Jumapili, 20 Agosti 2017

ASILI YA IBADA YA MWANADAMU



Kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu ni ushirikiano (fellowship) Biblia inasema,

“Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu ;wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na wanyama, nan chi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” (Mwanzo 1:26-27).

Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”. (Mwanzo 2:7).

“Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akaufunika na nyama mahali pake”. (Mwanzo 2:21)

“Kisha wakasikia sauti ya Bwana mungu akitembea bustanini wakati wajua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone BWANA Mungu akamwita Adamu Akamwambia, uko wapi?  Akasema Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha (Mwanzo 3:8-10)
Katika ushirikiano huo ndiko tunapata chimbuko la ibada ya mwanadamu. Mungu hawezi kufanya Ushirika na mwanadamu katika asili ya mwili moja kwa moja, hii ni kwa sababu Mungu yeye ni ROHO. kwa hiyo Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake. Na mfano huo upo katika ROHO. Ushirika wetu na Mungu uko katika ROHO, na kwaRoho tunafanana na Mungu.

“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi yenye uhai, mtu akawa nafsi hai”. (Mwanzo 2:7.)

Mwili ni nini?
-     Mwili ni nyumba au makao, ya roho.
Roho ni nini?  
-     Roho ni pumzi ya Mungu yenye uhai,

Ili kwa huyo Roho Mungu ajidhihirishe kwa ulimwengu katika ufahamu wetu. Yaani mwili ambao ni mavumbi. Katika msingi huo kusudi la Mungu kutuumba linatimia. Yapo makusudi makuu mawili ambayo ni:-
1.         Kumtumikia 
2.         Kumwabudu.
Mwanadamu awaye yote asiyefanya mambo hayo mawili amekosea lengo na kusudi la asili ya kuumbwa kwake.

Katika mambo haya mawili, wajibu wa kwanza ni kuabudu, yule unayemwabudu hatimaye unamtumikia na kuyakubali matakwa yake kwa kumtumikia.


Wajibu wa kwanza wa Adamu ulikuwa ni kuabudu na siyo kuhubiri ama kufanya huduma zingine, Mungu alikuja katika ibada wakati wa jua kupunga jioni ili kufanya ushirika nao.
-     Kuhubiri neno ni matokeo ya anguko la Adamu kumuasi Mungu na kuacha wajibu wake wa ibada na Mungu.
-     Msingi mkuu wa mahusiano ni Ibada. (Mwanzo 3:8) unasema wakasikia sauti ya Mungu akitembea bustanini.
Hii inaonyesha kwamba Adamu alikuwa na ushirika na Mungu kiasi cha kuzijua hatua za Mungu alivyotembea ikiwa ni ushahidi wakutosha kwamba walikua na ushirika mzuri.

Asili ya kuabudu
Kuabudu asili yake ni mbinguni, Kuabudu kulikuwepo kabla ya Adamu kuumbwa. Maana walikuwepo viumbe kabla ya Adamu huko mbinguni waliomwabudu Mungu.
Ibada ina asili katika Mungu mwenyewe, Uungu una asili ya kuabudiwa kwa hiyo chanzo cha ibada ni Mungu.
“Ulikuwa wapi nipoweka misingi ya nchi? Haya! Sema kama ukiwa na ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nanialiyenyoosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni. Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?”. (Ayubu 38:4-7)

Pia ukiangalia kitabu cha Zaburi 148:2-14. Unaweza kuaona malaika wanamwabudu na kumsifu Mungu.  Mstari wa 5 zaburi 148 unaonyesha agizo la Mungu akiagiza viumbe vyote kumwabudu na kumsifu kutoka mbinguni mpaka duniani, kuanzia viumbe vyenye uhai na visivyo na uhai kama ifuatavyo:-
Malaika na jeshi lake, Jua , mwezi na nyota zote, Mbingu na maji ya mbingu. Mstari wa 5 viumbe visivyoonekana Nchi yaani uumbaji wake wa dunia Samaki wa baharini Moto, mvua, theluji na mvuke, upepo na dhoruba Milima, na miti , wanyama wa porini na wakufugwa, Wadudu na ndege wa angani. Wafalme na watu wakubwa kwa wadogo wazee na watoto
Hawa wote wanaamuriwa kulisifu Jina la Bwana, Jina Pekee lililotukuka lenye adhama juu ya mbingu na nchi. Hii ni amri ya milele ambayo haitapita.

Midundo ya shangwe za malaika na mirindimo ya ibada hiyo ikaijaza mbingu wakati Mungu alipoumba ulimwengu. Malaika waliimba na kushangilia kazi ya uumbaji.

Imekuwa ni shauku ya Mungu kutaka ushirikiano huu wa ibada na viumbe vyake alivyoviumba, tangu hapo na mpaka milele katika mbingu mpya na nchi mpya, ambayo ni masikani yake pamoja na mwanadamu.

“Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani pamoja nao.” (Ufunuo. 21:3)

Jambo hili linafunuliwa na kufafanuliwa kwa ufasaha na Yesu alipomwambia mwanamke msamaria pale kisimani
“Lakini saa inakuja nayo sasa ipo ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika Roho na kweli” kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu, Mungu ni Roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na Kweli”. (Yohana 4:23-24).

Mungu anamtafuta mtu atakayemwabudu
Kwa nini? 
Kwa sababu anataka ushirika na mwanadamu Ili aufurahiye Upendo wa mwanadamu aliyemuumba kwa mfano wake na kutimiza kusudi lake la ushirika. Kuabudu katika Roho na Kweli huo ndiyo ushirika ambao Mungu anautafuta kwa mwanadamu. Kwa kuwa Jawabu la moyo wa Mwanadamu, ni kuwa na ushirika ambao unamgusa Mungu, na kumtukuza Mungu kwa roho yake yote.
Kumfurahia Mungu pasipokuwa na kitu kingine zaidi ya Mungu moyoni mwake. Kufanya uamuzi wa kumpenda Mungu kuwa ni jambo la milele. Ibada siyo kitu cha muda mfupi bali ni shughuli inayo endelea milele na milele kati ya mwanadamu na Mungu. Biblia inamnukuu Mariamu akisema,

“Mariamu akasema moyo wangu wamuadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, mwokozi wangu; Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake, kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa”. (Luka 1:46-47)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni