JUKWAA LA KIKRISTO NA KIJAMII AMBALO LINATOA FURSA KWA JAMII KUJADILI NA KUELIMISHANA JUU YA MAADILI NA MAISHA KWA UJUMLA
Alhamisi, 10 Januari 2013
Alhamisi, 3 Januari 2013
MIKUTANO YA INJILI KWA SIKU HIZI HAINA MATUNDA WALA HAMASA KAMA ZAMANI
Wakati naanza kupata akili ya kuelewa
kuhusu mambo ya imani yangu,nilikuta mikutano ya injili ikiwa ndio njia kuu ya
kuwaleta watu kwa Yesu. Lakini waliotutangulia katika imani hii wanatusimulia
kuwa Mwishoni mwa Miaka ya 1970 na Mwishoni mwa Miaka ya 1980 bado njia kuu
iliyokuwa ikitumika kuwaleta watu kwa Yesu ilikuwa ni Mikutano Ya Injili ya
hadhara ambapo watu wengi walimpokea Yesu kupitia mikutano hiyo. Wahubiri wa
kizazi hicho, Mzee Emmanuel Lazaro, Mzee Moses Kulola, Mzee Ayoub Mgweno na Wengineo
walikuwa na kazi kubwa ya kueneza
neno la Mungu na asilimia kubwa ya watu waliookoka katika zama hizo waliokoka
kwenye mikutano ya wahubiri hawa.
Miaka
ya 80, ikaanzishwa huduma inaitwa “The Big November Crusades” chini ya Mzee
Lutembeka na Mzee Kisondo. Mikutano hii ilikuwa na nguvu sana miaka
hiyo. Nakumbuka ilifanyika katika maeneo ya Mnazi Mmoja na Jangwani kwa wakazi
wa Dar, Wagonjwa walikuwa wanaletwa kutoka Muhimbili na walikuwa wakirudi
wamepona.
George Gichana kutoka Kenya ali maarufu “GG” nakumbuka enzi hizo pamoja na Mzee Roy Daman walikuwa wakija Dar-es-Salaam, kila shughuli ilikuwa inasimama na kila mtu akisubiria “The Big November” ili kuona miujiza lakini pia kuona kwaya kuu zilizokuwa zikitamba enzi hizo, Mtoni Lutheran, na wimbo wao wa Lulu, Chini ya Mwl. George Victory Singers na Wimbo wao wa Mchakamchaka, Chini ya Mwalimu Mwalubalile na Revival Singers na wimbo wao uko wapi, chini ya Mwalimu Mackenzie
George Gichana kutoka Kenya ali maarufu “GG” nakumbuka enzi hizo pamoja na Mzee Roy Daman walikuwa wakija Dar-es-Salaam, kila shughuli ilikuwa inasimama na kila mtu akisubiria “The Big November” ili kuona miujiza lakini pia kuona kwaya kuu zilizokuwa zikitamba enzi hizo, Mtoni Lutheran, na wimbo wao wa Lulu, Chini ya Mwl. George Victory Singers na Wimbo wao wa Mchakamchaka, Chini ya Mwalimu Mwalubalile na Revival Singers na wimbo wao uko wapi, chini ya Mwalimu Mackenzie
Miaka ya 90 na Mpaka sasa nimeona kama hii mikutano ya injili ya hadhara imekuwa kama haina matokeo mazuri ama makubwa kuliko katika kizazi kile cha Mwishoni mwa , 2010 niliamua kutembelea katika baadhi ya mikutano ya injili iliyokuwa inafanyika Tanga, nilitembelea pale kanisa la TAG Mwembe wa Yesu pale Kisha nikashiriki mkutano wa injili tuliouandaa kanisani kwetu KLPT Majani mapana , kinanisukuma kutazama mikutano hii ni kuamini pia kuona mikutano hii inavyoendeshwa, mwitikio wa waumini wenyewe kwenye mikutano hii, na pia mpango mkakati wa kuwatunza hawa wanaoamua kumpa Yesu Maisha yao.
Mbali
na mikutano ya injili, pia nimekuwa nikiwasikiliza watumishi wa Mungu wale
wanaohubiri kwenye vituo vya mabasi, pale Posta kuna rafiki yangu huwa
anahubiri, mwenge kituoni kuna mpendwa huwa anahubiri, stendi ya mkoa kuwa
wanaohubiri na kuna wengine wanakusanya sadaka kabisaaaa kwa ajili ya kupata
maomb meona kwenye kuangalia kwangu nikama ifuatavyo
|
Mbali na mikutano ya injili, pia nimekuwa
nikiwasikiliza watumishi wa Mungu wale wanaohubiri kwenye vituo vya mabasi,
pale Posta kuna rafiki yangu huwa anahubiri, mwenge kituoni kuna mpendwa huwa
anahubiri, stendi ya mkoa kuwa wanaohubiri na kuna wengine wanakusanya sadaka
kabisaaaa kwa ajili ya kupata maomb meona kwenye kuangalia kwangu nikama ifuatavyo.
Mikutano
Ya Injili.
1. Waumini wengi
(wenyeji) wa mikutano wanapatika siku za Jumamosi na Jumapili, siku za kawaida
mikutano huwa na watu wachache na kukosa hamasa ya watu.
2. Mkutano Mingi
inayowekwa kwenye viwanja vya makanisa huwa na washirika zaidi kuliko wenye
dhambi katika kuhudhuria. Ikifika saa ya kukata shauri muhubiri hutumia muda
mrefu wa kuamua kuimba pambiodent:-
3. Wahudumu wengi wa Mikutano wanakuwa hawako well trained kwa ajili ya hiyo kazi, Mfn. Namna ya kukaribisha watu, namna ya kubeba wagonjwa, namna ya kukemea mapepo na pia namna ya kusimama katika kuombea watu, kila Muhubiri ana style yake ya wahudumu kusimama.
3. Wahudumu wengi wa Mikutano wanakuwa hawako well trained kwa ajili ya hiyo kazi, Mfn. Namna ya kukaribisha watu, namna ya kubeba wagonjwa, namna ya kukemea mapepo na pia namna ya kusimama katika kuombea watu, kila Muhubiri ana style yake ya wahudumu kusimama.
4. Mikutano
inayofanyikia kama Jangwani, Biafra,
Kawe au katika viwanja vya wazi ni ngumu kuwapata wale kondoo wapya kutokana na
umbali wa viwanja na makazi ya watu pia.
Wengi
wanaohudhuria mikutano hii ni watu wa hali ya chini, wale wasiokuwa na kazi,
wafanyakazi wa ndani na wanafunzi. Watu ambao ni wafanyakazi wengi wanatingwa
na shughuli nyingi za kutafuta kipato.
6. Waongofu wapya
wengi huwa hawadumu, unaweza kuta waliookoka jumla ni 100, wanaoendelea mpaka
sasa ni wawili.
7. Wahubiri
wengi wa nje wanaongea vizuri lakini ile nguvu ya udhihirisho ni ndogo sana, yaani wagonjwa kupona wengi ni
wale wa tumbo, kichwa na maumivu tu. Ila vipofu, vilema na viziwi bado imekuwa
utata kuwapata waliofunguka
8. Ile tabia ya
watu kukata shauri na kuhamia kwenye “dhehebu” wenye kuhost mkutano imepitwa na
wakati. Wengi wanaokoka na kubaki huko huko waliko ambapo imepelekea kupunguza
morale ya “kuwavunia” wengine na makanisa kuamua ku-opt “Semina Za Ndani”.
9. Waumini wengi
si wepesi wa kwenda nao zaidi ya wenyeweji kujazana wenyewe uwanjani
1. Wengi wa wahubiri hawa hawajaribu kuonesha upendo wa Mungu, ila kuwatuhumu abiria na kuwaogopesha na siku ya mwisho. Nimewahi kumsikia Muhubiri pale Posta akiongelea mavazi na wakati mwingine hata Dowans katikati ya Mahubiri.
2. Muhubiri
anapokanza kuhubiri wanaomsikia ni wengine, mpaka ikifik kata shauri ni mara
chache mtu akakaa kituo cha basi zaidi ya nusu saa kusikiliza mahubiri kuliko
mtu kusikiliza sauti ya konda anapoita abiria
3. Mpango Mzima
wa sadaka sijajua kama wale watumishi wanakumbuka kutoa
kikumi, maana akichukua kila basi per day ana make inaweza kumfanya akaona ile
ndo ajira yake ya kila siku, kuhubiri na kukusanya sadaka
Lazima nikiri
kuwa kuhubiri katika hadhara pia ina faida sana kwenye maisha ya waamini, inakujenga
na kukupa ujasiri. Kwa sisi ambao tumekuwa bega kwa bega na wazee wetu kwenye
mikutano ya injili, lazima tukiri mikutano ya injili ya nje inakujenga kimwili
na kiroho na kisaikolojia pia.
Kwa changamoto
nilizozitaja kwangu naona mikutano ya injili inahitaji kutazamwa upya kwa maana
ya namna tunavyotumia rasilimali tulizonazo, muda, fedha, watu na kila
kilichopo. Semina za Kiroho ambazo zimekuwa zikijenga hata wapendwa nimebaini
zimekuwa natokeo makubwa kuliko mikutano ambayo Kanisa linatumia gharama kubwa
kuliko matunda ya mikutano hii. Nadhani ipo haja ya sisi wadau kusaidia kuliona
hili na pia kushauri pale tunapopaswa kushauri
Wasalaam,
Samuel Sasali
Papaa
Kweli mikutano ya nje imepungua na hii mi naona ni kusababishwa na mazingira nikimaanisha mikutano mingi ya zamani ilibase kwenye injili haswa na watu kuokoa, kwasasa mingiimeamiakwenye semina na semina nyingi kufanya na wenyehudumaya kialimu na mitume,pia naona imeamia kwenye majengo ya ndani nikimaanisha makanisa na mahema.
Kingine naona ni
wale wainjilisti wa zamani waliokuwakwenye majukwaa na viwanjani hawakuandaa
watu kipindi walichokuwepo ili ikitokea hawapo au kipindi chao cha kazi
kumalizika basi gurudumu litabebwa na hao walioachiwa.
Finally
kwangumimi naona ni swala la season kwa sasa Mungu anatumia huduma ya kialimu sana kuwafundisha
watu neno badala ya forces za wainjilisti.
Lakiniinabidi
kukutana na wainjilisti hawa wa zamani ni rahisikupata views zao katikahili na
pia tazama vijana wa sasa nguvu na upako wakiinjilisti umepoa sana kwao
wote wanabase kwenye miracles,unabii na n.k
Kwa mimi nahisî
msukumo wa kuendelea na mikutano pia umepungua.
yawezekana ni :
1. kuongezeka
waumini makanisa ya wale waliokuwa wanafanya mikutano hii ya injili ya nje.
2. mafundisho ya
kiinjilisti yamepungua na hivyo kukosekana kwa wainjilisti wapya kuendeleza
kazi.
3. Maendeleo ya
kiteknolojia yanayofanya matumizi ya redio na tv kuwa makubwa na hivyo
kuwafikia watu wengi zaidi kama vile afanyavyo mzee wa upako, mama
lwakatare na kakobe. Hata miziki ya injili inavyozidi kuimarika na kuwafikia
watu wengi kubadilisha maisha yao.
Jumamosi, 29 Desemba 2012
HARUSI YA ELIZABETH NA YOHANA ALLEN
| Aliyependeza namna hii ni mwimbaji wa Tanya Prise & Worship Team ya jijini Tanga akisema neno siku ya harusi yake |
| Mheshimiwa Yohana Allen akilishwa kiapo na Mchungaji Georgre Nywage siku ya alipofunga ndoa na Eliza. |
| wanaoonekana kwa mbele ni wapambe wa harusi wakiwasindikiza maharusi kutoka nje ya kanisa. |
| Bwana na bibi wakitoka nje ya ukumbi wa kanisa. |
| Haya jamani mbona mnapiga picha kabla hatujaweka pozi |
| haya sasa piga picha yako haraka tusije tukapoteza pozi. |
| mh! na sisi pia tusikose kumbukumbu hii muhimu sana. |
| huku Tanga huwa tunaenda kupiga picha baharini, sijui wenzetu msio na bahari mnapiga picha wapi? |
| Duh! mama Cesi naye hakuwa nyuma alishika nafasi yake sawasawa. |
| Mmh hili pozi hapa wala sio mahali pake. |
| Hapo ni sisi hao tulipendeza si kidogo. |
| Hapo naona bibi harusi alikuwa keshachoka na hekaheka za harusi. inabidi na mimi niishie hapa kwa kuwatakia maisha mema heri na baraka tele. |
Jumanne, 4 Desemba 2012
ALIYEFARIKI ATOKEA GHAFLA.
![]() |
| Hizi picha haihusiani na tukio linalolipotiwa ila imewekwa hapa kwa sababu ya mahusiano na vitendo vya kishetani |
“Bado
huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba za usiku wa kuamkia leo (jana)
alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili atoke, akapiga sana mlango...wakamfanya
dawa ndipo akajaribu kutulia hadi sasa bado yumo ndani na usiku alipewa chakula
akala na asubuhi amepewa uji” alisema mtu wa karibu wa mwanamke huyo.
MAMIA ya wakazi wa Kijiji cha
Lamadi, wilayani Busega mkoani Simiyu, juzi walifurika katika Kitongoji cha
Mabulugu kumshuhudia mwanamke Ngulima Kilinga (30), aliyedaiwa kufufuka huku
mwili wake ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mkula iliyopo mkoani humo.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake.
Habari zaidi kutoka katika kitongoji hicho zinasema mwanamke
huyo bado amefungiwa ndani ya nyumba yake akifanyiwa dawa za kienyeji ili
arudie katika hali yake ya kawaida, kwani kwa sasa anaonekana kama zezeta.
“Bado huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba za usiku wa
kuamkia leo (jana) alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili atoke, akapiga sana
mlango...wakamfanya dawa ndipo akajaribu kutulia hadi sasa bado yumo ndani na
usiku alipewa chakula akala na asubuhi amepewa uji” alisema mtu wa karibu wa
mwanamke huyo.
Pia inadaiwa kuwa tayari mganga wa kienyeji amekwisha kuja kwa
ajili ya kutengeneza mwanamke huyo ili aweze kurudia hali yake na kwamba
amewashukuru wananzengo hao kwa kuweka maiti kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo,
kwamba hiyo ndiyo njia sahihi.
Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi alithibitisha
tukio hilo, lakini akabainisha hayo ni mambo ya imani za kishirikina.
Kamanda Msangi alisema polisi walipelekwa katika eneo la tukio
kuhakikisha usalama wa wananchi na hadi saa 9:00 jioni jana, maiti ya mwanamke
huyo iliyokuwa hospitali ilikuwa haijazikwa.
Jana umati mkubwa wa watu ulifurika katika Hospitali ya Mkula
kulikohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo kuushuhudia.
Ndugu wa mwanamke huyo akiwamo mumewe
Ngitu Masisanga na mama yake mzazi, Mwashi Myeya walisema Ngulima aliugua
ghafla juzi baada ya kukwama na mfupa wa samaki wakati akila chakula nyumbani
kwake.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.
Alisema cha ajabu ni kwamba wakati wamelala nyumbani kwa
marehemu sambamba na waombolezaji wengine, saa 7 usiku marehemu alitokea akiwa
uchi.
Walisema marehemu huyo alimwita mtoto wake ampatie nguop na
kuchukua albamu ambapo aliangalia picha.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mbali na kutazama picha
hizo na kutaka kupewa nguo zake, pia marehemu huyo alichukua tochi iliyokuwa
ikiwaka na kuizima.
Mama mzazi wa marehemu alisema, “Kabla ya kukimbia nje tulimzuia
yeye kutoka nje tulimfungia mlango na sisi ndio tukakimbilia nje, licha ya
kufunga mlango alikuwa akiupiga kwa nguvu ufunguke ila na yeye aweze kutoka
nje, kuna mtu amefanya dawa za kienyeji ndio tunasubiri majibu.”
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI
HALI HALISI YA KANISA LA TANZANIA
![]() |
| Moses Kulola |
INGAWA takwimu zilizotokana na Sensa ya taifa zinaonyesha kuwa Ukristo kwa ujumla wake unakua kwa kasi ndogo, ikiwa ni chini ya asilimia 35 ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni 40, takwimu hizi haziendani na hali halisi inayoonekana hata kwa macho ya kawaida.
Pamoja na kuwa na msimamo mkali wa kuzingatia maadili na msimamo wa kuwapiga marufuku wanawake wasiofunika vichwa na waliovaa nywele za bandia kuingia kanisani humo, bado kanisa hilo limebaki kuwa miongoni mwa makanisa ya uamusho na lenye matawi sehemu nyingi za Tanzania.
Ngurumo ya Upako
Huduma hii iko chini ya mwanzilishi wake Mheshimiwa Nabii GeorDavie , na makao makuu yake yako nje kidogo ya jiji la Arusha, katika bara bara ya kuelekea Dodoma. Huduma ya Ngurumo ni miongoni mwa vituo vinavyokusanya idadi kubwa sana ya waumini kwa wakati mmoja.
Inaaminika kuwa zaidi ya watu 12,000 hukusanyika pamoja kumtukuza Mungu kila Jumapili na tayari inapanuka kwa kasi ya kutisha ikiwa na matawi katika mikoa mbali mbali ya Tanzania na nje.
Mafundisho ya Huduma hii yamelenga zaidi kwenye ukombozi na uponyaji. Kuna shuhuda nyingi za watu waliokuwa wamekaribia kufa walipoamini walipona na wako hai wakimtukuza Mungu wa mbinguni.
Pia ni mahali ambapo kuna shuhuda za kurejeshwa kwa watu waliokuwa wamechukuliwa misukule na wale ambao wanateswa na ibilisi.
Makala zake kwenye magazeti na vipindi vya Televisheni vimeelezwa kuwavuta watu wengi katika ufalme wa Mungu.
Living Water Center
Huduma hii kama ilivyo kwa huduma nilizotaja hapo juu, haikuanza siku nyingi sana, lakini pia imekuwa na uamusho mkubwa na tayari ina matawi kadhaa nchini ikiwa ni pamoja na jiji la Arusha na Mwanza.
Mikutano ya hadhara, iliyoongozwa na Kiongozi wake Mtume Onesmo Ndegi, katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha, pamoja na uwezo wake mkubwa wa kutumia njia za kisasa za mawasiliano kuhubiri, inaelezwa kuwa kivutio na uamsho mkubwa.
Muundo wa kanisa lake ambalo limejengwa kwa makuti kitaalamu na kuonekana kama kiota cha kitalii ni miongoni mwa mambo ya kipekee katika huduma hii ambayo huvutia watu wengi.
Kanisa hili ni pia linasisitiza mafundisho ya utakatifu, lakini likijikita zaidi kwenye ukombozi na mafanikio ya mwili na roho.
Kiongozi wake ni miongoni mwa wachungaji wa mwanzo kutumia televisheni kupeleka habari njema za injili ulimwenguni kote.
Mikocheni B. Assemblis of God
HILI ni kanisa la kipekee ambalo linaongozwa na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mchungaji Dk. Getrude Rwekatare, ambaye licha ya kuwa Mchungaji mwenye uwezo mkubwa wa kuhubiri, ni mwanamke ambaye mafanikio ya kimwili pia ni mfano wa mahubiri yake.
Pamoja na kuhubiri injili kwa muda mrefu tangu alipokuwa kiongozi wa wanawake kwenye kanisa la Tanzania Assemblies of God, Ilala, jijini Dar es Salaam, ni mwanaharakati wa haki za akina mama na watoto na mfanyabishara anayemiliki mtandao mpana wa shule za St. Mary’s International, Kenton, na kituo maarufu cha Redio kiitwacho Praise Power, ambacho kinatoa nafasi sawa kwa wahubiri wengine kuhubiri Injili kupitia vipindi vyake mbali mbali.
Kanisa lake pamoja na mambo mengine linahubiri Injili yenye msisitizo wa mafanikio. Pia anaendesha vituo kadhaa vya watoto yatima na tayari kanisa lake limefungua matawi katika jiji la Dar es Salaam.
Kanisa hili lilianzia kwenye majengo ya shule ya msingi Mikocheni mika tisa hivi iliyopita, lakini sasa limekua na kuweza kujenga jengo la ibada lenye uwezo wa kukusanya zaidi ya waumini 8,000 kwa ibada moja ya Jumapili.
Shule alipoanzia kanisa mchungaji huyo ameipa zawadi ya kuijengea majengo ya kisasa ya kufundishia na huu umebaki kuwa mfano wa jinsi kanisa linavyojali jamii.
HAKUNA LISILOWEZEKANA
Hii ni huduma ya Kiroho iliyoanzishwa na Askofu Sylvester Gamanywa, mmoja wa maaskofu vijana na shupavu mwenye jicho la kuona mbali na kushiriki katika harakati kadhaa.
Mara nyingi ni mtu wa kuingia katika kila jambo na kutumia mamlaka yake kutafuta ufumbuzi. Katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa miongoni mwa wahubiri wa kwanza kujitoa katika kuendesha kampeni ya kuhimiza amani na kuliombea taifa.
Akitumia kituo chake cha Redio ya Kikristo itwayo Wapo F.M, Askofu Gamanywa, aliongoza pia harakati za kuhimiza watu kubadili tabia ili kujikinga na gonjwa la UKIMWI, hapo serikali ikatambua mchango wake na akateuliwa kuwa mmoja wa Makamishina wa Tume ya kupambana na ugonjwa huo Tanzania.
Ingawa alikuwa mhubiri kwa muda mrefu, akimiliki pia Gazeti la Kikristo la Msema Kweli, Askofu Gamanywa alipata mafanikio makubwa katika miaka sita tu iliyopita ambapo uamsho mkubwa umedhihirika katika huduma yake.
Baada ya huduma yake kupanuka alifungua kituo cha miujiza na uponyaji huko Mbezi Beach, jijini kiitwacho BCIC, ambacho mbali ya kuwa ni kituo cha maombi na uponyaji kwa damu ya Yesu, ni mahali ambapo semina na masomo maalumu yanayolenga kuibadili tabia ya Watanzania hufanyika kwa mafanikio makubwa.
Kwa wakati huu Askofu Gamanywa, anaendesha kampeni iliyolenga kuokoa kizazi kijacho kwa kupambana na uharibifu wa maadili kwa vijana.
Calvary Assemblies of God (CAG)
Huduma hii ni moja kati ya huduma za kiroho hapa nchini, Ilianza miaka 15 iliyopita na imekuwa ikikua kwa kasi na kupata mafanikio makubwa sana ya kiroho. Mbeba maono wa huduma hii ni Mtume Dustun Maboya, ambaye yeye ndiye kiongozi mkuu wa huduma.
Hudumu hii chini ya Mtume Dustun Maboya, ilianzia mjini Morogoro mwaka 1994 huku ikiwa na waumini 200 tu, katika ibada moja na hadi kufikia sasa inakadiriwa kufikia zaidi ya waumini 5000 kwa ibada.
Msimamo na mkazo wa mafundisho ya huduma hii ni kuhubiri mafundisho ya wokovu na mafanikio ya kiroho na kimwili pia.
Mtume Dustan Maboya aliokoka mwaka 1977 na mwaka 1978 mara baada ya kupata wito wa kumtumikia Mungu alijiunga na chuo cha biblia cha mkoani Arusha na kuhitimu mwaka 1981. Baada ya hapo aliacha kazi na kuamua kumtumikia Mungu kwa kuanzisha huduma hii.
Kwa sasa Calvary Assemblies of God, chini ya Mtume Dunstun Maboya, imeenea nchi nzima na kufikisha idadi ya makanisa 460 kwa nchi nzima mjini na vijijini.
Silioam Ministry International
Huduma hii, ikiwa chini ya mbeba maono Mtume N.Z.Munuo, ilianza miaka mitano iliyopita na kuwa na makao yake makuu jijini Dar es salaam.
Huduma hii ambayo inaonyesha kukua kwa kasi sana, ilianza ikiwa na washirika watatu tu waliokuwa wakifanya ibada nyumbani kwa Mtume Munuo.
Kwa sasa huduma hii imetanuka nchi nzima na kuwa na matawi kila Wilaya na inakadiriwa ibada moja inakusanya waumini zaidi ya 3000 kwa jumapili.
Msimamo na mkazo wa mafundisho ya huduma hii ni kuvunja misingi mibovu ya shetani ndani ya watu na kisha kuwajenga watu hao katika nguzo nne, NENO,IMANI, UTAKATIFU na UTII.
Mtume Munuo, alipata wito wa kumtumikia Mungu na kumjengea nyumba ya ibada ambayo watu watamwabudu katika roho na kweli akiwa mwajiriwa wa Shirika la Umeme nchini na baadaye aliamua kuacha kazi na kwenda kumtumikia Mungu. Hiyo ilikuwa mwaka 2003.
Kwa sasa huduma hii tayari imekwishaanzisha chuo cha Biblia kinachoitwa Siloam Bible College, ambacho kimetumika kuwaandaa watumishi mbalimbali wa Mungu kutoka katika makanisa na huduma mbalimbali hapa nchini. Kwa sasa hudumu hii ya Siloam hapa nchini, chini ya mtume N.Munuo, ina jumla ya makanisa yapatayo 70 nchini.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


















