Alhamisi, 27 Aprili 2017

NAFASI YA HUDUMA YA NABII KATIKA KANISA (5)

Nafasi Ya Nabii
Nabii ni mtu anayepokea mafunuo ya Mungu na kusema kwa upako wa Mungu. Kwa kawaida, anatumiwa mara kwa mara katika karama ya kiroho ya unabii pamoja na zile karama za ufunuo: neno la hekima, neno la maarifa, na kupambanua roho.
Mwamini yeyote anaweza kutumiwa na Mungu katika karama ya unabii kama apendavyo Roho, lakini hiyo haimfanyi kuwa nabii. Nabii kwanza kabisa ni mtumishi anayeweza kuhubiri au kufundisha kwa upako. Kwa kuwa nafasi ya nabii inaonekana kuwa mwito wa pili (ona orodha katika 1Wakor. 12:28) "Na Mungu ameweka wengine katika kanisa wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu...," hata mtumishi wa kudumu asingeweza kutiwa katika nafasi ya nabii mpaka awe katika huduma kwa miaka kadhaa. Inapofikia wakati wake kushika nafasi hiyo, atakuwa na vitendea kazi vya kiroho vinavyoambatana na nafasi yenyewe.
Watu wawili wanaotajwa katika Agano Jipya kuwa manabii ni Yuda na Sila. Tunasoma katika Matendo 15:32 
"Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha".
kwamba walitoa unabii mrefu kwa kanisa la Antiokia, kama ifuatavyo:
Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha.
Mfano mwingine wa nabii kutoka katika Agano Jipya ni Agabo. Tunasoma hivi katika Matendo 11:27-28:
Siku hizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia. Na tulipokusanyika, akasimama mmoja wao jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio.
Ona kwamba Agabo alipewa neno la hekima – kitu kuhusu wakati ujao kilifunuliwa kwake. Agabo hakujua kila kitu ambacho kingetokea katika siku zijazo, ila alifahamu yale tu ambayo Roho Mtakatifu alipenda kumfunulia.
Katika Matendo 21:10-11, kuna mfano mwingine wa neno la hekima kufanya kazi katika huduma ya Agabo. Hapa, ilitokea kwa ajili ya mtu mmoja, Paulo.
Basi, tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. Alipotufikia, akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, “Roho Mtakatifu asema hivi, ‘Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa’.”
Je, Maandiko yanaruhusu katika kipindi hiki cha agano jipya kutafuta ushauri binasi kutoka kwa manabii? Hapana. Sababu ni hii: Waamini wote wana Roho Mtakatifu ndani yao ili kuwaongoza. Nabii anachoweza kufanya ni kuthibitisha tu kile ambacho mwamini tayari anajua ni mwongozo wa Mungu katika roho yake. Kwa mfano: Wakati Agabo alipomtabiria Paulo, hakumpa mwongozo kwamba afanye nini. Alithibitisha tu kile ambacho Paulo alikwisha fahamu kwa muda mrefu.
Kama tulivyokwisha kusema mapema, Paulo alishika nafasi ya nabii (na mwalimu) kabla ya kuitwa katika huduma ya utume (ona Matendo 13:1). Tunajua Paulo alipokea mafunuo kutoka kwa Bwana kulingana na Wagalatia 1:11-12, na pia alipata maono mengi tu (ona Matendo 9:1-9; 18:9, 10; 22:17-21; 23:11; 2Wakor. 12:1-4).

Kama ilivyo kwa habari ya mitume wa kweli, hatupati manabii wa kweli katika kanisa la uongo. Kanisa la uongo huwaepuka manabii wa kweli kama Sila, Yuda au Agabo. Sababu ni kwamba manabii wa kweli wataleta ufunuo wa Mungu kutopendezwa na kutokutii kwao (kama Yohana alivyofanya kwa makanisa mengi ya Asia Ndogo katika sura mbili za kwanza za Ufunuo). Kanisa la uongo halipendi hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni