Kabla
sijawekewa mikono kuwa kiongozi wa waimbaji wa jiji la Tanga, kiongozi wangu
mwenyekiti wa chama cha muziki wa injili kanda ya kaskazini, alinichukua ili
kunitambulisha kwa baadhi ya maaskofu wa kipentekoste waliokuwepo Tanga.
Nakumbuka askofu mmoja alitueleza sababu za kutuunga mkono ni kwamba waimbaji
wanaojitegemea wengi wao wamekuwa na maadili mabou sana na wanashindwa
kuwashauri kwa sababu hakuna chombo kinachoweza kuwaunganisha kati yao na
viongozi wa dini, akatueleza jinsi ambavyo yeye mwenyewe alivyomdhamini
mwimbaji mmoja dola 3,000$ ambazo huyo mwimbaji alitaka zitumwe kwenye akaunti
yake, pesa akapokea na kwenye mkutano huo hakwenda na pesa hizo hakurudisha. Hali
hii ilimtia aibu sana kwa wageni wake ambao walikuwa sio waswahili.
Huu
ni mmoja kati ya mambo mengi ya aibu ambayo yanafanywa na wale wanaojiita
waimbaji wakubwa. Lakini katika hotuba yangu baada ya kuapishwa, niligusia
kidogo hili jambo kwa kuwaeleza wakuu wadini, kwamba hawa waimbaji wengi wao
vipaji vyao huanza kuonekana kanisa, na huwa tunawakuza na kuvilea vipaji vyao toka
kanisani, wanakuwa chini ya malezi ya idara za vijana baadae wanaingia kwenye
kwaya ambazo zipo kanisani. Wakiwa hapo wanakuwa chini ya uangalizi wa jicho
kali la mchungaji, wazee wa kanisa na walimu wa kwaya, katika ngazi hii kuna
mafunzo wanayopewa katika kukuza kipaji chake na maadili ya kanisa.
Shida
inakuwa ni pale anapotaka kwenda mbele zaidi yaani nje ya uwigo wa kanisa kama
jengo la pahali. Mara nyingi wachungaji huwa hawakubali wakiamini kwamba ni matunda
yao na ni lazima atumike kanisani hapo. Matokeo yake mwimbaji huyo huanza
kufanya ukaidi na kuondoka wakati mwingine bila ya kuaga. Matokeo yake anakosa baraka
na kuyumba kimwelekeo. Katika eneo hili ni wachungaji wachache sana wanaoagana
na waimbaji wao kwa kuwapa mkono wa baraka. Na hii ni muhimu pia kukumbuka
kwamba waimbaji wetu nao wana ndoto zao katika maisha ya uimbaji na lazima
ziheshimiwe katika kupunguza migogoro na kuua vipaji ya waimbaji, hilo ni
lazima wachungaji walitambue na ikiwezekana wapate nafasi ya kuongea na
waimbaji mmoja mmoja, ili kujua maono yake, na ni lazima kumsaidia kwa hali na
mali katika kufikia lengo lake, kama na yeye anavyojitoa katika kusukuma huduma
ya kanisa, hapo ndipo litakuwa chimbuko la kuwa na waimbaji wakubwa ambao bado
wana mahusiano mazuri na Mungu na wachungaji wao pia. Kanisa ni zaidi ya jengo
la mahali fulani ni lazima tutengeneze uwigo mpana kuhakikisha kwamba vipaji
vilivyoko kanisa vinaweza kuhudumia taifa na dunia kwa ujumla.
wakati huu tunaona
waimbaji waliokuwa ni mtumishi wa Mungu kwa huduma ya uimbaji katika sehemu
mbalimbali ndani na nje ya nchi. Huduma zao zilipata mpenyo mkubwa sana sehemu
mbalimbali mpaka wakaota pembe,
Kutokana na umahili
wao katika uimbaji walipata umaarufu ndani na nje ya Kanisa na kupelekea
viongozi wa kisiasa kuwaomba wawasaidie kwenye kampeni za kisiasa za vyama vyao
ili wawasaidie kushinda katika chaguzi mbalimbali za uwakilishi wa kisiasa. Nao
kwa tamaa walikubaliana na ombi hilo, bila kuwaambia viongozi hao wa kisiasa
kwamba wito watu ni kumwimbia Mungu tu na si vinginevyo. Ni kweli kila mtu
anatamani kupata pesa lakini Yesu anauliza Itakufaa nini ukiupata ulimwengu
wote?
maana sijajua kwa
undani mafanikio waliyoyapata kwa kuwa waimbaji wa nyimbo za kampeni za siasa kuliko
faida watakazopata kwa kumtumikia Mungu wao.
-
Mwimbaji
ni chombo kitakatifu cha Bwana, Mfalme Daudi alifahamu vyema jambo hilo
akachukua hatua ya kuwaweka WAIMBAJI WAKFU MADHABAHUNI pa Bwana kuonesha kwamba
wametengwa rasmi kwa huduma hiyo.
Ikumbukwe kwamba
Mungu hakukubaliana na mfalme Belishaza alipovitumia vyombo vitakatifu
vilivyotwaliwa kutoka Hekalu la Yerusalemu na baba yake Nebukadreza.
Hebu
angalia Mungu alivyochukizwa na jambo hilo.
“Na wewe
mwanawe, Ee Belishaza hukujinyenyekeza moyo wako, ijapokuwa ulijua hayo yote,
Bali umejiinua juu ya Bwana wa Mbingu nao wamevileta vyombo vya nyumba yake
mbele yako na wewe, na wakuu wako na wake zako na masuria wako mmevinywea nawe
umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba na ya chuma na mti na ya
mawe wasioona wala kusikia wala kujua neno lolote, na Mungu yule ambae pumzi
yako ii mkononi mwake, na njia zako zote ni zake hukumtukuza. Ndipo kile
kitangaa cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake na maandiko haya
yameandikwa, MENE MENE,TEKELI NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii,
MENE. Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha, TEKELI, Umepimwa katika
mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka, PERESI Ufalme wako umegawanyika nao
wamepewa Waamedi na Waajemi. Danieli
5.22—28
-
Haya
ni maonyo makali kwa mtu ambaye anakitumia chombo cha Mungu kinyume na matumizi
yake, hivyo hivyo Mungu hayuko tayari kuona vipawa alivyotupa vinatumika hovyo,
mbali na kusudi la huduma hii.
Maana mafuta
tuliopewa sio ya kisiasa wala ya kuburudisha watu ni kwa ajili ya Mungu. Ni muhimu
kuwa na unyenyekevu na heshima na kujiepusha na kitu chochote kinachokuondoa
katika utumishi wako kwa Mungu. Linda sana ulicho nacho
na wito wako mtu asikunyanganye.
- Mambo yaliyompata
mfalme Belishaza baada ya kuvitumia vyombo vya Bwana vibaya katika msitari wa
30 unasema, usiku huo huo akafa.
Hii ni hatari
inayomkabili mtumishi yeyote anayekiuka kutumia vibaya kipawa na karama
aliopewa na Bwana. Kwa hiyo kila mwimbaji wa sifa ambaye amepakwa mafuta na
Mungu ni chombo cha Bwana hapaswi kutumia kipawa chake nje ya huduma ya Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni