Alhamisi, 27 Aprili 2017

mamlaka ya kutumika (10)

Mamlaka Ya Kutumika
Kwa kuwa Mungu anampa mchungaji mamlaka ya kiroho na kusimamia kanisani mwake, hili halimpi haki ya kutawala kwa nguvu kundi lake. Yeye si Bwana wao – Bwana wao ni Yesu. Wao si kundi lake – ni kundi la Mungu.
Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. Na Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka (1Petro 5:2-4).
Kila mchungaji atatoa hesabu ya huduma yake siku moja, mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.
Tena, kwa habari ya fedha, mchungaji/mzee/mwangalizi asifanye kitu peke yake. Kama kuna fedha zinakusanywa kila mara au mara kwa mara kwa sababu yoyote ile, wengine katika kusanyiko wawajibike ili kusiwe na kutoaminiana kuhusu matumizi ya fedha (ona 2Wakor. 8:18-23). Hao wengine wawe kundi lililochaguliwa au kuteuliwa.
Kulipa Wazee
Maandiko yanaonyesha wazi kwamba wazee/waangalizi/wachungaji wanapaswa kulipwa, maana ni watenda kazi wa kudumu wa kanisa. Kwa habari hii, Paulo aliandika kama ifuatavyo:
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hawa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, ‘Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka.’ Na tena, ‘Mtenda kazi astahili ujira wake.’ (1Timo. 5:17, 18).
Mada iko wazi kabisa – na Paulo anatumia neno ujira. Maneno yake yasiyokuwa wazi sana kuhusu wazee watawalao vema wahesabiwe kustahili heshima maradufu yanaeleweka kirahisi wakati mantiki inapotazamwa. Katika mistari kabla ya hii, Paulo anaandika waziwazi kuhusu jukumu la kanisa kuwasaidia kifedha wajane ambao wasingepata msaada kwa njia nyingine, na anaanza kwa maneno yale yale: “Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli” (ona 1Timo. 5:3-36). Basi, katika mantiki hii, “kuheshimu” maana yake ni kuwasaidia kifedha. Wazee wanaotawala vema wahesabiwe kustahili heshima mara mbili, yaani, wapokee mara mbili ya kiasi ambacho wajane wanapewa, na hata zaidi kama wana watoto wanaowategemea.
Makanisa jengo katika dunia nzima huwategemeza kifedha wachungaji wao (hata katika mataifa maskini), lakini inaonekana makanisa mengi yanayokutania nyumbani duniani kote – hasa nchi za Magharibi – hayafanyi hivyo. Hii ni kwa sababu ya ukweli kwamba makusudi hasa ya watu wengi katika nchi za Magharibi ya kujiunga na makanisa ya nyumbani ni uasi moyoni, nao wanatafuta na wamepata Ukristo usio na masharti mengi. Wanasema walijiunga na kanisa la nyumbani kwa sababu walitaka kuepukana na kifungo cha kanisa jengo, lakini ukweli ni kwamba walitaka kuepukana na aina yoyote ya kujitoa kikamilifu kwa Kristo. Wamepata makanisa yasiyotaka watu wajitolee kifedha, makansia yenye kwenda kinyumke kabisa na kile ambacho Kristo anatazamia kwa wanafunzi Wake. Hayo, mungu wao ni fedha, na wanathibitisha hilo kwa kujilundia hazina zao duniani badala ya mbinguni. Hao si wanafunzi wa kweli wa Kristo (ona Mathayo 6:19-24; Luka 14:33). Kama Ukristo wa mtu hauathiri anachofanya na fedha zake, huyo si Mkristo kabisa.
Makanisa yanayokutania nyumbani yenye kudai kwamba ni ya KiBiblia yanapaswa kuwatunza wachungaji wao kifedha, na kuwasaidia maskini na kusaidia kazi ya utume. Kwa kutoa na katika mambo yote yakifedha, wanapaswa kuzidi sana makanisa jengo, maana wao hawana majengo ya kulipia wala watumishi wengi wa kulipa mishahara. Wanahitajika watu kumi tu ambao watatoa zaka ili kumtunza mchungaji mmoja. Watu kumi wanaotoa asilimia ishirini ya mapato yao wanaweza kumtegemeza vizuri sana mchungaji mmoja na mishenari mmoja atakayeishi kwenye kiwango kile cha mchungaji wao.
Wachungaji Hufanya Nini?
Fikiri kwamba unamwuliza mshirika wa kawaida kanisani swali hili: “Je, ni kazi ya nani kufanya yafuatayo:- kuwashuhudia watu ambao hawajaokoka? Kuishi maisha matakatifu? Kuomba? Kuonya, kushauri na kusaidia waamini wengine? Kutembelea wagonjwa? Kuweka mikono juu ya wagonjwa kwa ajili ya uponyaji? Kubeba mizigo yaw engine? Kutumia karama zake kwa ajili ya kusanyiko? Kujikana, akijitoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu? Kufanya wanafunzi na kuwabatiza, na kuwafundisha kutii amri za Kristo?”
Washirika wengi wa kanisa, bila ya kusita, wangejibu kwa kusema, “Hayo yote ni majukumu ya mchungaji.” Lakini, ni sawa?
Kulingana na Maandiko, kila aaminiye anapaswa kuwashuhudia watu ambao hawajaokoka.
Mwe tayari sikuzote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu (1Petro 3:15).
Kila aaminiye anawajibika kuishi matisha matakatifu.
Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, ‘Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu’ (1Petro 1:15, 16).
Kila mwamini anatakiwa kuomba.
Furahini sikuzote. Ombeni bila kukoma (1Wathes. 5:16, 17).
Kila aaminiye anatazamiwa kuonya, kutia moyo na kuwasaidia waamini wengine.
Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote (1Wathes. 5:14. Maneno mepesi kukazia).
Kila aaminiye anatakiwa kutembelea wagonjwa.
Nalikuwa uchi, mkanivika. Nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama. Nalikuwa kifungoni, mkanijia (Mathayo 25:36).
Majukumu Zaidi
Lakini, si hayo tu. Kila aaminiye anapaswa kuweka mikono juu ya wagonjwa na kuwaponya pia.
Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona (Marko 16:17, 18).
Kila aaminiye anapaswa kubeba mizigo ya waamini wenzake.
Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo (Wagalatia 6:2).
Kila aaminiye anatazamiwa kutumia karama zake kwa ajili ya wengine.
Basi, kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha katika kufundisha kwake; mwenye kuonya katika kuonya kwake; mwenye kukirimu kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii; mwenye kurehemu kwa furaha (Warumi 12:6-8).
Kila mwamini anapaswa kujikana mwenyewe, na kujitoa kwa ajili ya Injili.
Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, ‘Mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha’ (Marko 8:34, 35).
Tena, kila mwamini anatazamiwa kufanya watu kuwa wanafunzi, na kuwabatiza, na kuwafundisha kutii amri zote za Kristo.
Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni (Mathayo 5:19. Maneno mepesi kukazia).
Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu (Waebrania 5:12).
Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari (Mathayo 28:19, 20)
Majukumu hayo yote yametolewa kwa kila aaminiye, lakini washirika wengi wa kanisa hufikiri kwamba yametolewa kwa wachungaji tu! Pengine sababu ni kwamba wachungaji wengi pia hufikiri kwamba hayo ni majukumu yao peke yao.
Basi, Wachungaji Wanapaswa Kufanya Nini?
Kama majukumu hayo yote yametolewa kwa kila aaminiye, wachungaji basi wanatakiwa kufanya nini? Kirahisi tu ni kwamba, wao wameitwa kuwawezesha hao waaminio watakatifu kufanya mambo hayo yote (ona Waefeso 4:11, 12). Wameitwa kuwafundisha hao waaminio watakatifu kutii amri zote za Kristo (ona Mathayo 28:19, 20) kwa kuonyesha mfano pamoja na kufundisha (ona 1Timo. 3:2; 4:12, 13; 5:17; 2Timo. 2:2; 3:16 – 4:4; 1Petro 5:1-4).
Maandiko hayawezi kuwa wazi kuliko hivyo. Nafasi ya KiBiblia ya mchungaji sio kukusanya watu wengi kiasi anachoweza Jumapili asubuhi kwenye ibada kanisani. Ni “kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo” (Wakolosai 1:28). KiBiblia, wachungaji hawatekenyi masikio ya watu (2Timo. 4:3). Wanafundisha, wanaonya, wanakemea, wanakaripia, na kurekebisha, na yote hufanywa kwa msingi wa Neno la Mungu (ona 2Timo. 3:16 – 4:4).
Paulo aliorodhesha baadhi ya sifa za mtu anayetaka kusimama katika nafasi ya mchungaji, katika barua yake ya kwanza kwa Timotheo. Sifa kumi na nne kati kumi na tano zinahusu tabia yake, kuonyesha kwamba mfano wa maisha yake ndicho kitu cha muhimu zaidi sana.
Ni neno la kuainiwa [kwamba] mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kusimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibuni, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi (1Timo. 3:1-7).
Ukifananisha sifa hizi na zile ambazo mara nyingi hutolewa na makanisa yanapotafuta mchungaji mpya utagundua tatizo la msingi katika makanisa mengi. Wao hutafuta meneja wa kusimamia wafanyakazi/mtu wa kustarehesha watu/mtoa hotuba fupi/msimamizi/mwanasaikolojia/mkurugenzi wa shughuli na mipango/bingwa wa kuchangisha fedha/rafiki wa kila mtu/farasi au punda wa kazi. Wanataka mtu “wa kuendesha huduma ya kanisa.” Lakini, mwangalizi KiBiblia, zaidi ya yote lazima we mtu mwenye tabia nzuri na aliyejitolea kwa Kristo, awe mtumishi wa kweli kwa sababu lengo lake ni kujizaa mwenyewe. Lazima aweze kuwaambia washirika wake, “Niigeni mimi, kama na mimi ninavyomwiga Kristo” (1Wakor. 11:1).
Kwa maelezo zaidi kuhusu nafasi ya mchungaji, soma pia maandiko yafuatayo: Matendo 20:28-31; 1Timo. 5:17-20; na Tito 1:5-9.
Nafasi Ya Shemasi
Mwisho, hebu tutazame kidogo habari za shemasi. Nafasi ya sehmasi ni nafasi nyingine katika kanisa la mahali ambayo si miongoni mwa zile karama tano za huduma. Mashemasi si kama wazee – wao hawana mamlaka ya kiutawala katika kanisa. Neno la Kiyunani diakonos ambalo limetafsiriwa shemasi maana yake ni “mtumishi” au “atoaye huduma”.
Wale watu saba waliochaguliwa kwa ajili ya kazi ya kuwalisha wajane wa kanisa la Yerusalemu kila siku ndiyo huhesabiwa kuwa mashemasi wa kwanza (ona Matendo 6:1-6). Walichaguliwa na kusanyiko na kupewa kazi na mitume. Wawili wao – Filipo na Stefano – walipandishwa cheo na Mungu, wakawa wainjilisti wenye nguvu sana.
Pia, mashemasi wanatajwa katika 1Timo. 3:8-13 na Wafilipi 1:1. Tena, inaonekana nafasi hii inaweza kuchukuliwa na mwanamume au mwanamke (ona 1Timo. 3:11).
Hiyo ni njia nyingine ya kusema hivi: “Kwa ajili ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo.”
Kama wanafunzi wa Yesu walitazamiwa kuwafundisha wanafunzi wao kutii kila kitu Yeye alichowaamuru, basi bila shaka wangewafundisha wanafunzi wao jinsi ya kufanya wengine kuwa wanafunzi pia, na kubatiza na kuwafundisha kuyashika yote ambayo Yesu aliamuru. Hivyo, kufanya wanafunzi, kubatiza na kufundisha wanafunzi ingekuwa amri inayoendelea, na inayofanya kazi kwa kila mwanafunzi aliyefuata.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni