Alhamisi, 27 Aprili 2017

WITO WA KARAMA ZA KUFANYA HUDUMA (4)

Mitume Wa Kweli Na Wa Uongo
Inaonekana kwamba baadhi ya watumishi siku hizi, kwa kutamani kuwa na madaraka juu ya makanisa, ni wepesi kujitangaza kwamba wameitwa kuwa mitume. Lakini wengi wao wana matatizo makubwa. Kwa kuwa hawajaanzisha makanisa (au labda wana moja au mawili) na hawana karama wala upako wa kiBiblia wa utume, inawabidi watafute wachungaji wepesi kudanganyika watakaowaruhusu wao kuwa na mamlaka juu ya makanisa yao. Kama wewe ni mchungaji, usidanganywe na hao mitume wa uongo wenye kujitukuza wenyewe na wenye njaa ya mamlaka. Wao kwa kawaida ni mbwa mwitu waliovaa mavazi ya kondoo. Mara nyingi wanachotafuta ni fedha tu. Maandiko yanaonya kuhusu mitume wa uongo yanasema; 
Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo (2Wakor. 11:13) 

Nayajua matendo yako, na taabu yako, subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana nawatu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; (Ufunuo 2:2). Kama inabidi wakwambie wao ni mitume, basi ni ishara kwamba wao si mitume. Matunda yao yanapaswa kuzungumza.
Mchungaji anayeanzisha kanisa na kuendelea kulichunga kama mchungaji kwa miaka mingi si mtume. Pengine wachungaji aina hiyo wanaweza kuitwa “wachungaji wa kitume” kwa kuwa walianzisha makanisa wenyewe. Pamoja na hayo, wasishike nafasi ya mtume kwa sababu mtume huendelea kuanzisha makanisa.
“Mishenari” aliyetumwa kweli na Mungu na kutiwa mafuta – ambalo ndilo jina la mitume siku hizi – mwenye wito wa kuanzisha makanisa, anaweza kusimama kama mtume. Lakini, wamishenari wanaofanya kazi ya kuanzisha shule za Biblia au kuwafundisha wachungaji si mitume bali waalimu.
Huduma ya kweli ya mtume huonekana kwa ishara na maajabu, ambavyo ni vyombo vinavyosaidia kuanzisha kanisa. Paulo aliandika hivi:
Kwa sababu sikuwa duni ya mtume walio wakuu kwa lolote, nijapokuwa si kitu. Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza (2Wakor. 12:11b-12).
Kama mtu hana ishara na maajabu katika huduma yake, yeye si mtume. Basi, mitume wa kweli si wengi, na hawapatikani katika kanisa bandia, lisilo takatifu, lenye kuhubiri injili bandia. Sana sana wanapatikana katika maeneo mapya kabisa duniani ambayo hajapata Injili bado.

CHEO CHA JUU CHA MTUME
Katika orodha zote za karama za huduma katika Agano Jipya, nafasi ya mtume hutajwa kwanza, kuonyesha kwamba ndiyo wito wa hali ya juu zaidi Biblia inasema "Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; (Waefeso 4:11)

"Na Mungu amewaweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha". (1Wakor. 12:28).
Hakuna mtu aanzaye huduma yake kama mtume. Mtu anaweza kuwa na wito wa mtume, lakini hataanza katika nafasi hiyo. Ni lazima kwanza ajithibitishe kuwa mwaminifu kwa miaka mingi katika kuhubiri na kufundisha, kisha hatimaye atasimama katika nafasi ambayo Mungu amemwandalia. Paulo aliitwa kuwa mtume toka tumboni mwa mama yake, lakini alifanya huduma kwa miaka mingi kabla ya kuingia katika nafasi hiyo hatimaye (angalia Wagalatia 1:15 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake"

Wagalatia– 2:1) 
"Kisha baada ya miaka kumi na minne, nalipanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami"

Alianza kama mwalimu na nabii 
Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Mfalme Herode, na Sauli (ona Matendo 13:1-2), 

ndipo baadaye akapandishwa cheo na kuwa mtume, wakati alipotumwa na Roho Mtakatifu 

(ona Matendo 14:14). 
"Walakini mitume Barnaba na Paulo, walipopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakapiga kelele."
Tunaona wengine wakitajwa kama mitume licha ya Paulo na wale Thenashara, katika Matendo 1:15-26; 14:14; Warumi 16:7; 2Wakor. 8:23; Wagalatia 1:17-19; Wafilipi 2:25 na 1Wathes. 1:1 na 2:6. (Neno mtenda kazi katika 2Wakor. 8:23 na Wafilipi 2:25 katika Kiyunani ni apostolos.) Hii hupingana na dhana iliyoko siku hizi kwamba nafasi ya mtume ilikuwa kwa ajili ya watu kumi na mbili tu.

Ila, ni mitume kumi na mbili tu wanaoweza kuhesabiwa kuwa “Mitume wa Mwanakondoo,” na ni hao kumi na mbili tu ndiyo watakaokuwa na nafasi ya pekee katika utawala wa Kristo wa miaka elfu moja (tazama Mathayo 19:28; Ufunuo 21:14). Hatuhitaji tena mitume kama Petro, Yakobo na Yohana ambao walivuviwa kipekee ili kuandika Maandiko, kwa sababu ufunuo wa Biblia umekamilika. Ila, sku hizi bado tunahitaji mitume watakaoanzisha makanisa kwa nguvu za Roho Mtakatifu, kama walivyofanya akina Paulo na wengine, kulingana na tunavyosoma katika Kitabu cha Matendo ya Mitume.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni