
Kwa sababu anataka
ushirika na mwanadamu Ili aufurahiye Upendo wa mwanadamu aliyemuumba kwa mfano
wake na kutimiza kusudi lake la ushirika. Kuabudu katika Roho na Kweli huo
ndiyo ushirika ambao Mungu anautafuta kwa mwanadamu. Kwa kuwa Jawabu la moyo wa
Mwanadamu, ni kuwa na ushirika ambao unamgusa Mungu, na kumtukuza Mungu kwa
roho yake yote.
Kumfurahia Mungu pasipokuwa na kitu kingine
zaidi ya Mungu moyoni mwake. Kufanya uamuzi wa kumpenda Mungu kuwa ni jambo la
milele. Ibada siyo kitu cha muda mfupi bali ni shughuli inayo endelea milele na
milele kati ya mwanadamu na Mungu. Biblia inamnukuu Mariamu akisema,
“Mariamu akasema moyo wangu
wamuadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, mwokozi wangu; Kwa kuwa
ameutazama Unyonge wa mjakazi wake, kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote
wataniita mbarikiwa”. (Luka 1:46-47)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni