JUKWAA LA KIKRISTO NA KIJAMII AMBALO LINATOA FURSA KWA JAMII KUJADILI NA KUELIMISHANA JUU YA MAADILI NA MAISHA KWA UJUMLA
Jumanne, 4 Desemba 2012
ALIYEFARIKI ATOKEA GHAFLA.
![]() |
| Hizi picha haihusiani na tukio linalolipotiwa ila imewekwa hapa kwa sababu ya mahusiano na vitendo vya kishetani |
“Bado
huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba za usiku wa kuamkia leo (jana)
alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili atoke, akapiga sana mlango...wakamfanya
dawa ndipo akajaribu kutulia hadi sasa bado yumo ndani na usiku alipewa chakula
akala na asubuhi amepewa uji” alisema mtu wa karibu wa mwanamke huyo.
MAMIA ya wakazi wa Kijiji cha
Lamadi, wilayani Busega mkoani Simiyu, juzi walifurika katika Kitongoji cha
Mabulugu kumshuhudia mwanamke Ngulima Kilinga (30), aliyedaiwa kufufuka huku
mwili wake ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mkula iliyopo mkoani humo.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake.
Habari zaidi kutoka katika kitongoji hicho zinasema mwanamke
huyo bado amefungiwa ndani ya nyumba yake akifanyiwa dawa za kienyeji ili
arudie katika hali yake ya kawaida, kwani kwa sasa anaonekana kama zezeta.
“Bado huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba za usiku wa
kuamkia leo (jana) alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili atoke, akapiga sana
mlango...wakamfanya dawa ndipo akajaribu kutulia hadi sasa bado yumo ndani na
usiku alipewa chakula akala na asubuhi amepewa uji” alisema mtu wa karibu wa
mwanamke huyo.
Pia inadaiwa kuwa tayari mganga wa kienyeji amekwisha kuja kwa
ajili ya kutengeneza mwanamke huyo ili aweze kurudia hali yake na kwamba
amewashukuru wananzengo hao kwa kuweka maiti kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo,
kwamba hiyo ndiyo njia sahihi.
Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi alithibitisha
tukio hilo, lakini akabainisha hayo ni mambo ya imani za kishirikina.
Kamanda Msangi alisema polisi walipelekwa katika eneo la tukio
kuhakikisha usalama wa wananchi na hadi saa 9:00 jioni jana, maiti ya mwanamke
huyo iliyokuwa hospitali ilikuwa haijazikwa.
Jana umati mkubwa wa watu ulifurika katika Hospitali ya Mkula
kulikohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo kuushuhudia.
Ndugu wa mwanamke huyo akiwamo mumewe
Ngitu Masisanga na mama yake mzazi, Mwashi Myeya walisema Ngulima aliugua
ghafla juzi baada ya kukwama na mfupa wa samaki wakati akila chakula nyumbani
kwake.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.
Alisema cha ajabu ni kwamba wakati wamelala nyumbani kwa
marehemu sambamba na waombolezaji wengine, saa 7 usiku marehemu alitokea akiwa
uchi.
Walisema marehemu huyo alimwita mtoto wake ampatie nguop na
kuchukua albamu ambapo aliangalia picha.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mbali na kutazama picha
hizo na kutaka kupewa nguo zake, pia marehemu huyo alichukua tochi iliyokuwa
ikiwaka na kuizima.
Mama mzazi wa marehemu alisema, “Kabla ya kukimbia nje tulimzuia
yeye kutoka nje tulimfungia mlango na sisi ndio tukakimbilia nje, licha ya
kufunga mlango alikuwa akiupiga kwa nguvu ufunguke ila na yeye aweze kutoka
nje, kuna mtu amefanya dawa za kienyeji ndio tunasubiri majibu.”
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI
HALI HALISI YA KANISA LA TANZANIA
![]() |
| Moses Kulola |
INGAWA takwimu zilizotokana na Sensa ya taifa zinaonyesha kuwa Ukristo kwa ujumla wake unakua kwa kasi ndogo, ikiwa ni chini ya asilimia 35 ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni 40, takwimu hizi haziendani na hali halisi inayoonekana hata kwa macho ya kawaida.
Pamoja na kuwa na msimamo mkali wa kuzingatia maadili na msimamo wa kuwapiga marufuku wanawake wasiofunika vichwa na waliovaa nywele za bandia kuingia kanisani humo, bado kanisa hilo limebaki kuwa miongoni mwa makanisa ya uamusho na lenye matawi sehemu nyingi za Tanzania.
Ngurumo ya Upako
Huduma hii iko chini ya mwanzilishi wake Mheshimiwa Nabii GeorDavie , na makao makuu yake yako nje kidogo ya jiji la Arusha, katika bara bara ya kuelekea Dodoma. Huduma ya Ngurumo ni miongoni mwa vituo vinavyokusanya idadi kubwa sana ya waumini kwa wakati mmoja.
Inaaminika kuwa zaidi ya watu 12,000 hukusanyika pamoja kumtukuza Mungu kila Jumapili na tayari inapanuka kwa kasi ya kutisha ikiwa na matawi katika mikoa mbali mbali ya Tanzania na nje.
Mafundisho ya Huduma hii yamelenga zaidi kwenye ukombozi na uponyaji. Kuna shuhuda nyingi za watu waliokuwa wamekaribia kufa walipoamini walipona na wako hai wakimtukuza Mungu wa mbinguni.
Pia ni mahali ambapo kuna shuhuda za kurejeshwa kwa watu waliokuwa wamechukuliwa misukule na wale ambao wanateswa na ibilisi.
Makala zake kwenye magazeti na vipindi vya Televisheni vimeelezwa kuwavuta watu wengi katika ufalme wa Mungu.
Living Water Center
Huduma hii kama ilivyo kwa huduma nilizotaja hapo juu, haikuanza siku nyingi sana, lakini pia imekuwa na uamusho mkubwa na tayari ina matawi kadhaa nchini ikiwa ni pamoja na jiji la Arusha na Mwanza.
Mikutano ya hadhara, iliyoongozwa na Kiongozi wake Mtume Onesmo Ndegi, katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha, pamoja na uwezo wake mkubwa wa kutumia njia za kisasa za mawasiliano kuhubiri, inaelezwa kuwa kivutio na uamsho mkubwa.
Muundo wa kanisa lake ambalo limejengwa kwa makuti kitaalamu na kuonekana kama kiota cha kitalii ni miongoni mwa mambo ya kipekee katika huduma hii ambayo huvutia watu wengi.
Kanisa hili ni pia linasisitiza mafundisho ya utakatifu, lakini likijikita zaidi kwenye ukombozi na mafanikio ya mwili na roho.
Kiongozi wake ni miongoni mwa wachungaji wa mwanzo kutumia televisheni kupeleka habari njema za injili ulimwenguni kote.
Mikocheni B. Assemblis of God
HILI ni kanisa la kipekee ambalo linaongozwa na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mchungaji Dk. Getrude Rwekatare, ambaye licha ya kuwa Mchungaji mwenye uwezo mkubwa wa kuhubiri, ni mwanamke ambaye mafanikio ya kimwili pia ni mfano wa mahubiri yake.
Pamoja na kuhubiri injili kwa muda mrefu tangu alipokuwa kiongozi wa wanawake kwenye kanisa la Tanzania Assemblies of God, Ilala, jijini Dar es Salaam, ni mwanaharakati wa haki za akina mama na watoto na mfanyabishara anayemiliki mtandao mpana wa shule za St. Mary’s International, Kenton, na kituo maarufu cha Redio kiitwacho Praise Power, ambacho kinatoa nafasi sawa kwa wahubiri wengine kuhubiri Injili kupitia vipindi vyake mbali mbali.
Kanisa lake pamoja na mambo mengine linahubiri Injili yenye msisitizo wa mafanikio. Pia anaendesha vituo kadhaa vya watoto yatima na tayari kanisa lake limefungua matawi katika jiji la Dar es Salaam.
Kanisa hili lilianzia kwenye majengo ya shule ya msingi Mikocheni mika tisa hivi iliyopita, lakini sasa limekua na kuweza kujenga jengo la ibada lenye uwezo wa kukusanya zaidi ya waumini 8,000 kwa ibada moja ya Jumapili.
Shule alipoanzia kanisa mchungaji huyo ameipa zawadi ya kuijengea majengo ya kisasa ya kufundishia na huu umebaki kuwa mfano wa jinsi kanisa linavyojali jamii.
HAKUNA LISILOWEZEKANA
Hii ni huduma ya Kiroho iliyoanzishwa na Askofu Sylvester Gamanywa, mmoja wa maaskofu vijana na shupavu mwenye jicho la kuona mbali na kushiriki katika harakati kadhaa.
Mara nyingi ni mtu wa kuingia katika kila jambo na kutumia mamlaka yake kutafuta ufumbuzi. Katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa miongoni mwa wahubiri wa kwanza kujitoa katika kuendesha kampeni ya kuhimiza amani na kuliombea taifa.
Akitumia kituo chake cha Redio ya Kikristo itwayo Wapo F.M, Askofu Gamanywa, aliongoza pia harakati za kuhimiza watu kubadili tabia ili kujikinga na gonjwa la UKIMWI, hapo serikali ikatambua mchango wake na akateuliwa kuwa mmoja wa Makamishina wa Tume ya kupambana na ugonjwa huo Tanzania.
Ingawa alikuwa mhubiri kwa muda mrefu, akimiliki pia Gazeti la Kikristo la Msema Kweli, Askofu Gamanywa alipata mafanikio makubwa katika miaka sita tu iliyopita ambapo uamsho mkubwa umedhihirika katika huduma yake.
Baada ya huduma yake kupanuka alifungua kituo cha miujiza na uponyaji huko Mbezi Beach, jijini kiitwacho BCIC, ambacho mbali ya kuwa ni kituo cha maombi na uponyaji kwa damu ya Yesu, ni mahali ambapo semina na masomo maalumu yanayolenga kuibadili tabia ya Watanzania hufanyika kwa mafanikio makubwa.
Kwa wakati huu Askofu Gamanywa, anaendesha kampeni iliyolenga kuokoa kizazi kijacho kwa kupambana na uharibifu wa maadili kwa vijana.
Calvary Assemblies of God (CAG)
Huduma hii ni moja kati ya huduma za kiroho hapa nchini, Ilianza miaka 15 iliyopita na imekuwa ikikua kwa kasi na kupata mafanikio makubwa sana ya kiroho. Mbeba maono wa huduma hii ni Mtume Dustun Maboya, ambaye yeye ndiye kiongozi mkuu wa huduma.
Hudumu hii chini ya Mtume Dustun Maboya, ilianzia mjini Morogoro mwaka 1994 huku ikiwa na waumini 200 tu, katika ibada moja na hadi kufikia sasa inakadiriwa kufikia zaidi ya waumini 5000 kwa ibada.
Msimamo na mkazo wa mafundisho ya huduma hii ni kuhubiri mafundisho ya wokovu na mafanikio ya kiroho na kimwili pia.
Mtume Dustan Maboya aliokoka mwaka 1977 na mwaka 1978 mara baada ya kupata wito wa kumtumikia Mungu alijiunga na chuo cha biblia cha mkoani Arusha na kuhitimu mwaka 1981. Baada ya hapo aliacha kazi na kuamua kumtumikia Mungu kwa kuanzisha huduma hii.
Kwa sasa Calvary Assemblies of God, chini ya Mtume Dunstun Maboya, imeenea nchi nzima na kufikisha idadi ya makanisa 460 kwa nchi nzima mjini na vijijini.
Silioam Ministry International
Huduma hii, ikiwa chini ya mbeba maono Mtume N.Z.Munuo, ilianza miaka mitano iliyopita na kuwa na makao yake makuu jijini Dar es salaam.
Huduma hii ambayo inaonyesha kukua kwa kasi sana, ilianza ikiwa na washirika watatu tu waliokuwa wakifanya ibada nyumbani kwa Mtume Munuo.
Kwa sasa huduma hii imetanuka nchi nzima na kuwa na matawi kila Wilaya na inakadiriwa ibada moja inakusanya waumini zaidi ya 3000 kwa jumapili.
Msimamo na mkazo wa mafundisho ya huduma hii ni kuvunja misingi mibovu ya shetani ndani ya watu na kisha kuwajenga watu hao katika nguzo nne, NENO,IMANI, UTAKATIFU na UTII.
Mtume Munuo, alipata wito wa kumtumikia Mungu na kumjengea nyumba ya ibada ambayo watu watamwabudu katika roho na kweli akiwa mwajiriwa wa Shirika la Umeme nchini na baadaye aliamua kuacha kazi na kwenda kumtumikia Mungu. Hiyo ilikuwa mwaka 2003.
Kwa sasa huduma hii tayari imekwishaanzisha chuo cha Biblia kinachoitwa Siloam Bible College, ambacho kimetumika kuwaandaa watumishi mbalimbali wa Mungu kutoka katika makanisa na huduma mbalimbali hapa nchini. Kwa sasa hudumu hii ya Siloam hapa nchini, chini ya mtume N.Munuo, ina jumla ya makanisa yapatayo 70 nchini.
Alhamisi, 29 Novemba 2012
BOB MARLEY MHUBIRI WA AMANI NA UPENDO BILA YESU
Mcheza mpira wa miguu,
Mhubiri wa amani na upendo, Mwanamapinduzi, Mwanaharakati, Mpiganaji,
Mwanasiasa, Mwanamuziki wa Reggae na Nyota ya kwanza katika ulimwengu wa tatu
Bob Marley.
Alizaliwa akiitwa Robert Nesta Marley na mama wa Kijamaica mwenye asili ya Afrika, bi Cedella Booker na baba mwanajeshi Mwingereza aliyefariki kijana Robert akiwa bado mdogo sana akiwaacha katika umasikini mkubwa.
Bob Marley alizaliwa panapo usiku wa kuamkia Februari 6, 1945, St Anns Parish kijiji cha Nine Miles (maili tisa) huko Jamaica.
Kumbukumbu zake za utotoni na ujanani zimejaa harakati za maisha na muziki. Harakati zilizomkutanisha na kijana machachari Peter Tosh na pia Bunny Livingstone (Wailer) na hatimaye vijana wengine kama Junior Braithwaite na Beverly Kelso. Panapo mwaka 1963, Bob akiwa na wenzake waliojiita Wailing Wailers waliweza kusaini mkataba na prodyuza maarufu wakati huo Coxsone Dodd na kutoa vibao kadhaa kikiwemo 'Simmer Down' kilichowatambulisha vema katika ulimwengu wa muziki wa Jamaica.
Bob na Rita Anderson walioana mwaka 1966 baada ya Bob kurejea Jamaica akitokea Marekani ambako alikacha kwenda vitani Vietnam. Aliporudi Jamaica, Bob alikuta imani ya Kirastafari ikiwa imepamba moto kufuatia ziara ya Mfalme wa Ethiopia Haile Sellassie (Ras Tafarr Makonen) hapo mwaka 1965. Hotuba ya Sellassie ndicho kibao cha Bob kiitwacho 'War'
Kundi la Wailing Wailers halikudumu sana. Lilivunjika mwaka 1974 na Bob kuunda kundi lake maarufu zaidi katika historia ya muziki wa reggae la 'Bob Marley and the Wailers' wakafanikiwa kutoa albamu ya 'Catch A Fire' panapo mwaka 1975 ikiwa na kibao maarufu kilichopatwa kuimbwa tena na wanamuziki wengi sana cha 'No Woman No Cry'
Mwaka 1976, Bob Marley alifanikiwa kuwapatanisha mahasimu wakubwa wa kisiasa nchini Jamaica, waziri mkuu na kiongozi mkuu wa upinzani, Michael Manley na Edward Seaga. Wajamaica walimwona Bob Marley kama shujaa halisi wa taifa lao. Bob na kundi lake walishambuliwa na risasi siku tatu kabla ya tukio hilo, lakini walipona.
Mwaka huohuo wa 1976, Bob Marley na kundi lake walitoa albamu ya 'Exodus' iliyovunja rekond ya mauzo na kukaa kwenye chati ya Billboard kwa majuma 52 ikikamata namba moja.
Bob Marley alizunguka mabara yote ya ulimwengu kupiga muziki wake uliokubalika sana. Maonesho makubwa zaidi aliyafanya Uingereza, Ujerumani, New Zealand, St. Barbara, California huku pia akishiriki kama mgeni mwalikwa muhimu katika sherehe ya uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980.
Maradhi ya kansa iliyoanzia kidoleni mguuni kwake, yaliukatisha uhai wake panapo Mei 11, 1981 huko Miami Marekani akiwa angali kijana wa umri wa miaka 36. Katika kibao chake cha 'Rastaman Chant' alipata kusema, "One bright morning when my work is over, I'll fly away to Zion"
Hata hivyo aliiacha kazi yake kama mhubiri wa amani na upendo.
Serikali ya Jamaica, kwa kuutambua mchango wake, ilimtunukia nishani ya juu zaidi 'Order of Merit.'
Bob Marley aliacha watoto 12, wengi wao wanajihusisha na muziki wa reggae na hip hop.
Bob Marley atakumbukwa zaidi duniani kama balozi na shujaa halisi wa muziki wa reggae. Atakumbukwa kwa kuuweka muziki huu wenye nguvu katika ramani ya ulimwengu.
Muziki wake utaendelea kuishi vizazi na vizazi. Ni urithi muhimu sana kwa wanaoupenda muziki wake. Ama kwa hakika wanajivunia sana miaka 36 ya uhai wake.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi daima. Amina.

MKASA WA MELI YA TITANIC
Pichani, meli ya RMS Titanic ikiondoka Southampton Uingereza hapo Aprili 10, 1912
kwa meli ya Titanic kulitokana na tatizo la usukani
LONDON – Meli ya Titanic iligonga
siwa barafu (iceberg) tarehe 14 Aprili 1912 mnamo saa 5.40 usiku kutokana na
hitilafu ya usukani. Lakini ikazama kwa kasi zaidi kutokana na Afisa
mwandamizi wa meli hiyo kumwamuru nahodha aendelee na safari. Hayo
yameelezwa jana Jumatano na mwandishi wa Kiingereza alipohojiwa na shirika la
habari la Reuters.
Louise Patten, mwandishi na mjukuu
wa Afisa mwandamizi wa meli hiyo Charles Lightoller, ameamua kusema ukweli juu
ya kile kilichotokea karibia miaka 100 iliyopita. Ukweli huo ulikuwa
umefichwa kwa makusudi kwa kiasi cha miaka 100 ili kulinda heshima ya babu yake
aliyekuja kuwa shujaa wa vita kuu ya dunia.
Lightoller, afisa mkuu
aliyesalimika katika ajali ile ya kihistoria aliuficha ukweli huo alipohojiwa
mara mbili. Alihofu kuwa ukweli huo ungeifilisi kampuni iliyoitengeneza
meli hiyo na pia kuwapotezesha ajira wenzake walioajiriwa katika kampuni hiyo.
"Wangeweza kuikwepa barafu
ile kama isingekuwa kasoro kwenye usukani," Patten ameiambia Daily
Telegraph.
Mabaki ya meli ya Titanic kama
yanvyoonekana katika picha hii iliyopigwa hivi karibuni.
"Badala ya kuuelekeza usukani
wa Titanic kwa usalama kuelekea kushoto kwa siwa barafu lile, iligundulika kuwa
usukani haufanyi kazi upande huo. Aliyeushika usukani, nahodha
Robert Hitchins, alichanganyikiwa na kuuelekeza upande usio sahihi."
Patten, ameyafunua hayo ili kwenda
sambamba na utowaji wa riwaya yake mpya "Good as Gold" ambayo
ameitumia kuelezea mazungumzo ya manahodha hao. Kwa mujibu wa mazungumzo
hayo, kulikuwa na mifumo miwili tofauti ya usukani.
Jambo lililokuwa la muhimu sana,
mfumo mmoja ulikusudiwa kuuzungusha usukani kuelekea upande mmoja, na
mfumo mwingine, kinyume chake.
Kosa hilo la usukani
lilipofanyika, Patten akaongeza, "walikuwa na dakika 4 tu za
kuubadili mfumo huo. Wakati afisa mkuu William Murdoch alipoligundua kosa
la Hitchin na kujaribu kulirekebisha, alikuwa amechelewa."
Babu yake Patten hakuwa akiangalia
wakati meli ikigonga siwa barafu, lakini alikuwepo wakati wa kikao cha mwisho
cha maafisa wa meli ya Titanic kabla ya meli hiyo kuzama kabisa.
Babu yake Patten si tu alisikia
juu ya makosa hayo, bali pia amri kutoka kwa J. Bruce Ismay, mwenyekiti wa
White Star Line, kampuni iliyoitengeneza meli hiyo akimwamuru nahodha wa meli
kuendelea na safari. Tendo la kuendelea na safari lilisababisha meli
kuzama kwa kasi kubwa sana. Masaa saba tu hadi kufikia saa 2.20 asubuhi,
meli ilikuwa imezama yote.
"Kama Titanic ingesimamishwa
pale pale, isingezama kamwe kwani ingeweza kumudu kusubiri meli za uokoaji na
pasingekuwepo vifo vile.," alisema Patten.
Meli ya RMS
Titanic ilikuwa
ndiyo meli kubwa zaidi duniani wakati ikiondoka Southampton, Uingereza,
kuelekea New York katika safari yake ya kifahari zaidi melini panapo Aprili 10,
1912. Siku nne baadaye ikiwa safarini iligonga siwa barafu na kuzama.
Ajali hiyo kubwa zaidi ya meli katika historia, iligharimu maisha ya watu 1517
kati ya watu 2227 waliokuwa ndani ya meli hiyo ikijumlisha abiria na
wafanyakazi.
Nimeiandika habari hii baada ya
kuisoma kwenye mtandao wa Reuters kwa sababu moja. Nimetaka tuone tofauti
ya wenzetu wa Ulaya. Miaka 100 sasa, wao bado wanajali juu ya chanzo cha
ajali. Sisi meli ya Mv Bukoba iliyozama miaka 14 tu nyuma, nani anajali
tena kujua chanzo kilikuwa nini? Wenzetu na rekodi nzuri ya watu waliokuwemo.
Sisi wala hatujawahi kuwa na idadi kamili ya wahanga
Hebu litazame hili jedwali juu ya
rekodi za abiria wa Titanic. Sisi hadi leo hatuna idadi kamili ya wahanga
wa majanga makubwa.
category
|
waliokuwa melini
|
waliopona
|
asilimia waliopona
|
waliokufa
|
asilimia waliokufa
|
1st class
|
329
|
199
|
60.5 %
|
130
|
39.5 %
|
2nd class
|
285
|
119
|
41.8 %
|
166
|
58.2 %
|
3rd class
|
710
|
174
|
24.5 %
|
536
|
75.5 %
|
crew
|
899
|
214
|
23.8 %
|
685
|
76.2 %
|
Jumla
|
2,223
|
706
|
31.8 %
|
1,517
|
68.2 %
|
Chanzo jedwali: wikipedia
IMEWEKWA NA FA
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)

.jpg)

.jpg)

.jpg)
.jpg)